Tuwakumbuke Mastaa Waliowahi Kutamba Pamba Fc ya Mwanza

Tuwakumbuke Mastaa Waliowahi Kutamba Pamba Fc ya Mwanza

Wengi wametajwa ila naongeza , Ibrahim Magongo, Alphonce modest (namba 3 bora ya muda wote), John Makelele, Khalifan Ngasa (baba wa Mrisho Ngasa) bila kumsahau superdupa coach Pius Nyamko r.i.p
 
Hivi Pius Nyamko alikuwa mkongo kweli?
Aliyekuwa Mkongo, jina lake nimelisahau, ila alikuwa maarufu kwa jina la "BATALOGOTA BENYEWE KUNYAVU!"
Jina hilo lilitokana na MAJIGAMBO yake kuwa timu zitakazokutana na Pamba, zitakuwa na kazi moja tu, kuokota mipira kwenye nyavu baada ya kufungwa magoli!
 
Pamba ya miaka ile ilikuwa inacheza kwa kujiamini sana. Walikuwa wakimiliki mpira hata ukiwa golini mwao walikuwa hawana papara nao, watausukuma step kwa step hadi ufikie goli la mpinzani. Yanga na Simba walikuwa wakienda Mwanza lazima warudi wakiwa wamefungwa.
 
Back
Top Bottom