Tuwape maua yenu Mahakama ya Rufani Tanzania

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
331
Reaction score
416
Anayestahili kupongezwa basi na apongezwe! Ni jambo dogo lakini nasukumwa kuwapongeza wafanyakazi wa mahakama ya RUFANI TANZANIA hasa kitengo Cha kupokea simu.

Kutopokea simu au kutojibu barua za wananchi ni jambo la kawaida Kwa taasisi za serikali Tanzania. Ni KERO kubwa inayoongeza ugumu wa maisha.

Utalazimika kusafiri hata Kwa jambo dogo. Ni taasisi chache sana za serikali ndiyo wanaopokea simu au kujibu barua.

Mimi siishi DSM wala Dodoma nikiwa na jambo ambalo siyo lazima kusafiri naitafuta namba kwenye mtandao napiga simu, lakini ukweli ni kwamba simu Huwa hazipokelewi. Mna shida Gani nyie watu wa vitengo hivyo serikalini?

Lakini Nimejaribu mara nyingi kupiga simu MAHAKAMA YA RUFANI ukweli wanapokea simu! Inatusaidia sana tunaoishi mbali na huo mji wenu. Mimi Leo niwashukiruuu nawapongeza.
 
Barua Zama hizi? Kweli sisi bado
 
Pongezi kwao
 
Hongera kwa uungwana!
 
Mahakama ni kutenda haki, hjaya mengine ni cosmetics. Msalimie Mwambegele
 
Mahakama ni kutenda haki, hjaya mengine ni cosmetics. Msalimie Mwambegelel

Mahakama ni kutenda haki, hjaya mengine ni cosmetics. Msalimie Mwambegele
Haki ni pamoja na kusikilizwa (natural justice). Kama simu tu wangekuwa hawapokei hayo mengine tungejuwaje wanatutendea haki! Mwambegelel Yuko vizuri hasa ukisoma hukumu zake anaonesha weledi mkubwa katika taaluma.
 
Kongole kwao.

Mda sio mrefu watakwambia "Mkono mtupu haulambwi"

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…