Tuwapigie kura wasanii wetu kwenye MVP Music Award tulete tuzo Bongo

Tuwapigie kura wasanii wetu kwenye MVP Music Award tulete tuzo Bongo

sundoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
2,067
Reaction score
2,759
Kumekuwa na ukame wa Tuzo za mziki Africa hapa bongo. Na hii imetokana na kutokupiga kampeni za kutosha kuwapigia kura wasanii wetu. Sasa kuanzia leo tunaamua kuleta bongo kila tuzo za Africa na dunia. Tuanze na hii!

Hizi ni tuzo kubwa huko Nigeria. Turudishe heshima ya Tanzania.

Kwa kuwa wasanii wetu wengine wako wawili kwenye kipengele kimoja tupange tumpigie nani kura kila kipengele ili tusigawanye kura na tukashindwa kuchukua tuzo.

Vipengele:
*BEST MALE*
Hapa yupo Harmonize na Diamond. Tumpigie HARMONIZE kwa kuwa Diamond yupo kwenye vipengele vingine vingi.

*BEST FEMALE*
Tumpigie Maua Sama. Yupo peke yake toka Tz na East Africa

*BEST HIP HOP*
Hapa hakuna mbongo. Tumpe Khaligraph Jones mkali jirani yetu toka Kenya.

*BEST POP*
Tumpigie *Diamond Platnumz* yupo peke yake toka Tz na East Africa

*BEST COLLABORATION*
Hapa kuna JIBEBE na KATIKA. Tuipigie kura KATIKA YA NAVY KENZO kwa kuwa Diamond bado yupo kwenye vipengele vingine vingi. Isitoshe na kwenye KATIKA yumo

*DIGITAL ARTIST OF THE YEAR*
*Tumpigie Diamond Platnumz.* Hapa yupo peke yake kutoka Tanzania & East Africa

*BEST GROUP OF THE YEAR*

Tuwapigie Navy Kenzo

*SONG OF THE YEAR*
Hapa kuna *African Beauty ya Diamond*, na kuna *KWANGWARU* ya Harmonize na Diamond. Tuipigie *KWANGWARU* maana itapata kura nyingi zaidi toka nchi nyjngine za Africa kwa kuwa mpaka sasa ndo most viewed African music video kwa 2018. Na pia Diamond yumo

*BEST NEW ARTIST*
Tumpigie MBOSSO. Yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*LISTENERS' CHOICE*
Hapa ipo KATIKA ya Navy Kenzo na KWANGWARU ya Harmonze na Diamond. Tuipigie KATIKA ya Navy Kenzo maana KWANGWARU tushaipigia hapo juu

*AFRICAN PRODUCER OF THE YEAR*
Tumpigie NAHREEL yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*AFRICAN ARTIST OF THE YEAR*
Tumpigie *Diamond Platnumz* yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*JINSI YA KUPIGA KURA*
Click hii link
Soundcity MVP Awards Festival – Nominees are… Vote Now

Utakutana na vipengele vya tuzo zenyewe na majina ya wasanii husika (Nominees) gusa msanii unayempigia kura. Kura nu mara 1.

Tuache team zisizokuwa na maana. Tulete tuzo nyumbani.

*SAMBAZA KWA GROUPS ZAKO ZOTE*
 
MSANII WA KWANZA NTAEMPIGIA KURA NI HUYU KWENYE AVATAR (motigbana ndo ng0ma kali 2018) afu nakuja kwa mkuu wa kaya m0ndi
 
Mpigieni kula Mbosso wazee kwenye new artist of the year... Kijana ana deserve
 
Mbona kiba100 hayupo???.. daah kweli hapendagi show off
 
Back
Top Bottom