Tuwapuuze wakosoaji vipepeo wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Tuwapuuze wakosoaji vipepeo wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Waziri Mkuu ni nafasi nyeti sana katika muundo wa kiutendaji, je katika muundo na mamlaka na uhuru wa kimamuuzi hasa autonomy kwa muktadha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikoje? katika nafasi hii. Ina nikera sana kuona kwamba Waziri Mkuu nchi hii ni nafasi inadharauliwa sana na haina heshima sana hasa katika dhana ya uhuru wa kimaamuzi na ushauri na utekelezaji wa majukumu, taasisi au mamlaka ya uteuzi ya nafasi hii ya Waziri Mkuu ni muhimu ikachakata sana sana independence ya kifikra, miongozo, kanuni, taratibu, miongozo, ubunifu, utekelezaji, ushirikishwaji na mengine. Hichi cheo cha Waziri Mkuu ni muhimu sana sana, Waziri Mkuu anapaswa kupewa meno na ukali wa meno hayo huletwa na mamlaka ya uteuzi kwa dhamira, matarajio, maelekezo, ya mamalka hio, kiranja anafuata kanuni za kiranja mkuu, mwalimu wa zamu, mwalimu wa nidhamu, na mkuu wa shule, na miongozo iliyopo.

Je Majaliwa huyu na yule wa Magufuli ni yule yule?
kwa nini, Majaliwa kama Mtu na kama kiongozi na kama mtoto wa Rwangwa ni yuleyule, dini yake, imani kabila lake. Tumtendee haki na kutenda haki ni wajibu- umpende usimpende haki na wajibu ni pande zote na kwa yeyote awaye yule.

Kama Majaliwa ameamua kufanya namna boss atakavyo ama hali ilivyo sasa ya mazingira ya kiutendaji livyo. aachwe adance na tune ya sasa katika utendaji.

Wanaotamani aitwe Sukuma Gang wamefeli huyu ni Mwera Og.

Wenye chuki waje na hoja zingine zenye mashiko yasiyo akisi nguvu ya kisheria na kimaamuzi.

Kama shida ni kwamba alikuwa na Magufuli, Je Mamlaka kuu ya sasa imetoka mbinguni au nayo ilikuwa na Magufuli, shida nini? anawazuia kula?anazuia msiweke nia ya kugombea urais? Tuache Ubazazi na Ufedhuri wa fikra zenye wivu wa kindoige ndoige.

Majaliwa hana meno na inafahamika cheo hiki hakina meno, meno ya waziri mkuu humarishwa na mamlaka ya juu yake, awamu hii ni wakati wa kutuliza joto, kupoza maumivu, kufungua nchi, kuleta mashirikiano, utulivu, kula kwa urefu wa kamba, mnataka Majaliwa awe anabwatuka wakati mamlaka kuu haibwatuki? na kutobwatuka sio kosa ni hulka na ni muundo pia na si dhambi.

Ufanisi ni pamoja na mzaingira wezeshi kama nyenzo, rasilimali, convinience, utayari wa kibajeti na allocation yake,

Rejea: Wenye Wivu Ndoige mnaobwatuka mnakumbuka ajali ya treni ya Dodoma iliua wangapi, MV Bukoba iliua wangapi? ajali za moto zimeua wangapi (Namba one na Morogoro), ajali ya Icelanders iliua wangapi, AirMsae iliua wangapi, Karanja Mbeya-Tukuyu iliua wangapi? na Majeruhi wapo mkitaka rejea zipo.

Acheni Kuzingua Cheo cha Waziri Mkuu hakino meno na uhuru huo wa ukali mnaoutaka na hata maamuzi ya kudetermine fate mnaoyataka nyie.

Kama machawa wanataka hiko cheo wachukue lakini si kwa hoja mfu na nyepesi ambazo hazina hata muktadha ya kuitazama nafasi ya waziri mkuu kimaamuzi.

Mmesahau Enzi za Pinda ishu ya Escrow alisema hadi amsubiri Rais Kikwete, na alikiri hana mamlaka ya kumwachisha mtu kazi, halafu huyo ndio mtendaji mkuu wa shughuli za serikali.

Bendera cheo ndio Uwaziri Mkuu wa Tanzania, Mshajiuliza kati ya Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi ni nani Katibu wa Cabinet Meeting? na kwanini iwe hivyo?

Majaliwa hajawahi kuwa kikwazo kwa mamlaka ya juu, ila kama wapambe au wakosoaji wanaona mambo yao hayawezi kufanikiwa bila kumtoa Majaliwa fanyeni yenu ila msilete visingizio mfu na vsiyo ona matobo katika mamlaka ya cheo hiki katika kusimamia na kuhukumu.

Mtawala mkuu ni mpole na haina ubaya na ni haki yake haina ubaya ila nae majaliwa aachwe na upole wake, nafasi ya waziri mkuu haina ubwete/uhuru huo wa kujiongeza kama mnavyofikiria nyie.

Wasilisho hili halina unazi, kutumwa, wala uchawa, bali kuitzama nafasi ya Waziri Mkuu na si Waziri Mkuu mwenyewe. Kama tunataka awe tunavyotaka basi na sheria na miongozo iweke nguvu ya kimamlaka ya uwajibishaji katika ofisi ya Waziri Mkuu iwepo.

Mimi sio shabiki yake Majaliwa ila nina haki na wajibu wa kumtetea na kumlinda panapo hukumu ahaukumiwe kwa haki na kwa dhamira njema.

Sina utimilifu wa aina iliyo tukufu, karibu kwa ukosoaji, marekebisho, na aina yoyote ya maoni.

Mods: naomba please hili andiko halina ubaya simsfii mlengwa wala kumtukana, dhamira ni kushawishi dhamiri njema na yenye hoja katika ukosoaji wa aina yoyote na ni muhimu kujenga muktadha na dirisha sahihi lenye kubeba hoja na utetezi wake.

Nawasilisha nikiendelea kutafakari mkinzano na ushabihiano wa kihoja kati Waziri wa fedha, wabunge mfano Profesa Muhongo, Mamlaka kuu, kuhusu uchumi wa kati wa chini.

CCM jengeni utaratibu wa private parliamentary dockets kwa baadhi ya mambo mnayo yaona hayahitajiki public access, lakini je, jambo lililosemwa na mamlaka ya uteuzi wa waziri wa fedha linaweza kuyeyusha point ya Muhongo, who misled the boss then?

Ni wakati gani aibu ni aibu na kwa nani, na wakati gani? inapotoka kwa nani?

Baraka njema na iwe nasi sote.

Shukrani.
 
Back
Top Bottom