Lumbi9
JF-Expert Member
- Oct 12, 2014
- 8,666
- 12,178
Jamani tuwe makini na vyakula vya njiani
kuna jirani yangu hapa yamemkuta. Katoka kazini kafika stend akakuta pweza, basi akala pweza wa buku jero.
Akaomba na supu ya pweza ya mia tano akashushia. Baadae akaelekea nyumbani kwake akamkuta mkewe akamuomba maji ya kunywa, alipopewa akayanywa kisha mke wake akamtengea maji ya kuoga.
Baada ya kuoga akajumuika na familia kula chakula cha usiku wakalala. Baada ya hapo sasa, asubuhi kaamka kaoga kavaa vizuri kaenda kazini.
Kwa ujumla yuko vizuri kiafya.