KOSA WALILOLIFANYA WASUDANI KWA KUSHIKIWA AKILI NA MWANAMKE (MWANAHARAKATI) "ALAA SALAA" NDILO HILO HILO WANALIFANYA WATANZANIA KWA KUSHIKIWA AKILI NA WANAHARAKATI "MANGE KIMAMBI" NA KUNDI LAKE
——————————————————
"Alaa Salaa" Ni bint mwenye umri 22 na mwanafunzi wa chuo kikuu aliyejipamba na sifa ya mpigania haki nchini sudani dhidi ya Utawala wa Omar Al bashir
Wanaume wenye akili timam wakamkabidhi maisha yao na akili zao kwa madai ya kuwapigania haki zao na kuwakomboa dhidi ya waliyemuita ni Dikteta Omar Al bashir.
Media za wa magharibi kama kawaida yao zikampaiza sana bint huyu "Alaaa Salaa" na kumpa sifa ya ushujaa na uzalendo tena na kumuita majina makubwa kwa lugha ya kisudani kama vile:
( THE KANDAKE OF SUDANES REVOLUTION WOMAN)
MWANAMAPINDUZI MWANAMKE WA KISUDANI
Alivishwa "kilemba" cha "ukoka" na mabeberu wa kimagharibi, kwa kuhamasisha kwa namna ya kipekee kila kona ya Sudani.
Na akatambulika kuwa mwanamke "shujaa" asieogopa wanaume wenye silaha za kijeshi waliopitia mafunzo ya kulenga shabaha.
* Kwa masikitiko makubwa lengo la mabeberu kwa kumtumia mwanamke huyu Lengo likatimia.
* Omar al bashir akapinduliwa na jeshi likashika nchi.
* Na Wasudani wakapiga vifijo vya furaha kila kona ya Sudani.
Wakidhani kuwa waliohamasishwa na wanaharakati kwa maneno matamu yenye matumaini ndio sasa yanaenda kutimia kwa kumuondoa madarakani Rais Omar Al bashir.
Kumbe walikuwa wanalambishwa asali yenye sumu.
hakuwafikiria Familia zao zitakuwaje baada ya hapo, wazazi wao wanaowategemea kiuchumi watakuwaje, Mali zao walizozitafuta kwa mda mrefu zitakuwaje....!!!
Kichokuwa mbele yao ni Omar Al bashir anakula mema ya nchi peke yake na familia yake.
Wakaingia barabarani wakaiharibu nchi yao waliijenga wenyewe kwa nguvu na jasho, kwa kupigania bei ya mkate tu kupanda.
Wakamsahau Allah au Mola wao, aliyewaumba na ndio mwenye kutoa riziki wakampa jukumu hilo kiumbe Al bashir.
* Allah akawavisha vazi la njaaa baada ya hapo.
* Walikula majani badala ya ule mkate walioandamana kwa sababu umepanda bei.
Jinamizi la mauwaji likatanda katika ardhi ya sudan, ubakaji ukawa ndio mfumo rasmi katka ardh ya sudani, unyanyasaji ambao haukuwahi kushuhudiwa ndio umekuwa ni kivutio katika ardh ya Sudani.
Leo hii ni Mwaka wa "Saba" Tangu kuanza TAREHE ( 8- 4 - 2019) Tangu mapinduzi ya "Al bashir" mwanamke huyu shujaa Haonekani tena katika media za waliomsifu,
👉 Wale wa Sudani waliokuwa nae bega kwa bega wengi wao wako makaburini.
"Alaaa Salaa" Haonekani tena kwenye majukwaa ya kupigania haki, mpaka leo Sudani umekuwa uwanja wa mapambano na vita vya wenyewe Kwa wenyewe Kwa maana ya ndugu na jamaa, swahiba na rafiki.
Allah awarehemu waliofitinika na fitna za wanaharakati.
——
KOSA KAMA LA WASUDANI WANALIRUDIA WATANZANIA
Watanzania wenye kusifika kwa amani na utulivu busara na uvumilivu wameingia katika mfumo uliowaangamiza Wasudani.
Watanzania wenye akili timamu wanaziweka rehani akili zao, utu wao, busara zao, heshima zao, wanamkabidhi mwanaharakati MANGE KIMAMBI """* Na kundi lake bila kujali mazuri yaliyotuzunguka bali tunatamani ziyada ya haya tuliokuwa nayo kwa kuangamiza juhudi zetu wenyewe kwa kushawishika na wanaharakati tuliwapa jina la "wapigania haki."
Bali kwa mapenzi yake mungu akatupa mazingatio machache kwa kilichotokea "Octoba 29" bila kuhadithiwa tukaonjeshwa tone la shubiri lililochukuwa siku zisizozid 10, bali mpaka leo athari zake zinalitafuna taifa letu.
Watanzania walewale wanarudia tena kuwapa akili zao na maisha yao wakina "mange kimambi" na kundi lake kuwa lile tone la shubiri halijakata kiu sasa wanataka "jagi kamili December9."
* Wanataka wagongwe na nyoka mara mbili.
* Wamejisahaulisha kuwa :
Baadhi ya majeruhi vidonda vyao havijapona.
* Baadhi ya wajane eda zao hazijaisha....!!!
* Baadhi ya waliozikwa miili yao bado hata baadhi ya nyama zao hazijamalizwa na mchanga,
👉 Bali miundo mbinu na huduma za kijamii mpaka leo baadhi hazijatengemaa.
NDIO MANA QURAN MARA NYINGI IMEWAZINDUA WANADAMU KWA KUWAAMBIA:-
* HIVI NYIE HAMNA AKILI???
* JE HAMZINGATIII??
* JE HAMTAFAKARI???
—————-
✍️mzalendo number moja
Tanzania 🇹🇿kwanza mambo mengine badaye🚶♂️