Tuwekee hapa majina ya miti inayofaa kuoteshwa mazingira ya nyumbani

Tuwekee hapa majina ya miti inayofaa kuoteshwa mazingira ya nyumbani

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Wakuu sio kila mti unafaa kuoteshwa mazingira ya nyumbani maana kuna inayokuwa mikubwa kiasi cha kupasua hata kuta za nyumba kuna ya kutoa majani mengi kiasi cha kuchafua uwanja n.k

Wajuzi tuwekeeni hapa majina ya miti mbalimbali inayofaa kuoteshwa ktk mazingira ya nyumbani
 
Pia unaweza kuweka majina ya miti isiyofaa mazingira ya home na sababu kwanini unaona haifai
 
Wakuu sio kila mti unafaa kuoteshwa mazingira ya nyumbani maana kuna inayokuwa mikubwa kiasi cha kupasua hata kuta za nyumba kuna ya kutoa majani mengi kiasi cha kuchafua uwanja n.k

Wajuzi tuwekeeni hapa majina ya miti mbalimbali inayofaa kuoteshwa ktk mazingira ya nyumbani
Hapo ilifaa kichwa kisomeke Hasara ya Kupanda miti Majumbani bila Kuzingatia Ukubwa wa Kiwanja na ushauri.
Hasara hizo ni.
  1. Kuzuia mwanga
  2. Nyufa kwenye kuta
  3. Kuchafua uwanja kwa majani
  4. Kuzuia upepo
  5. Mazalio ya wadudu na ndege
 
Unapotaka kupanda miti lazima uzingatie...

1.Ukubwa wa eneo lako;Kuna miti inahitaji eneo kubwa ili iweze kutandaza mizizi yake vizuri.
  • Sasa siyo na kieneo chako cha mita 18 kwa 18,unataka upande miembe
  • Kuna miti inapendeza kuwa mbali na nyumba ili kuweza kuruhusu mwanga ndani ya jengo.
  • Siyo unapanda miashoki karibu na nyumba
2.Kuna miti inahitaji ardhi yenye maji ya Kutosha
  • Siyo unataka mkaratusi kwenye ardhi kame
  • Kuna miti inahitaji uwe na Ukwasi wa kugharamia kutoa majani kila siku

3.Kuna miti inatakiwa ipandwe kwa kuangalia uelekeo wa upepo ukoje..
  • Unaweza jikuta unazuia upepo ndani ya jengo.
4.Kazi ya miti...
  • Kuna miti inatoa maua ya Kuvutia.
  • Kuna miti ni mizuri kwa kivuli
  • Kuna miti inatoa harufu nzuri hasa nyakati za usiku
  • Kuna miti ni miti shamba
  • Kuna miti watoto huweza kupanda na kucheza
Hizo ni mojawapo ya kuchagua aina ya miti utakayopanda ndani ya eneo lako....
 
Hapo ilifaa kichwa kisomeke Hasara ya Kupanda miti Majumbani bila Kuzingatia Ukubwa wa Kiwanja na ushauri.
Hasara hizo ni.
  1. Kuzuia mwanga
  2. Nyufa kwenye kuta
  3. Kuchafua uwanja kwa majani
  4. Kuzuia upepo
  5. Mazalio ya wadudu na ndege
nimekupata mkuu ILA sikumaanisha ivo

NATAKA kujua aina ya miti RAFIKI ya kupanda hom uwanjani bila kuleta uharibifu wa aina yoyote
 
1. Mkunazi.
2. Muarubaini. 3. Mvumbasi=Holly Basil/Kashwagara/Kiitamarogo
4. Mfunguo/Mwetango
5. Msharifu/Wonder Leaves
6. Lemon Grass/Mchaichai
7. Mstafeli/Soarsoup
8. Mkomamanga
9. Mmbilimbi.
10. Mdimu/Mlimao
11. Mzaituni
12 Kadhalika
Mkuu wenzako tutataja nini sasa 😂😂😂😂🙏🙏🙏
 
1. Mkunazi.
2. Muarubaini. 3. Mvumbasi=Holly Basil/Kashwagara/Kiitamarogo
4. Mfunguo/Mwetango
5. Msharifu/Wonder Leaves
6. Lemon Grass/Mchaichai
7. Mstafeli/Soarsoup
8. Mkomamanga
9. Mmbilimbi.
10. Mdimu/Mlimao
11. Mzaituni
12 Kadhalika
tawire kiongozi
[emoji1666][emoji1666]
 
nimekupata mkuu ILA sikumaanisha ivo

NATAKA kujua aina ya miti RAFIKI ya kupanda hom uwanjani bila kuleta uharibifu wa aina yoyote
Kila mti uharibifu wa aina moja ama nyingine.
Uharibifu hutokana na
ukubwa wa eneo lako ....
Umbali kutoka ukuta
Huduma kwa miti husika....
 
Wakuu sio kila mti unafaa kuoteshwa mazingira ya nyumbani maana kuna inayokuwa mikubwa kiasi cha kupasua hata kuta za nyumba kuna ya kutoa majani mengi kiasi cha kuchafua uwanja n.k

Wajuzi tuwekeeni hapa majina ya miti mbalimbali inayofaa kuoteshwa ktk mazingira ya nyumbani
Miti yote panda isipokuwa mpapai.Umeniudhi sana.
 
nimekupata mkuu ILA sikumaanisha ivo

NATAKA kujua aina ya miti RAFIKI ya kupanda hom uwanjani bila kuleta uharibifu wa aina yoyote
Mkuu,
Hapo wengi watajikita kutaja ambayo ikiwa karibu na nyumba inaleta nyufa...lakini watasahau uharibifu wa
  • Mazalia ya wadudu/ Mbu/Nyuki.
  • Chanzo cha miizio/ allergic reaction.
  • Husababisha ukungu kwenye ukuta.
  • n.k
Ndiyo mana nkasema lazima uwe na key points takribani unazozilenga....
Ila ukisema hakuna madhara kabisa, itakuwa ni uongo.
 
mpapai una shida gani mkuu
Mpapai panda shambani kwako porini sio nyumbani.Mizizi yake inanawizi kuliko kigogo chake.Kigogo ni kimoja lakini mizizi ni mingi sana na inatambaa kwenda mbali chini ya nyumba.Mizizi ina nguvu ya kutambaa na kusukuma mpaka mawe makubwa ya makaro.
Siku ukiukata ndio balaa zaidi.Kama hukuung'oa haraka na ukawacha uoze basi maji maji yake ni kama acid yanachimba shimo ambalo wewe mwenyewe ukitumbukia unazama wote.
Achana na mpapai kama mti wa bustani,Ufanye ni mti wa matunda ya kibiashara upande porini tu.
 
Back
Top Bottom