Tuwe makini jamani

Tuwe makini jamani

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,666
Reaction score
12,178
Jamani tuwe makini na vyakula vya njiani
kuna jirani yangu hapa yamemkuta. Katoka kazini kafika stend akakuta pweza, basi akala pweza wa buku jero.

Akaomba na supu ya pweza ya mia tano akashushia. Baadae akaelekea nyumbani kwake akamkuta mkewe akamuomba maji ya kunywa, alipopewa akayanywa kisha mke wake akamtengea maji ya kuoga.

Baada ya kuoga akajumuika na familia kula chakula cha usiku wakalala. Baada ya hapo sasa, asubuhi kaamka kaoga kavaa vizuri kaenda kazini.

Kwa ujumla yuko vizuri kiafya.
 
Kwa hivyo kama asingelikula pweza na kuinywa supu ya pweza asingelitengewa maji ya kuoga baada ya kunywa maji na pia asingelioga asubuhi aende kazini?

Maswali ni mengi ila majibu kumkichwa. Asante kwa fumbo lako.
 
Hiki ulichoandika huko kwetu kanda ya ziwa tunaita UDUVI.
 
😂😂😂
Sijajua kama na wewe upo makini aise?
 
Duuuuuhhhhh,wanaume wa Dsm mnakula pweza ndyo mnaenda kupandana na wake zenu!!!!
 
Back
Top Bottom