MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Mutuombee…’’ majaji watoa wito huo wanapojitayarisha kutoa hukumu yao
Maelezo ya picha.
Majaji wa Mahakama ya Juu Zaidi watatoa uamuzi wao Jumatatu 3 Septemba 2022.
Kusikilizwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya urais kumekamilika Ijumaa huku Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu akitoa ombi la kuwaombea majaji wanaporejea kufanyia kazi kuandika na kutoa uamuzi wa kesi hiyo.
“Mutuombee tunapoanza awamu inayofuata. Sio sehemu ngumu sana lakini inahitaji umakini wa hali ya juu na kwa sababu hiyo tunakuomba utuombee Mungu atusaidie tuendelee katika ari ile ile tuliyokuwa nayo katika mwaka mmoja uliopita na tuwe na utambuzi wa hali ya juu sana, tutarudisha kwa Kenya hukumu ambayo si tofauti na kile ambacho Wakenya wanatarajia,”
Mwilu alisema.