Uchaguzi 2020 Tuwakumbushe wanaowania Urais 2020

Uchaguzi 2020 Tuwakumbushe wanaowania Urais 2020

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Uchaguzi Mkuu Tanzania ni mwaka huu wa 2020, bila shaka wako watanzania wenzetu watapenda kuwania kiti cha Urais wa Tanzania. Sisi wasaka tonge tuna yetu mengi ya kuwaambia wenzetu wenye ndoto za kuwa Rais wa nchi hii.

Hebu kwa njia hii tuwakumbushe wenzetu hawa mambo gani wayafahamu kabla na baada ya kuupata urais.

Mfano, mimi ninayo machache ambayo kila muwania urais lazima ayatambue:

1. Hakuna msaada kutoka kwa yeyote utakaosaidia kuijenga nchi yetu vile tunavyotaka iwe. Hivyo ufikirie namna ya kuiendesha nchi bila kutegemea misaada ya wahisani.

2. Ukoloni bado upo kwa kutumia mbinu nyingi tofauti. Zile sababu zilizowafanya wakoloni waje Tanzania kwenye miaka ile bado wanazo hata leo hii. Hivyo fikiria mapema namna utakavyokabiliana na ukoloni mamboleo.

3. Elimu ndio inayoweza kuwakutanisha watoto wa matajiri na wale wa masikini. Elimu nafuu kwa kila mtanzania ni lazima sio hiari.

4. Taifa haliwezi kujitegemea kama watu wake hawana nguvu kubwa ya kufanya manunuzi ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi. Hivyo fikiria sasa namna utakavyowajaza hela wananchi ili waweze kufanya manunuzi na kulipa kodi.

5. Afya njema kwa wote. Fikiria mapema namna watu wote watakavyopata matibabu, maji ya kunywa, makazi na usafiri.

6. Usalama wa nchi: Nchi zinazotuzunguuka zina silaha kubwa kiasi gani?

7. Demokrasia na utawala bora kwetu ni haki sio hisani, kufungana midomo sio poa. Mhakikishie kila mtu haki ya kuiona kesho akiwa salama.

8. Ikulu sio pango la walanguzi, uwe na uwezo wa kuwaambia ndugu na marafiki zako wasikutumie kufanikisha maovu yako.

9. Ukabila, ukanda na udini usivirudishe nchini tena, utagombana hata na Mzee Nyerere, RIP ukifanya hivyo.

10. Uhusiano mwema na mataifa mengine unapunguza gharama za kujilinda.
 
Back
Top Bottom