mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Ukiijua kweli itakuweka huru. Nduguzangu hii ni ngumu kumeza ila ipo katika politiko sayansi nimeona si vyema kuficha ngoja tuelimishane japo kidogo. Nikisema sayansi ninamaana ni uchunguzi wa kimaabara kupata ukweli, iko hivi Mbowe alijenga nguvu ya umma bila huo umma kuupa hiyo nguvu. Nini maana yake. Katika uongozi wa nguvu ya umma uwa maamuzi, mamlaka na haki zinasikilizwa kutoka chini kwenda juu.
Tofauti kabisa na Mbowe ambapo mdomoni alikuwa anauburi nguvu ya umma wakati maamuzi yote yalitoka juu kwa mtu mmoja au watu wachache kuwafikia wengi ndiyo maana leo yupo Segerea wafuasi wake wanapanga foleni kwenda kumsalimia wakati kama ingekuwa kweli ni nguvu ya umma wasinge sogea hata mmoja pale gerezani ila wote wangekuwa barabarani.
Ndiyo maana kisayansi utaona Nelson Mandela alipofungwa gerezani ni mkewe, watoto wake na baadhi tu ya viongozi wachache ndiyo walikuwa wanakwenda kumtembelea na si umati wote ulikusanyika gerezani. Ila habari ilikuwa kule Natali, Soweto, Zululandi na mitaani Kaburu Bota alikuwa anausikia mziki mkubwa. Lakini leo tumeshuhudia watu wakikodi magari kutoka mikoani kwenda gerezani na mahakamani kumwona kiongozi wao.
Angalia Jakobu Zuma alipohukumiwa kufungwa kwa uonevu hakuna mtu alieenda gerezani hata kumsalimia au kutia fujo, mziki waliufungulia kama nguvu ya umma mtaani. Hii ndiyo maana ya nguvu ya umma, sasa ukiona wafuasi wanaomba kibali kwa bwana jela kumwona mtuumiwa au mfungwa ujue biashara imeisha kwani wamekubali yote.
Jamani huu ni ukweli ila si mtam hivyo kama wewe mfuasi unaenda Segerea wewe ni mtu mstaarabu sana tena kuzidi wale wa Lumumba unafuata sharia za nchi na unaenda pale kiungwana kumsalimia mtuhumiwa kama tunavyokwenda kuwaona wagonjwa hosipitali na hiyo si nguvu ya umma hata mkiwa milioni bado uwezi kuita nguvu ya umma.
Hivyo Mbowe yeye mwenyewe kwa mikono yake alifeki nguvu ya umma na kujenga nguvu ya waungwana ndiyo maana leo waungwana wote wanajipanga jinsi na namna ya kwenda Segerea kumsalimia kiongozi wao na hii inamaana kuwa hata atakapo hukumiwa (kama) ndiyo wataenda kwa wingi sana kumwona Mbowe gerezani. Eleweni nguvu ya umma si kufuata katiba, nguvu ya umma yenyewe ni katiba tosha sasa ukiona nguvu ya uma inafuata katiba ujue hapo ni matango poli.
Hivyo kwa vijana wa Ufipa mliobahatika kwenda shule na mnapenda nguvu ya umma anzeni kushauri na kujenga nguvu ya umma kwani inawezekana na humu waacheni vilaza waendelee kutukana mitusi kwani hawana elimu ninyi jengeni taasisi hiyo iposiku Mungu mkubwa.
Mi nalishauri jeshi la magereza kuweka utaratibu mzuri wa hawa waungwana kuweza kumsalimia kiongozi wao kwani hilo si kosa hata kidogo bali wanafuata sharia na wanaimani na kiongozi wao na wanampenda na ni watiifu kwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.