Tuwaheshimu wazazi/walezi wetu ila tusiwasulubu wajukuu zao kwa jinsi walivyokuwa wakitupiga kikatili

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Tukiachilia mbali ulaji wa ugali jambo lingine ambalo lina mchango mkubwa kwenye ujinga na umaskini wetu ni kujengewa hofu kuanzia utotoni. Wengi wetu tumejaa hofu hatuna uhuru kabisa wa matumizi za akili na vipaji vyetu. Sababu za kuwa hivyo ni nyingi ila kwa leo nitagusia kwa ngazi ya familia.

Huu uzi nimeuandika baada ya kuona watu wengi wakimtetea mama aliyerekodiwa akimpiga kikatili mwanae. Utetezi wao wa kipumbavu ni kuwa eti wao walivyokuwa wadogo walikuwa wakipigwa mno kuliko hata huyo mtoto videoni. Wengine walienda mbali kwa kudai hadi makovu ya vipigo hadi leo wanayo. Huu ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu mno. Ndo maana wengi wetu tunaishia kuwalaumu viongozi huku tukisahau kuwa hata sisi tuna mchango mkubwa kwenye huu umaskini wa taifa.

Nchi ilipaswa iwe na kina Diamond, Filbert Bayi, Dr Janabi, Samatta na mabingwa wengine wa tasnia mbalimbali ila kwa sababu ya ujinga wa wazazi wengi kutengeneza hofu kwa watoto kupitia vipigo waliishia kuua ari ya watoto kukuza vipaji vyao. Zamani mtoto ukikutwa hata umewasha redio mkulima kipigo chake ni balaa. Na wale wafia dini hutumia mstari wa biblia usemao "usimnyime mtoto mapigo" kuhalalisha upumbavu wao.

Ninatoa wito kwa wazazi/walezi kuadhibu watoto kwa kiasi na sio kushindwa ku-control hasira na kufanya ukatili. Nyakati zimebadilika. Hizi simu zenye camera zinaweza kukutia matatizoni ingawa mtoto ni wako.
 
Fact

Hiyo hofu tuliojengewa ndo imesababisha watu kuwa kujiingiza katika UCHAWA wa vyama vya siasa n.k
 
Back
Top Bottom