Tuwekeze kwa wajasiriamali wadogo wanaojituma

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Habari wakuu,

Nina wazo la 'win/win situation' inawezekana wewe ni mjasiriamali uko kwenye kundi hili:-​
  • Muuza genge​
  • Muuza mishikaki/ nyama mapande​
  • Muuza matunda​
  • Mama ntilie​
  • Mtembeza karanga, soda, biskuti n.k​
  • Chinga wa nguo​
  • Muuza nyanya, vitunguu n.k sokoni​
  • Muuza vyombo kwa kutembeza​
  • Unachoma mahindi​
  • Unauza mihogo​
  • Unauza samaki walio kaangwa​
  • Muuza barafu kwa kutembeza n.k​
Soko la uhakika unalo, ila unashindwa kukuza biashara yako kutokana na changamoto ya mtaji kuwa mdogo; tunaweza tukajadiliana namna ya kutimiza ndoto yako.

Kitakachofanyika tutaingia ubia, tutawekeza nguvu ili wewe ufanikishe lengo lako, nasi pia tusonge mbele.

Muhimu: Biashara uwe tayari ulishaianza

Kwa sasa tuanze na Arusha​
 
Tatizo la wafanyabiashara ndogondogo ni kukosa elimu na sio mtaji mpe mtaji mchoma mahindi million 10 uone kama ataweza kuizalisha
 
There is a reason banks asks for collateral au mikopo ya kitaa ni mikopo Umiza....

Achana na wafanyabiashara wadogo tu bali Majority of People in developing countries hawakopesheki...
 
Formula nitakayoitumia ni kuwapelekea mzigo na si fedha, katika kujihami na hiyo changamoto.
 
Kuna mdau alikuwa ana kijiwe cha chips na soda..., kila akienda anakuta mzigo upo anaambiwa Biashara mbaya kumbe mdau na yeye ana gunia lake la viazi, mayai na soda hapo karibu kila mzigo ukipungua anaongezea (refill)....

Sisemi issue yako haiwezekani au sio nzuri bali watanzania wa sasa tumekuwa wapuuzi wa kutupa, wizi / so called ujanjaujanja wakati ni upuuzi ndio umekuwa sifa...., Yaani tungekuwa waaminifu Biashara nyingi kama Bodaboda kuwapa watu waendeshe au kukopesha kwa riba ingekuwa one of the best businesses..., lakini sio sababu rasilimali watu sio dependable...
 
Nakubaliana na wewe, uaminifu kwa sisi ngozi nyeusi ni changamoto; ila kama umeshaligundua hilo ni vizuri kuliwekea angalizo na namna ya kulitatua
 
Wewe kwanini hizo pesa zako usifungue miradi ukatoa ajira? Hao wafanyabiashara wadogo wengi wao hela ikiongezeka lazima wachanganyikiwe. Labda uwape elimu kwanza hata kwa mwaka mzima
 
Swali lako ni sawa na kusema, kwa nini benki wasifungue biashara na kufanya kwa kutumia hizo hela za wateja.
Lengo kubwa la kutumia njia hii ni kukwepa baadhi ya changamoto (risk).
 
Back
Top Bottom