SoC02 Tuurejeshe upendo uliopoa

SoC02 Tuurejeshe upendo uliopoa

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 27, 2022
Posts
94
Reaction score
134
UPENDO ULIOPOA

Kuna aina nyingi za upendo ambazo binadamu tunajihusisha nao. Kwa sasa upendo ninaoutamani urejee ni ule upendo usio na sababu,upendo unaojali na kuthamini mazingira yote. Upendo unaothamini na kurejesha ubinadamu.

Tujaribu kurejea maisha ya zamani yale ya mtoto wamjomba kulelewa ama kusomeshwa na shangazi, tunakumbuka namna familia zetu zilikuwa zinapokea wageni wa familia, ukoo ama jirani zetu wa kule kijijini tulipotokea?

Kuna namna tulikuwa tunasaidiana kwa moyo na upendo wa dhati kabisa bila hata kuifikiria hali yetu ya kiuchumi. Nakubali kabisa maisha yamebadilika kulingana na sababu mbalimbali za maendeleo ya sayansi na teknolojia ama mabadiliko ya kiuchumi na afya pia. Ila nadhani kilichopotea katika jamii yetu ya sasa ni upendo. Tumeupoteza ama umepoa sana baina yetu.

Kuna nyakati mama aliweza kwenda sokoni na kumuachia kijana wa kiume mtoto wa kike amlee pindi mama kaenda kuhemea mahitaji ya nyumba jambo ambalo kwa sasa halipo kutokana na kutokumuamini kabisa kijana yule labda kwa sababu ya matukio mbalimbali ambayo si ya kibanadamu tunayoyashuhudia katika jamii yetu sasa.

Tukumbuke nyakati ambazo mtoto wa jirani anaweza kuonywa na wazazi wa mtaa ama kijiji chote pindi anapoenda kinyume na maadili ya jamii husika jambo ambalo kwa sasa mtoto wako ni wako na si wa jamii.

MADHARA YATOKANAYO NA KUPOA KWA UPENDO

  • ONGEZEKO LA MATUKIO MAOVU KWENYE JAMII.
  • Kuna matendo engi maovu yapo kwenye jamii yetu kutokana na ukosefu wa upendo. Mfano kwa sasa kusikia kaka kamlawiti dogo wake ni jambo lililokithiri mno kwenye jamii, baba mzazi kumbaka na kumpa ujauzito binti ni aibu inayobebwa pia na baadhi ya familia zetu. Imefikia sasa ni ngumu kumuachia mtoto wa kiume amlee mdogo wake ama mjomba kuwalea mabinti wa shangazi maana ataupanda mtarawanda bila jamii kufahamu mapema hadi pale madhara makubwa yanapomfika binti ama kijana.

  • KUTENGENEZA TAIFA LISILORITHISHA MAARIFA KWA VIZAZI VIJAVYO
  • Kutoweka kwa upendo huu kumetengeneza mazingira na roho ya uchoyo wa maarifa kwa kuamini kila tulifanyalo ni lazima lihusishe fedha kwa maana kwamba hakuna ujuzi unaorithishwa hata katika ngazi ya familia kwa kuamini kwamba anayerithishwa ujuzi huo atamzidi maarifa mrithishaji jambo ambalo kwa mtazamo wangu naona ni chanzo cha kutengeneza Taifa lisilo na urithi wa busara na maarifa ya waliotangulia kuona jua.

  • KUCHELEWESHA MAENDELEO ENDELEVU
  • Ukosekanaji wa upendo hupelekea jamii kutokufikia maendeleo endelevu kwa haraka maana penye uhitaji wa maendeleo endelevu huhitaji ushirikianao. Hakuna jambo linaloweza kufanywa kwa wingi na haraka bila kuwa na ushirikiano na hakuna ushirikiano uanodumu bila kuwepo upendo.

  • ONGEZEKO LA WATOTO WASIO NA MAKAZI MAALUM
  • Ile jamii ya kumfanya mtoto wa mwingine ni wangu imepotea, upendo umeitokomeza jamii hii ambapo binadamu yupo radhi ale chakula asaze amwage huku jirani yake amekosa kikombe cha uji na pengine watoto wengi wa familia hizi hupita mitaani kujitafutia chochote cha kuweka tumboni ili siku ipite. Watoto hawa wanaokosa makazi wengi hutoka katika familia zenye changamoto nyingi ama wamepoteza wazazi. Ila waliopoteza wazazi ukute kuna ndugu kwenye familia ama ukoo wao na hakuna anayeweza kujitolea kushirikiana nao katika makuzi na malezi yao kabisa jambo ambalo hujikuta wakitafuta faraja kutoka jamii barabarani ambapo pia huchukuliwa tofauti na haja zao.


TUNAWEZA KUYAELEKEZA MACHO YETU KATIKA MAMBO YAFUATAYO ILI TUUREJESHE UPENDO ULIOPOTEA;

  • Tushirikishe vizazi vyetu elimu sahihi juu ya upendo usio na sababu yaani upendo umee mioyoni mwao ambao tafsiri halisi ya upendo haitaangalia wingi ama uchache wa umiliki wa vitu ama pesa.
  • Tuwafundishe watoto wetu kuuthamini utu ambao hapa kila mmoja atajiona kwenye macho ya mwengine na kuchukua kila changamoto ama mafanikio ya mwenzie ni yake pia. Kulia na wnaolia na kucheka na wanaocheka.
  • Tukiweza kutengeneza kizazi kinachojiweka kwenye nafasi za wengine ni rahisi kabisa kutengeneza familia zenye upendo, zisizo na unyanyasaji, unyanyapaa na dhuluma na kila aina ya uonevu.
  • Kusaidia mfumo mzima wa elimu kutafuta namna ya kufundisha upendo na ushirikiano katika taasisi zote za Elimu. Hii itasaidia umimi na huweza kuleta ushirikiano miongoni mwa wanafunzi na inaweza kuleta mbadiliko chanya ya ujifunzaji na ufundishaji.
  • Tunaweza kuyafanikisha yote haya endapo tunaanza mabadiliko haya kwa kujipenda na kujikubali sisi wenyewe. Kwa mfano; binadamu anahitaji urafiki na binadamu mwingine, haswa tukiangalia katika Nyanja hii ya mitandao ya kijamii. Binadamu huyu anaanza kwa kutokuwa muwazi kwa rafiki anayehitaji awe rafiki yake, anaweka picha isiyo halisi, amatumia jina lisilo lake na inawezekana akampa taarifa za uongo huyo rafiki mpya, watu hawa wanaweza kuwa marafiki lakini pia ukweli ukidhihirika wanaweza kuwa maadui pia. Hapa naamini mno kwamba upendo huenda sambamba na ukweli. Ukiwa mkweli maana yake umejipenda na kumthamini mwingine pia.

  • Kwa namna ambayo tunaweza kutengeneza kizazi kipya chenye mtazamo chanya, mabadiliko yaanze na mimi na wewe yaani sisi tukibadilika, tuna uwezo mkubwa wa kubadilisha vizazi vyetu na vizazi vyote vijavyo. Tusipokubali kushirikiana katika mabadiliko haya bado tutaendelea kukumbatia maovu mengi baina yetu, bado tutaficha ualifu mwingi miongoni mwetu, bado tujimilikisha na kujilimbikizia vingi wakati kuna ndugu zetu waliopembeni yetu ambao wanahitaji mengi mno kuliko uroho na uchoyo uliokithiri miongoni mwa walimbikiz mali.
Mwalimu Demitria Thomas Gibure.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom