Itakuwa ni kujidanganya mchana kweupe kuwa hali ya kisiasa nchini ni shwari na kuwa kazi inaendelea.
Kufuatia mkutano wa Msajili na wadau wa Siasa kuna habari ya timu (Task Force) ya watu 10 kufanikisha kufikiwa kwa maazimio takriban 80 yaliyoafikiwa kama ilivyoripotiwa.
Fahari ya macho haifilisi duka. Si haba kuwafahamu wajumbe wa tume hii ili kuendelea kufahamiana zaidi katikati ya sintofahamu zilizopo.
Kama vipi kuwafahamu wajumbe majina, wasifu, mafungamano yao kisiasa, nk, ingependeza zaidi.
Inasemekana kuwa katika timu hii, waheshimiwa hawa wamo:
(a) Profesa Rwekaza Mukandara (REDET)
(b) Dean Fupe (KKKT)
(c) Sheikh Alhad Mussa (BAKWATA)
(d) Dr. Edward Hosea (TLS)
"Lisemwalo lipo kama halipo waungwana wanasema linakuja nyuma."
Kongole kwao.
Kwamba watu hao 10 ni kutokea kwenye mchanganuo huu:
1. Mwandishi wa habari........Pascal Mayala
2. Jaji mstaafu..........
3. Mwanaharakati nguli.......Cyprian Musiba
4. Kiongozi wa dini (Mkristo).........Gwajima
5. Kiongozi wa dini (Muislam) ....Sheikh wa dar
6. Kiongozi mstaafu (chama cha upinzani)....Dk Slaa
7. Kiongozi mstaafu (chama tawala)....Wasira
8. Mhadhiri vyuo kikuu...Bana
9. Mkulima.....Aliyegombea urais CCM 2015
10. Mjasiriamali.......Mange
Timu haitakuwa tofauti sana na hiyo, Majina yanaweza badilika lakini tabia za wajumbe zitafanana na za hap.
NADHANI KUNA NAMNA CCM WANATUONA WABONGO MISUKULE.