Tuwe makini na minada ya nguo nyakati za Usiku

King Sae

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2018
Posts
3,282
Reaction score
6,471
...amani iwe kwetu sote.

Leo nimetoka zangu mihangaikoni naludi geto mida ya usiku tatu kasoro ,ile nashuka tu stand...hatua chache mbele nikakutana na mnada wa nguo afu Bei chee,nikasema ngoja nisogee nikaangalie ikiwezekana ninunue ata fulani mbili za kushindia.

Nikastuka mbna nguo nzuri hv afu wanauza Bei rahisi na zawadi juu na kwanini wauze usiku, hisia zikaniambia fanya kilichokuleta...nikachomoa mwekundu uku nikisikilizia jirani yngu anunue ili niangalie vzur...mara nkaona nguo nzur nyeupe,fasta nikanyosha mkono then nkarushiwa,sjaingalia vzur jamaa anadai pesa nikampa...kwa kifupi nilinunua nguo tatu kwa elfu tatu jumla elf 9.

Nkataka nichomoe mwekundu mwengine ninunue majinsi...baada ya kuona watu wanayachangamkia,loooh akili akaniambia nenda nyumbani ukaoge then urudi Kwenye mnada.

Kufika geto,harakaharaka nikataka nizijarbu zle nguo...nilivyozigeuza nje ndani ndani nje, ahahaa nilichoka...kumbe yale malonyalonya form six sijui grade F wameyapunguza na kuyafua kisha kuyapiga pasi fresh...

Ilinibidi niludi tena kuwaangalia wajinga wanavyopigwa...nikagundua kuna watu wananunua Ili tu kushawishi wajinga wanunue...kumbe wao sio ata wateja.

Daah....nililudi geto kwa unyonge Sana uku nikiwaza ile elf 9 yngu..bora ningenywea supu asubuhi.

TUWENI MAKINI NA MINADA YA NGUO NYAKATI ZA USIKU.
 
MKUU PALE UNAWEZA UZIWA JINZI IMEKOLEA RANGI ILA UKIENDA KUFUA UNAKUTA RANGI YOTE INATOKA ,HUWA WANAWEKA RANGI ZA MKEKA AU BATIKI
 
Daah pole Sana Aisee ,
Kuna siku mm nilipigwa pale karume karibia na geti LA kiwanda cha bia aisee ilikua mwaka 2011 nilikuta jamaa kamwaga suluali za vitambaa chini anauza buku tatu tatu nikanunua mbili, kimuonekanao zilikua poa Sana , na watu walikua wanazichangamkia ,
Sasa bana zile nguo zilikua zimebandikwa lebo Fulani hivi Kama kuonyesha ni Mpya aisee,
Nimefika zangu home nikasema ngoja nijipime hizi Nguo , zikanitosha fresh kabisa .
Sasa bana nikasema hebu ngoja nitoe haya malebo , kutoa tuu lahaula , nikatana na tundu linaniangalia , kumbe wamebandika lebo kuficha matundu aisee niliboreka ,mbaya zaidi matundu yenyewe yalikua kwenye makalio
Ikabaidi tu ziwe matambara ya deki , kwel mjini shule
 
MKUU PALE UNAWEZA UZIWA JINZI IMEKOLEA RANGI ILA UKIENDA KUFUA UNAKUTA RANGI YOTE INATOKA ,HUWA WANAWEKA RANGI ZA MKEKA AU BATIKI
Na kweli mkuu Mana kulikuwa na jinsi kali zinauzwa elfu 5 adi 4
 
Mkuu wale wanaochangamkia usikute ni wapambe tuu Ili kuvuta wengine....

Polee sanaa mkuu
 
🤣🤣🤣🤣🤣pole
 
Mkuu na wewe uliligwa kiboya malebo matakonii tena
 

Hahahhahah
 
Wale jamaa hufanya mambo kama CCM wanavyofanya mikutano yao ya kampeni kwa kuswaga watu kutoka, hao jamaa nao hujaza wapambe kibao ili udhanie nao ni wateja ili uvutiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…