Tuweni makini na hawa wapenzi wa mtandaoni

Inawezekana hiyo chanika, muhudumu wa afya, muuza mayai ndiyo code yenyewe. Inawezekana tukio lilifanyikia kimara, yeye kasema chanika. Inawezekana mwanamke alikuwa muuza juisi ila yeye kasema mayai.
wachambuzi leo mmeamkaje maana sio kwa uchambuzi huu. Kisa cha kwanza kasema hadi mchaga na watoto wawili tuachane na hayo vipi huko kwenu kuna maji, umeme na barabara nzuri maana kama upo tanganyika na huna hizo changamoto wew sio mtanzania halisi
 
Unavyoandika utadhani ni jambo zuri tu mtu kuwa nalo!!!!!😒😒
 
Hivi gharama za kupima homa ya ini zinakwendaje?
Inategemea na ulipo na level ya hospitali.

Kama ulipo kuna hospitali ya wilaya kupima haitazidi elfu 15 na chanjo itakua elfu 10.

Wakati ukienda hospitali ya level ya juu kupimwa itaanzia elfu 30 na chanjo itaanzia hapo na zaidi.

Pamoja na gharama kubwa ila ukiwaambia unawachangia damu wanakupima free.
 
Kipimo gani hicho kiliyumba?
 
Nawaangalia tu mnaodai tiba ya ukimwi ipo.

Kuna watu maarufu sana na wana pesa na wapo Marekani na wana ukimwi hadi leo.

Kitu ambacho wengi hatukua tunajua ni kwamba virusi wa UKIMWI wakishakuingia wanavamia DNA yako na kuiunda upya huku na hao virusi wakiwa sehemu ya DNA.

Wazia mgeni amefika nyumbani kwako, anapanga samani za ndani upya, anapaka rangi ya nyumba upya, anabadili vitasa vya mlango, anabdilisha milango na anahamisha nyumba yenyewe.

Hua nashangaa watu wanadai UKIMWI usiogopwe, iogopwe homa ya ini. Homa ya ini ukiitambua mapema ukikomaa na dawa unapona. UKIMWI ukiutambua mapema that's your new identity.

Acheni masihara na UKIMWI. Wengi wenu humu mnaweza pitisha miaka hadi mitano hamjaona mtu aliyefubazwa na UKIMWI ndiyo sababu mnaandika hivi. Nimeshuhudia mgonjwa anatafutiwa drip ya fluconazole, naenda kilomita 50 kufuata drip narudi nakuta amefariki.

Nimeshuhudia mtu anakufa huku madaktari wanapambana kumuokoa mimi nipo pembeni. Yule mama alikufa macho hajafumba, alikua anapiga kwikwi kwa saa nne mfululizo mpaka umauti unamkuta.

Kisha unakutana na mtu anakuambia bora UKIMWI. Aisee
 
Ukimwi kupata dawa bado. Itakuwa ukimwi ni pigo kubwa sana kitabibu na kiimani. Russia Wana tibu cancer lakini ukimwi sijasikia kbsaa. Ukisikia Ugo kwa Hadi warussi na wajerumani wanahangaika bado ujue ni habari nyingine.
 
Mkuu,
Ukipata ukimwi na miaka 35, unaweza kuishi hadi miaka 70 kama ukiishi kwa kufuata kanuni. Hizo cases za kufa hata mwenye malaria anaweza kufa akiwa ameachama mdomo au macho yanaangalia, kufa kuna formula moja tu, uwezo wa ku-retain pumzi unapotea, iwe malaria, pressure, moyo, figo, homa ya ini na ukimwi.

Kuna magonjwa yanakupa mda wa kuishi na kutafakari maisha, lakini kuna magonjwa hayakupi huo mda, unaugua na kufa instantly. Kwa dunia ya sasa ambayo dawa zipo, ukimwi sio ugonjwa wa kutisha sana, japo unaogopesha😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…