kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Tuwapongeze akina Gwajima, Heche na wengine kwa kuwaruhusu wasemeseme tu vile wanavyovisema na namna wanavyovisema, maana hayo ndiyo matakwa ya demokrasia za Magharibi. Kama hawavunji sheria yoyote kwa mujibu wa katiba waacheni waithibitishie dunia kuwa Tanzania kuna demokrasia pana na na uhuru wa kusema. Tuwaache waendelee kusema mbele ya camera za vyombo vya habari vya Magharibi kama DW, BBC, France 24, nk ili nchi za magharibi watuone tunavyojali uhuru wa watu katika kutoa maoni hata kama hayana tija kwa nchi yetu na Afrika.
Changamoto zipo duniani kote bila kujali taifa, Maana hakuna nchi duniani ambako watu hawauawi kionevu na kwa bahati mbaya. Ukweli lazima kuwepo na watu ambao wanalaani mabaya yanapotokea na kazi ya vyombo vya upelelezi iwe ni kuwabaini wahalifu na kutoa taarifa kwa hatua zilizochukuliwa.
Kazi ya za watu wa dini ni kubadilisha tabia za waumini wao waache uhalifu na wawe na tabia njema zinazompendeza Mungu. Kama ukiwa na tabia inayompendeza mungu bila shaka tabia hiyo itawapendeza binadamu wenzako na watawala.
Waendelee kusema ili kuimarisha demokrasia yetu kimataifa.