Tuwe wakweli, Rais Samia ameleta matumaini. Aliyepita aliwachukia wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi na wakulima

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Mpk sasa naweza kusema kuwa Rais Samia ana roho nzuri na ana nia njema na taifa hili.

Mtangulizi wake alikuwa na mwelekeo wa kuwadidimiza (kuwafukarisha) wafanyabiashara. Alitamka hadharani kuwa matajiri wataishi kama mashetani. Ndipo akaanza kiwazushia tuhuma mbalimbali na kuanza kufunga akaunti zao za benki. Mama ameufutilia mbali upuuzi huu.

Mtangulizi wa Rais Samia aliwachukia wafanyakazi. Ktk kipindi chake hakuwahi kuongeza mishahara ya watumishi wa umma. Pia aliwapunguzia mishahara maCEO mbalimbali wa mashirika ya umma kwa kisingizio kisicho na mashiko. Mama amutupilia mbali upuuzi huu.

Wanasiasa walipewa vikwazo na vitisho vya kila aina. Waulize Kinana, Membe, Lowasa, Sumaye, Msambatavangu, Sofia Simba na wanasiasa wote wa upinzani watakupa full story ya mbabe huyu. Mama ameufutilia mbali upuuzi huu. Bado tatizo moja tu kwenye siasa akilitatua mama atakuwa kaupiga mwingi KATIBA MPYA.

Wakulima hawakuruhusiwa kuuza mazao yao mahala watakapo
. Yaani mkulima anahangaika kulima mwenyewe, kununua pembejeo mwenyewe na avune mwenyewe halafu serikali impangie wapi pa kuuza mazao yake. Huyu jamaa alikuwa hajui maana ya kilimo biashara. Mama ameutupilia mbali upuuzi huu.
 
Angalizo tuu kwa mleta mada!!

Hii furaha uliyonayo isije kupelekea ukichaa na hata kufa ghafla kwa sababu ya sherehe ya nyongeza ya mshahara

Nawaheshimu wasiotegemea boss atapike ndo wapate mlo

Mara nyingi wenye kutegemea boss atapike ndio wale, boss akikasirika, kwa mtindo huu wa maisha na chukula tunachokula, wengi wamekuwa wakifa kwa presha!
 
Tumpe muda mkuu. Huyu mama ana roho na moyo safi

Huko kwingine ana afadhali, lakini kwenye eneo hili naona ana uccm mwingi, na wanaccm wenzake hawakubali maana wanajua ndio mwisho wa chama chao. Simply sioni kama ana jipya upande huu.
 

Irrelevant.
 
Sasa Hivi Kila Mtu Anafanya Atajavyo
Yaani Daladala Kutoka Kingolwira ~Mjini Morogoro Tshs 800/= Wanatoza Zaidi
Wakati Hata Kilometres 10 Hazifiki
Ukienda Na Kurudi 1600/=
 
I once told a friend of mine that, in Tanzania, with regards to leadership standards and accountability, the bar is too low.

He replied sarcastically with a rhetorical question.

What bar?

There is no bar. There was a chalked line which was long ago washed away by rain.

So yeah, it is hard to go lower than that.
 
Yule alikuwa na mapepo. Alimfokea jaji mihayo wa watu eti kwanini umevaa barakoa, tena kanisani!!!

Yule alikuwa ni special case ya mirembe kama alivyosema anthony dialo kipindi kile.
 
Huko kwingine ana afadhali, lakini kwenye eneo hili naona ana uccm mwingi, na wanaccm wenzake hawakubali maana wanajua ndio mwisho wa chama chao. Simply sioni kama ana jipya upande huu.
Hapa ndiyo mtego wake mkubwa. Ngoja tuone atautegua vipi
 
Sasa Hivi Kila Mtu Anafanya Atajavyo
Yaani Daladala Kutoka Kingolwira ~Mjini Morogoro Tshs 800/= Wanatoza Zaidi
Wakati Hata Kilometres 10 Hazifiki
Ukienda Na Kurudi 1600/=
Huu sasa ni uholela ambao unaweza kidhibitiwa na kutii sheria bila shuruti ama kwa shuruti
 
YULE ALIKUWA NA MAPEPO. ALIMFOKEA JAJI MIHAYO WA WATU ETI KWANINI UMEVAA BARAKOA, TENA KANISANI!!!

YULE ALIKUWA NI SPECIAL CASE YA MIREMBE KAMA ALIVYOSEMA ANTHONY DIALO KIPINDI KILE.
Yes. Mzee Diallo alisema tulichagua mtu aliyekuwa na faili Milembe
 
Sasa Hivi Kila Mtu Anafanya Atajavyo
Yaani Daladala Kutoka Kingolwira ~Mjini Morogoro Tshs 800/= Wanatoza Zaidi
Wakati Hata Kilometres 10 Hazifiki
Ukienda Na Kurudi 1600/=
Jiuwe basi ukaishi na yule mwehu mbinguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…