Mramba,Yona na mafisadi wengine kweli wamepelekwa mahakamani lakini bado hawajahukumiwa. Hata hatufahamu hatima ya mali zao ambazo wamezipata kwa njia za kifisadi.Lakini wapo pia mafisadi wengine wengi ambao bado wako mtaani wanatanua huku wakitung'ong'a.Wengi tunawajua ingawa serikali hii ya ajabu inasema haiwajui ingawa ina vyombo vyote vya usalama.Sijui hata kitengo cha usalama kina kazi gani, nadhani kimepoteza maana kabisa.Kingevunjwa tu,kwa vile kinapoteza bure hela ya walalahoi.Katika hali hii tutafanya makosa kabisa kuanza kuipongeza serikali katika hatua hizi za awali kabisa.Ni vema tukasubiri mpaka wale wote wenye tuhuma wafikishwe mahakamani,wahukumiwe na kufilisiwa.Wote tunaifahamu historia ya serikali yetu.Ni ya kibabaishaji mno.Hatuna shaka kabisa kwamba shutuma dhidi yao ni za kweli kabisa.Kipato chao cha halali kisingewafanya wawe matajiri wa kutupwa kiasi hicho.Tunaisubiri serikali.