SoC02 Tuwatolee risasi mashujaa

Stories of Change - 2022 Competition

Yazidu Hamza Bitika

New Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
4
Reaction score
1
Habari za wakati huu ewe msomaji wa makala hii, nipende kukushukuru kwanza kwa kutenga muda wako kwaajili ya kutengeneza maarifa mapya kutoka katika ujumbe huu uliojaa madini na ninaamini hutajutia hata sekunde yako moja katika kusoma makala hii.

Jana tarehe 25/07/2022 ilikua ni siku Kubwa sana kwenye taifa letu la Tanzania, na hii ni kutokana na kumbukizi ya wale wote waliopoteza nguvu, jasho na damu kwaajili ya kulipambania taifa hili la Tanzania, labda nianze kwa kuuliza kwa Watanzania na Serikali inayotuongoza Watanzania, " ni ipi maana halisi ya mashujaa?"

Je, ni wale tu waliolala katika mchanga ama vipi? Hapa najaribu kutazama ni namna gani tunakuwa wanafki na tunakosa haya katika nyuso zetu, na kama si hivyo basi hii siku tuibadilishe jina labda tuseme ni siku ya " waliokufa vitani" lakini kama ni mashujaa si hao tu, tunao vikongwe wetu, wengine wanavilema, wengine hawajui asubuhi yao na wengine hawaifahamu jioni yao. Lakini jambo la ajabu na la kusikitisha ni kwamba tunawafumbia macho hawa na kuwakumbuka wale tu waliokufa kwenye vita, kwani Jamani huyu mzee aliyepigana vita ambaye hadi sasa yupo hai na hatumkumbuki hata akifa leo atazikwa kwa mashujaa au makaburi ya wote, kama tunawakumbuka wafu tu, huyu tutamkumbuka lini?

Ama najiuliza tunasherehekea siku ya mashujaa hakuna hata muwakilishi wa wale wapiganaji hata moja aliyeitwa kwenye hizo sherehe hata kusema Neno, inatosha sana kuwafariji kama tunaogopa kuwatengea bajeti zao.

Au labda hawaitwi kwenye haya matukio kwasababu wanakero nyingi mioyoni mwao wataharibu sherehe na kuharibu maslahi ya kisiasa ya watu? Unajua ninapata maswali mengi sana. Alafu sio lazima Serikali itoe fedha labda, hapana, basi uanzishwe hata utaratibu wa kuwatambua hata kwa kila kata, naamini Watanzania wanaupendo na watawakirimu hawa wazee katika haya masiku yenyewe.

Kwa kufanya hivyo tutakua watu Wazuri na wema ila si tu kwa kwenda minalani na kujenga minala ya kisasa halafu wahusika waliopoteza nguvu zao hawana hata unga wa chakula ni otovu wa nidhamu kwa hawa wazee, tuwaheshimishe tuzitoe risasi zilizojaa katika mioyo Yao, hata mbingu zitang'aa juu yetu, kwani hili jambo linamadhara hata ya kuwavunja moyo watu, lakini tukifanya kama mataifa mengine mfano China wanavyowajali mashujaa wao waliohai tunngekua ni watu wenye busara sana.

Uzalendo ni kitu muhimu sana katika maendeleo ya taifa lolote lile duniani, hivyo tujifunze kutoka kwa wazee wetu hawa namna walivyokua wazalendo wa taifa lao, na kwa jinsi walivyolipigania taifa lao kwa jasho na damu. Sisi wote tutakufa lakini Tanzania itabaki, hii ardhi ya Tanzania ipo mpaka Kiama, lakini Mimi na wewe tutaondoka, hivyo hii ardhi ni muhimu sana kuliko wewe, lipende Taifa lako, na wote tukiipenda nchi yetu tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Nakushukuru kwa kusoma makala hii hadi sasa, naamini kuwa wote kwa pamoja, tukiongozwa na viongozi tutalifanyia kazi hili.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Kazi iendelee!!
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…