Tuweke Akiba Ya Maneno

Tuweke Akiba Ya Maneno

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Wakati barabara ya Shekilango inajengwa mimi ni mmoja wa watu walioponda wajenzi kwa jinsi walivyokuwa wanajenga.

Yaani ilikuwa vurugu mechi, mara wamechimba hapa wameacha, wamejenga hapa wameacha, wametindua huku wameacha. Nikajisemea sijawahi kuona wajenzi wabovu kama hawa na hii njia itakuwa kituko.

Baada ya barabara ile kuisha nilistaajabu jinsi ilivyo nzuri na kiwango cha kuridhisha kabisa! Sasa hivi kuna ujenzi unaendelea wa barabara ya KIlwa na Kawawa ukijumuisha barabara za mwendoksai.

Watu wengi wanaponda ujenzi ule na mkandarasi wake. Nawaambia tu tuweke akiba ya maneno. Sidhani kama wajenzi wale wanajenga nje ya ramani na michoro ya barabara ile. Lazima kuna watu wanaangalia vitu hivi vinazingatiwa.

Namna yao ya ujenzi ni kama ile ya Shekilango yaani vurugu mechi mwanzo mwisho ila kwa ninavyoona sehemu chache 'zilizokamilika' hii itakuwa barabara bora kuliko hata ile ya Kimara-Kivukoni.

Najua wengi watapinga hasa ambao hata huwa hawatumii hizo barabara wanafuata mkumbo tu na mawazo hasi ila narudia tena tuweka akiba ya maneno.
 
Ya usitukane mamba kabla ya kuvuka mto.
Ngojeni barabara iishe afu ndo mje mtoe kasoro.
 
Back
Top Bottom