Tuwalazimishe viongozi wetu kuwa wazalendo na kuishi wanayoyaongea jukwaani

Tuwalazimishe viongozi wetu kuwa wazalendo na kuishi wanayoyaongea jukwaani

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Wananchi wengi bado wako usingizini na ni wazito sana kuwahoji viongozi.

Kama ilivyo vigumu kwa muumini wa dini kumnyooshea kidole kiongozi wake wa kiimani/kiroho anapofanya kinyume na anayohubiri imekuwa vigumu na sisi kuwawajibisha viongozi waishi wanayoyasema.

Leo viongozi wetu wako bize kuhubiri a wazazi wasitoe michango mashuleni kwasababu serikali sikivu inatekeleza mpango wa elimu bure.

Maskini Wanajamii wangu hata hawakumbuki kuuliza maswali ya msingi;

1. Siku hizi viongozi hawana watoto? Kama wanao mbona hawasomi na watoto wao!? Au wao hawataki kule mema ya nchi?

2. Kama serikali imejenga shule nzuri kweli mbona watoto wao wanasoma shule ambazo hazikujengwa na serikali? Ina maana serikali haijui kujenga shule vizuri hadi watamani watoto wao wasome shule zilizojengwa na watu baki?

Maswali Kama hayo wayaulize upande wa huduma za afya pia.

Kama tunavyokutana na mawaziri, ma DC, RC, wabunge, wakurugenzi, madiwani na wengineo kwenye nyumba za ibada hivyo hivyo na iwe mashuleni na vituo vya afya.

Siku tukiamka na kuanza kulidai hili na wakaona kweli tunamaanisha, madai ya katiba mpya yatachuku siku 3 kutekelezwa.

Wanajua bado wengi wako usingizini ndiomaana wanafanya haya.

Amkeni, Amkeni Amkeni...inawezekana watoto wenu kula shuleni endapo na wa kwao watakuwemo.

Inawezekana watoto wenu kukalia madawati endapo na wa kwao watakuwemo.

Inawezekana watoto wenu kusoma kwenye maabara zenye vifaa endapo na wakwao watakuwemo.

Inawezekana watoto wenu kufundishwa na walimu wenye morali ya kazi endapo na wa kwao watakuwemo.

Wakija kusema elimu ni bure, waulizeni watoto wao kwanini hawasomi shule za bure?

Wakiwaambia hakuna kutoa mchango shuleni, waulizeni na watoto wao wanashinda njaa Kama wa kwenu? waambieni wapeleke na fedha za chakula na wapishi angalau watoto wenu wanywe uji tu inatosha maana huwezi kusoma na njaa.

Mwisho muwaulize, watoto huko wanakosoma wanakaa chini Kama wa kwenu? Na wanarundikana madarasani Kama wa kwenu?

Mwanao atakapokosa nafasi kwasababu ya ufaulu mdogo, kushindwa kujieleza vizuri au kukosa "connection" tambua kabisa aliyemtenga na hivyo vitu muhimu ni wewe kumsikiliza kiongozi wako aliyekuhubiria asiyoyaishi.

Waswahili husema, "ukitembea na waridi utanukia uaridi."
 
Back
Top Bottom