Tuwekeze kwenye elimu na kuachana na mizaha

Tuwekeze kwenye elimu na kuachana na mizaha

Joined
Mar 15, 2013
Posts
24
Reaction score
9
Hayati Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati taifa letu limepata uhuru alisema kwamba ni lazima nchi yetu kupambana na maadui wakubwa watatu yaani UMASKINI, MARADHI na UJINGA.

Baada ya kuwa na mikakati hiyo jitihada zilifanyika nyingi sana kujitahidi kushinda maadui hawa watatu na kwa wakati ule mafanikio yalionekana licha ya kwamba maadui hawa wameendelea kuwa tishio kubwa sana kwa ustawi wa nchi yetu katika zama za leo.

Tatizo kubwa ni kwamba tunajitahidi kupambana na maadui wote watatu bila mafanikio huku adui mkubwa sana ambaye ndiye anayeongoza wenzake tukimfanyia mzaha.Ni dhahiri kwamba UJINGA ni chanzo na kisababishi kikubwa cha maadui wengine yaani umaskini na maradhi.Watu ni maskini kwa sababu hawana uelewa wa kujiinua kiuchumi, vilevile maradhi yameshamiri kwa sababu watu hawana uelewa juu ya kufanya usafi na kujikinga na maradhi. Katika zama zetu sasa, tunashuhudia akili ndogo jinsi inavyotawala akili nyingi, watu wenye taaluma ndogo kuongoza watu wenye taaluma za juu zaidi, watu wasio na weledi na kazi tunawaona leo hii wakijivinjari na vyeo na kufanya maamuzi katika kazi ambayo hayana tija kwa Taifa letu, madaraka yanagawaanywa kwa baadhi ya watu kwa sababu ya urafiki, undugu na kulipana fadhira bila kuzingatia maslahi ya nchi yetu, tenda mbalimbali na zabuni zikitolewa kwa ujanja na manufaa ya wachache na matokeo yake kinachotokea ni maafa kwa wananchi.

Elimu yetu kwa sasa kwa kiasi kikubwa inawafanya watu wawe wajinga licha ya kuonekana wamesoma kwa sababu tumekiuka miiko ya zamani na kuingiza miiko ya kidigitali ambayo kuiweza ni vigumu.Kusema kweli hatuwezi kutoa elimu eti kwa kuangalia Ulaya wanatoaje elimu yao kwa sababu ya vigezo kadha wa kadha vya kisiasa, kitamaduni na kiuchumi.

Wanafunzi wamekuwa wakifanya vibaya mitihani mwaka hadi mwaka huku zikiwekwa jitihada ambazo hazionekani kuwa na tija.Huwezi kumuua chatu kwa kutumia unyasi tu zinahitajika jitihada za kitaifa kwa ujumla ili kujadili na kukubaliana aina ya elimu yenye tija tunayohitaji; zamani kulikuwa na elimu ya kujitegema ambayo ilkuwa inawafanya hata wanafunzi waliokuwa wanaishia darasa la saba kuwa na manufaa kwa jamii kwa sababu shuleni hawakufundishwa kusoma na kuandika tu bali hata stadi za maisha kama kilimo, ufugaji, ufundi, biashara tena kwa vitendo vilifundishwa kwa ufasaha.Leo kwa sababu ya mihemuko ya kisiasa na matakwa ya Mataifa wahisani elimu ya kujitegemea imefutika kiasi kwamba imefikia hatua seehemu nyingine za nchi yetu wanafunzi wakifanya usafi jamii inalalamika eti walimu ndio wafanye usafi kwa sababu watoto wao wameenda kusoma tu, swali ni kwamba nini maana ya kusoma? wanafunzi wakifundihswa masula ya ukakamavu jamii hulalamika kwamba watoto wao wanaumizwa bure, wanfunzi wakiandaa shamba la shule ni matatizo makubwa sana.Hay yote yanafanyika kwa sababu ndivyo miongozo mingi ya elimu inavyosema siku hizi. Walimu kwa sasa hawana uwezo wa kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi kwa sababu ya sheria zilizowekwa.

Wanafunzi wengi wameendelea kufanya vibaya kwa sababu kuu kwamba NIDHAMU yao kwa wakati huu ni sifuri na hakuna anayeoneka kuwajibika, walimu wamekuwa watu wa kulalamika kila wakati bial kusikilizwa na wahusika yaani serikali.

Nimalizie kwa kusema kwamba tufanye mdahalo juu ya aina ya elimu tunayoitaka wananchi kwa kuangalia manufaa ya elimu waipatayo watoto wetu.Nidhamu bora ndo uwe wimbo kwa kila shule pia elimu ya kujitegemea yenye vitendo irudishwe.
 
Back
Top Bottom