Tuwe makini na wachungaji wanaotoa shuhuda za waumini

Tuwe makini na wachungaji wanaotoa shuhuda za waumini

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Habari za humu wanajamii,

Ni kwa muda sasa huwa ninamfuatilia huyu mchungaji wa KKKT ushirika wa Kijitonyama Mchungaji Kimaro,hadi kuna muda niliwahi kushawishika kwenda kanisani kwake.

Sasa katika kufatilia hayo mahubiri yake sasa sijui ni shetan au ni kawaida, ninaanza kuona kama tunapigwa hivi na hii ni kutokana na visa vyake anavyokuwa anasimulia, kuna kisa kimoja nilisikiliza jana usiku, eti kuna mfanyabiashara mmoja hapo Kariakoo miaka ya 2012-2015 aliahidi kutoa sadaka ya asilimia 10 baada ya kununua gari yake v8 ya thamani ya milioni 150. Sasa baada ya kununua hiyo gari alienda hadi kwa mchungaji Kimaro na kuomba aiweke wakfu yaani aibariki hiyi gari ya milllion 150, na baaada ya kubarikiwa alitoa laki mbili kama sadaka.

Baada ya kuondoka pale kwa mchungaji dakika kama 30 hivi alivamiwa na majambazi akapigwa risasai saba katika eneo la tumbo na mbavu, baada ya kutokea hilo tukio alipelekwa MOI hatimaye India kwa matibabu amabapo alitumia milioni 300 kwa matibabu tu.

Baada ya miezi saba ya kupona ikabidi aende kwa mchungaji Kimaro kutubu na kutoa zile milion 15 alizotia nadhiri.

Kisa kinaendelea kwa Mchungaju kusema kwamba kuna siku kulikuwa na ibada ya shukurani huko Kilimanjaro ambapoa mchungaji Kimaro alisimamisha wa kwa ajili ya kutoa sadaka na alisema watu kuanzia milioni moja kwenda juu tu ndio walete hizo sadaka na yule mfanyabiashara alitoa milion 30 kuhofia kwamba asipotoa atapa majanga tena

Baada ya hapo akaanza kusema oh hayupo hapo kwa ajili ya kuwalaghai watu ili kupata pesa kama pesa yeye pia anaweza na kujua kuzitafuta kabla hata ya hapo alikuwa anabiashara zake na pesa alikuwa anapata.

Ninyi mnaosali huko tuelezeni huyu Mchungaji au mimi tu ndio nimeanza kutomwelewa?
 
Kuna kitu kinaitwa NADHIRI maana yake ni kuweka agano na MUNGU au Shetani pale unaposhindwa kulitimiza adhabu yake ni Kali sana ,Kuna mtu mmoja aliweka agano la kuwa Padre baadae akaacha jamaa hayupo sawa ni kama mwehu,pia wapo walioweka maagano na waganga na wakashindwa kutimiza wakapata majanga makubwa ,so ishu hapo sio Hela ishu ni agano alilofunga na Mungu
 
Yer 17:5 SUV

Bwana asema hivi,

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,
amfanyaye mwanadamu kua kinga yake,
na moyoni mwake amemwacha Bwana.
 
Fungu la kumi lilikuwa kwa ajili ya walawi agano la kale

Hao wachungaji Nguruwe wanakula ukiwaambia biblia imekataza wanakwambia hilo ni agano la kale .

agano la kale limekataza hadi wanawake kutoboa masikio. Na kuweka hizo hereni.. agano la kale Limekataza hadi kukopesha kwa riba. Hayo wachungaji hawayafati hayo makatazo wanasema ni agano la kale.

Cha kushangaza kwenye zaka na sadaka(PESA) wanalitumia hilo hilo agano la kale kudai fungu la kumi kwamba ni sheria ya Mungu ila maagizo mengine ya agano la kale wanayakataa kwamba hizi ni zama la agano jipya.
 
We nenda kanisani sali kwa Mungu unaemuamini, hayo mengine ukiona ni magumu kwako achana nayo
 
Ujanja ujanja

Inaaminika kuwa Mungu ndio mtoaji, sasa iweje tena atake fungu la kumi? Kwa nini asilikate juu kwa juu kabla ya mtu kupatiwa?
 
KKKT imekuwa kama makanisa ya manabii. Ujinga ujinga tu stori za uongo kutafuta pesa kinguvu.
 
Ni Wachagga hao mtapigwa sana mtuulize sisi ambao tuliowahi kuishi mikoa hiyo.hao kwao pesa ndo kila kitu na hawana urafiki na maskini.
 
Ni Wachagga hao mtapigwa sana mtuulize sisi ambao tuliowahi kuishi mikoa hiyo.hao kwao pesa ndo kila kitu na hawana urafiki na maskini.

Mmmh
 
Fungu la kumi lilikuwa kwa ajili ya walawi agano la kale

Hao wachungaji Nguruwe wanakula ukiwaambia biblia imekataza wanakwambia hilo ni agano la kale .

agano la kale limekataza hadi wanawake kutoboa masikio. Na kuweka hizo hereni.. agano la kale Limekataza hadi kukopesha kwa riba. Hayo wachungaji hawayafati hayo makatazo wanasema ni agano la kale.

Cha kushangaza kwenye zaka na sadaka(PESA) wanalitumia hilo hilo agano la kale kudai fungu la kumi kwamba ni sheria ya Mungu ila maagizo mengine ya agano la kale wanayakataa kwamba hizi ni zama la agano jipya.
Uko sahihi agano jipya tunatoa kwa moyo wa kupenda, ila kinachoonekana hapo huyo jamaa aliweka nadhiri (ahadi yako kwa Mungu) na uongo ni dhambi. Ni muhimu kutimiza nadhiri au kufanya toba ukishindwa.
 
Back
Top Bottom