Tuwe wakweli kocha Nabi hana mbinu za mechi za kimataifa. Rekodi zinaongea.

Hata mechi za ndani anashinda Kwa sababu mechi nyingi zinachezwa nje ya uwanja , Yani Hz mechi za ndani hata kichaa ukimpa timu anashinda cha msingi tu kamati ya nje ya uwanja iwe vzur
 
Uwe unaelewa nimesema wakina Kisinda ina maana ana wenzake. Kuna wachezaji kwenye timu, inafika wakati hawana msaada na timu. Mfano nimetoa huyo Kisinda...
Kushinda na kutoshinda yote ni matokeo ya mpira, na tumeyapokea.
Kuijumla wachezaji karibu wote hawakuwa mchezoni hasa kwanzia kati
 
Sawa mkuuu ndo maana ya jukwaa nikikosea unanirekebisha. [emoji122][emoji122]
 
Acha chuki kwa Prof wewe, zalan kala 9 mbona husemi
 
Kuijumla wachezaji karibu wote hawakuwa mchezoni hasa kwanzia kati
Kuna shida mahala fulani, ndiyo maana nasema tusimtupie lawama zote Nabi, ana za kwake ila si zote. Kwa wachezaji zinawaangukia asilimia kubwa kuna kitu hakipo sawa, ile morali wanayokuwa nayo uwanjani, imepotea. Tungeanzia hapo but wapenda mpira lawama ni kocha tu...
 
Umesema vyema.
Japo kiuhalisia uchezaji wa Yanga msimu huu, pamoja na kwamba unafanana na msimu uliopita, intensity ni ya kiwango cha chini mno. Wachezaji hawafiki kwenye maeneo kwa wakati.
Ukitafuta mchezaji ambaye hajashuka utendaji kazi uwanjani kulinganisha na msimu uliopita, kwa sasa ni wa kutafuta. Labda Job, labda Kibwana, labda Moloko.

Uchezaji wa Yanga au tuseme mbinu za Nabi ni wa kutabirika sana. Wanashambulia polepole sana hivyo wanawapa timu pinzani muda wa kutosha kujipanga vizuri na kurekebisha makosa yao kama yalikuwepo. Kwenye mpira wa miguu unatumia makosa ya mpinzani au kumlazimisha kufanya makosa ili umfunge. Sasa kama unampa nafasi ya kujipanga utamfunga kwa urahisi?

Goal threat kwa yanga ni kwa nani? na hasa viwango vya wachezaji wa timu pinzani vikiwa sawa au juu ya Yanga. Labda Mayele. Labda Feisal. Mwingine nani? Usiseme Aziz Ki. Kwenye open play shooting accuracy yake ni mbovu sana tegemea off target kuliko on target.
Utaanza kujiuliza mbona NBC Premier League Yanga ina unbeaten? Team nyingi za ndani zina wachezaji wenye unora wa chini kuliko wachezaji wa Yanga. Kwa sababu ya tofauti ya ubora, timu wachezaji wa timu pinzani hupoteza concetration ndio maana Yanga mara nyingi inapata matokeo kipindi cha pili. Lakini inapata shida kwa timu zinazocheza kwa intensity kubwa (eg. mexhi dhidi ya KMC, Geita ) au zenye wachezaji wa ubora unaoelekeana (eg. mechi dhidi ya Simba, Azam)
 
Nakubaliana na wewe
 
Aisee umetisha sana mkuu. Kwanini usiombe kazi EFM kuwaondoa wale wachambuzi wa mchongo kina Jemedari? [emoji1][emoji1][emoji1][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Upo sahihi kabisa
Nabi mbinu za kimataifa Hana
Ila mkuu hujaweka mechi ya zalani .
Kwa nn Nabi anapenda kumuanzisha kisinda ,
Kisinda kaisha anatakiwa asugue banchi tuu
Huyo Nabi mnayesema hana mbinu za kimataifa ana medali ya dhahabu kwenye mkoba wake baada ya kutwaa ubingwa wa shirikisho Afrika akiwa na As Leopard, timu ambayo haikuwa imechukua ubingwa wowote wa Afrika tangu kuundwa kwake.
Nabi ameshaingia fainali na kupoteza katika haya haya mashindano ya kimataifa mnayosema hana mbinu nayo.
Aliwahi pia kufika nusu fainali. Hapo uhalali wa kusema hana mbinu za kimataifa tunatoa wapi? Je tatizo ni Nabi au Yanga yenyewe?
Yanga imeingia makundi Afrika mara tatu na haikufanya vizuri kwenye makundi ukilinganisha na Simba ambayo imeingia makundi mara nne na kati ya hizo 3 imefanya vizuri, tunasubiri tuone hii ya nne watafanya nini
 
Simba keshachezea khamsa khamsa za kutosha mpaka leo hii unaona Simba kuingia makundi sio ajabu tena.

Yanga lazima wakubali kwanza kupitia magumu.
 
Hawa utopolo ovyo kabisa, sasa tutaanza kuamini huku kwenye NBC league wanashinda kwa ujanja ujanja wa kuhonga marefa na wachezaji wa timu pinzani
Kama kuwafunga ni rahisi wafungeni nyie basi uko kwenye nbc league. Kwani lazima wafungwe na timu zingine
 
Simba keshachezea khamsa khamsa za kutosha mpaka leo hii unaona Simba kuingia makundi sio ajabu tena.

Yanga lazima wakubali kwanza kupitia magumu.
Umeongea ukweli ndugu, bado kuna technical know-how za michuano ya kimataifa yanga hana lakini sio kwamba timu mbovu al hilal alipaki basi game zote mbili jana waarabu walipaki basi na kujiangusha tu kupoteza muda shida inakuja kwa yanga anaposes mpira ila kupenya ngome ya adui ndo shida inapoanzia
 
Hizo ni hasira tu na zote mnamuangushia Nabi... Bado ana nafasi ya kuunda kikosi next time kwa mechi za kimataifa. Kosa lake ni kuwaanzisha kina Kisinda... akiambiwa atajirekebisha.
Kisinda anatakiwa kusugua benchi.
Morison asianze aingie kama sub maana huwa hakabi pia huwa na impact akiingia kama sub.
Fei acheze namba kumi na siyo Ki Aziz.
Babu kaju aanze badala ya Aucho.
Makambo asugue benchi na baadae atafute timu pamoja na mwanariadha Kisinda.
Moloko aanze kila mechi kama hana changamoto yoyote.
 
Caf kule ukienda na maneno ya un beaten,mara sijui mabingwa wa kihistoria kule utachemsha.kule panataka watu wafanye kazi kila point inayohusu timu kupata ushindi kuanzia saikorojia ya wachezaji,timu,kocha,viongozi,mashabiki n,k
 
Watu mkishiba makande mnajiona wachambuzi
 
kwanini usiajiriwe wewe mwenye mbinu uwe kocha wetu?
 
Nyoooo, umeumbuka chaku bimbi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…