Tuwapongeze TFF kwa Video Support kwenye ligi, So far so good

Tuwapongeze TFF kwa Video Support kwenye ligi, So far so good

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Inakera sana makosa ya kibinadamu yakitumika kudhoofisha jitihada za timu, makocha na wachezaji kuwekeza kwenye ushindi wa timu kiwanjani.

🇹🇿 Tanzania’s Premier League is now using FVS (Football Video Support).Tanzania becomes the fi.jpg

Football Video Support (FVS) kwenye ligi ya NBC mpaka sasa imeleta utulivu wa hali ya juu. Kelele juu ya waamuzi mpaka sasa hazijasikika au ziko kwenye low mode. Tumsifu rais Karia na TFF kwa uthubutu huu.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni akiwa bado hai anahema. Binafsi namuona akiwa Rais wa CAF huko mbeleni.

Waliozoea vya kunyonga lazima watasikika wakiiponda FVS kwa sababu za hapa na pale. Mungu ibariki Tanzania ibariki TFF kupunguza makosa ya kibinadamu kwenye ligi yetu.

Simba na Yanga zitauchukia mfumo very soon kwakuwa ya tabia zao dhidi ya timu nyingine kwenye ligi.
 
Hakika ni za kwetu! Tarajia sababu za mifumo sio muda FVS itakufilia mbali, ili tupate bingwa wa mchongo iwe jua iwe mvua! (save my note)
 
Eeh kweli video support imepunguza sana hizo makeke za kibinadamu, ila bado kuna mechi za mkoani zinaendelea bila skrini na hapo ndio maafa. Ngoja tuone ligi itakavyomalizika, maana FVS ikiwa ipo kote ndio itakua fair kabisa. ngoma
 
Hakika ni za kwetu! Tarajia sababu za mifumo sio muda FVS itakufilia mbali, ili tupate bingwa wa mchongo iwe jua iwe mvua! (save my note)
Hasa pale mfumo unapozalisha red cards na penati kwa vigogo wa ligi.
 
Eeh kweli video support imepunguza sana hizo makeke za kibinadamu, ila bado kuna mechi za mkoani zinaendelea bila skrini na hapo ndio maafa. Ngoja tuone ligi itakavyomalizika, maana FVS ikiwa ipo kote ndio itakua fair kabisa. ngoma
mechi za mikoa wap na wap unapazunguzmia

jana mech ya coastal union fvs ilikuwepo mkwakwani

leo mechi ya simba na kagera kaitaba FVS ikikuwepo

unazingumzia mikoa ipi au ndo kukalili
 
Simba na Yanga zitauchukia mfumo very soon kwakuwa ya tabia zao dhidi ya timu nyingine kwenye ligi.
Simba SC ndio wanafuaika wakubwa wa makosa ya marefa 'makosa ya kibinadamu'. Mechi ya kwanza tu tayari wamepata kadi nyekundu, watauchukia sana mfumo wa FVS. Muda utasema.
 
Back
Top Bottom