Tuwasindikize wanaoenda kuripoti Polisi kwa Video mpya ya Simba

Najua kuna watu mapovu yanawatoka kwa sababu tu ya wivu na kujipoza kwa machungu ya mafanikio ya Mond kwa kujenga beef..,maisha hayako hivyo jitahidi kivyako utoke !! Hivi kwanini hamjiulizi wewe ndio ulianza mziki kitambo enzi zile pale kota za bandari gerezani kariakoo..ukaimbaa...ukaimba...hadi R.kelly akakuona ukaimba nae pia mwisho wa yote ulipoona mziki hauna dili ukatangaza kustaafu kwakua ulikua unafanyia muziki "SIFA na sio HELA"
Chibu ndio mwanamziki wa kwanza wa kitanzania international ambaye ameonyesha music industry ni biashara katoboa tena haswa jina lake ukipita mitaa ya Hollywood california linajulikana julikana .Nakupa mfano kwa wale wanaojua Hip Hop kuna mtu ana rap kwa Nas?tangu enzi hizo...hata mtaani kwake watu wote wanajua kama yeye ni mfalme wa Hip Hop huwambii kitu lakini je mauzo yake yanafanana na Jay Z? vipi pale Drake rhymes zake zinafika hata robo ya Nas?sasa mbona Jay Z,Drake ,...wanauza sana kushinda Nas haujiulizi tu?Music industry ime transform kutoka kuwa mistari migumu ,tata na tenzi za rohoni sana na kuwa SWAGA!!
Hapo ndipo Mond anampiga chini mshikaji wa kariakoo ,hizi ni enzi za Music ya Swag wewe ukijifanya vitenzi sana ,vina sana ,viambishi sana watu wanapiga swaga wanauza hata Neyo analijua hili ndio maana Chris Brown anauza sana kushinda yeye Music ni swaga ,acha maneno na usilinganishe Mond na Mambo yakijinga

Aya press play hapa tuongezee views then ukatangaze zinanunuliwa

 
Kama kuna mtu anataka kubisha bas tuanzie hapa kwenye huu mfano other wise acha maneno angalia mwimbo tuendlee kununua viewers.
 
Ngoja nimwambie mama bhoke aniletee togwa ya baridi huku naendelea kucheki hii video! sijui nitaangalia mara ngapi! sio kwa ubora huu
 
Baada ya Diamond kusaini mkataba na record label ya Universal Music Group (UMG), baadhi ya mambo yameshaanza kubadilika, na baadhi ya mashabiki, hususan wale wa Tanzania hawana furaha.

Of course, kuna mjadala mwingi kuhusiana na ‘kusainishwa kwake’ hasa kwasababu aliwahi kudai kuwa hawezi kuwa chini ya label, labda kama itakuwa ni partnership.

Hata hivyo kwenye mahojiano yake na Clouds FM, Novemba mwaka jana, Diamond alisema Universal Music Group walitoa dola milioni 1 (takriban shilingi bilioni 2.2 za Tanzania) kumsainisha mkataba wa kusambaza nyimbo za wasanii wa label ya Diamond Platnumz, WCB. Naye meneja wake, Sallam aliiambia Bongo5 kuwa mkataba huo ulisainiwa tangu July mwaka jana, lakini tangazo rasmi limetolewa, Alhamis hii, Feb 2.

Kwakuwa sasa UMG imechukua usukani rasmi kwa kusambaza nyimbo za Diamond, mashabiki wake wanapaswa kutambua kuwa, baadhi ya mambo yatabadilika. Kwa sasa nyimbo zake zitakuwa na mlolongo mrefu kutoka na sio kama zamani ‘click link kwenye bio kuona video yangu Youtube.’ Mfano sasa, Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, ilianza kwa kuchezwa Trace TV, ambayo tunajua kuwa inapatikana DSTV pekee, hiyo ina maana kuwa hadi sasa ni Watanzania wachache wamekwishaiona.

Kwasababu lengo la UMG ni kumpeleka Diamond mbali zaidi kimataifa, Marry You unakuwa wimbo wake wa kwanza kuwekwa kwenye platform za kustream muziki kwa kulipia, ambako shabiki wa kawaida wa Masasi au Njombe, nyingi hawajawahi kuzisikia, lakini yule wa Stockholm, Sweden ndio maeneo yao ya kujidai, tayari anaufurahia wimbo huo.

Bila shaka, lengo la UMG sasa ni kumpatia Diamond mashabiki wapya wa kimataifa kumuongezea wigo wa kupata fedha za kigeni na hivyo kukuza mapato yake ambayo yataisaidia pia UMG kurudisha gharama zake za uwekezaji kwa kumsainisha, sababu hii ni biashara, sio charity. Kwa mtazamo huo, kipaumbele cha UMG kwa kazi za Diamond, sasa kitakuwa si Tanzania tu, bali kimataifa zaidi, huo ni ukweli ambao mashabiki wanapaswa kuutambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…