The Giantist
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 214
- 86
Na:
MC Wenceslaus
Dodoma.
12.01.2021
Habari za leo ndugu watanzania wenzangu na wazalendo wote wa Tanzania hii! Ni matumaini yangu kuwa tunaendelea kuwajibika vema katika ujenzi wa uchumi wa nchi yetu Tanzania. Nitumie nafasi hii kuwatakia mapumziko mema ya siku ya leo hasa tunapoadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika tarehe kama ya leo yaani 12.01.1964, huko visiwani Zanzibar, Mapinduzi hayo yaliongozwa kwa ustadi mkubwa na madhubuti wa Mzee wetu muasisi wa Jamhuri ya watu huru wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid A. Karume, pamoja na wanachama wote wa Afro-Shiraz Party (ASP) kwa kushirikiana kwa karibu na wananchi wa Zanzibar.
Kwa hakika Mapinduzi hayo yameendelea kuwa Ni matukufu sio kwa sababu waliotekeleza Mapinduzi hayo ni watakatifu, la hasha! Bali itoshe kusema kuwa msukumo uliopelekea kutekelezwa kwa Mapinduzi hayo yalikuwa na dhamira nzuri na njema kwa watu wa Zanzibar (yaani matakatifu) ikiwa ni kuhakikisha kuwa wazanzibar wanapata haki sawa na heshima ndani ya nchi yao wenyewe kama ambavyo Mwenyezi Mungu aliwapatia ili waweze kuilea na kuitunza na kuilinda kisiwa chao. Dhamira hiyo pekee ndio imepelekea hata leo tuwe na nguvu ya kusema ni Mapinduzi matukufu, ambayo shabaha yake kubwa ni kuuondoa utawala wa kitumwa na wa kibaguzi uliokuwa ukitekelezwa na utawala wa usultani.
Ni miaka 57 sasa, ipo haja ya kutazama kuwa ile shabaha ya Mapinduzi haya matukufu kama imetimizwa. Na kama jibu ni ndio, je ni katika kiwango gani..? Je, inaridhisha..? Na kadhalika.... Maisha ya mzanzibar kabla ya Mapinduzi ni lazima tuyatazame na maisha ya mzanzibar baada ya Mapinduzi. Ndio kusema ipo haja ya kulinganisha maisha ya mzanzibar kwa miaka zaidi 60 wakati wa usultani, na maisha ya mzanzibar kwa miaka 57 tu mara baada ya Mapinduzi, kwa hivyo tutaweza kutathimini maendeleo ya haya Mapinduzi matukufu.
Sitaongea kwa marefu sana, ila nitajitahidi kugusa maeneo ya msingi na muhimu sana. Imezoeleka kuwa serikali ni mlezi wa Jamhuri, na kwamba itatekeleza kazi zake kwa manufaa na maslahi mapana ya Jamhuri. Ndio kusema bila Jamhuri hakuna serikali. Lakini pia ni Jamhuri ndiyo inayounda taifa kwa msingi huo, taifa yaani nchi inapata maana yake kutoka kwa wananchi na kwamba serikali ni wakala wa taifa au nchi ambayo wajibu wake ni kwa wananchi.
Taifa la Zanzibar tangu kuumbwa kwake siamini kama ilikuwa tupu! Ni nchi ile, hivyo kwa miaka mingi ilikaliwa na watu ambao waliwajibika kwa taifa hilo, kwa maana ya kuitunza kwa kuilima na kuondoa misitu isiyokuwa na tija na Kisha kuipa hadhi ya taifa lililosafi na linalokaliwa na watu. Taifa hilo liliweza kuwapa watu wake mahitaji yao ya muhimu ikiwemo mandhari mazuri, hali ya hewa Safi, mazao Safi yaliyovunwa kwenye ardhi yake, na mambo mengine mengi ya asili ambayo hayatengani na maisha ya mtu ikiwemo amani na usalama.
Wakazi wazanzibar waliishi katika maisha hayo ya urafiki na taifa lao lakini baina yao wao kwa wao. Hata hivyo, hali ilibadilika mara baada ya utawala wa sultani kuweka mizizi kwenye kisiwa cha Zanzibar, wakazi wenyeji walipoteza amani na usalama na urafiki baina yao wao na taifa lao wenyewe. Utumwa ukaanza na unyanyasaji ukashamiri, wazanzibar wakajihisi hawana thamani ndani ya taifa lao, ndugu zao waliuzwa utumwani, wapendwa na wenzi wao wakatenganishwa na taifa lao na mbele ya macho yao, vilio kwenye mashamba ya karafuu na vifo vikajitwalia makazi pamoja nao wakati wote usiku na mchana. Hayo ndiyo maisha ya mzanzibar wakati wa usultani.
Mabwana wale wa Sultani, hawakumuona mzanzibar kama binadamu anayestahili heshima, hivyo alistahili kutendewa baya zaidi. Wanawake wa kizanzibar walipotendewa matendo ya ovyo na muarabu haikuonekana kuwa ni kosa, na ikiwa atatendewa na mzanzibar mwenzake itachukuliwa kuwa ni kawaida ya tabia za wanyama pori yaani wazanzibar walifananishwa na wanyama pori! Kwa ufupi maisha ya mzanzibar wakati wa usultani ndani ya nchi yake, yalionekana ni sawa kabisa na yale masimulizi ya maisha ya roho za watu Jehanamu.
Historia ya watu wa Zanzibar ilianza kubadilika mapema katika mwaka wa 1905. Ikumbukwe kuwa ni katika mwaka huo ndipo vita vya maji maji vilizuka katika nchi za kusini na pwani ya Tanganyika, kupinga utawala wa kidhalimu wa mjerumani, vikiongozwa na Kinjekitile Ngware. Na katika mwaka huo, kule Zanzibar nyota njema yenye kuashiria uhuru wa watu wa Zanzibar kutoka kwenye makucha ya usultani iliibuka na kung'ara, ni katika mwaka huo Dawa ya kukoma kwa utumwa kwa wazanzibar ilipopatikana, ni mwaka huo ndipo alipozaliwa Mwanamapinduzi na Kiongozi wa Mapinduzi wa maisha ya wazanzibar kutoka kwenye maisha ya kitumwa na kwenda maisha huru, naye ni Sheikh Abeid Karume alizaliwa. Baada ya miaka 59 kutoka mwaka 1905, Mzee karume aliona madhira ya usultani dhidi ya maisha ya wazanzibar. Aliona suluhu ni kufanya Mapinduzi, ambayo yataleta nuru na kurudisha matumaini ya maisha yaliyo mema kwa watu wa zanzibar.
Mzee karume alitamani kuona wazanzibar wanahesabika kuwa ni watu wenye kustahili heshima na kupata huduma zote za muhimu za maisha, alitaka kuona wazanzibar wanashirikiana katika kuamua hatma ya Zanzibar yao pasipokupangiwa na Sultani, ulinzi na usalama na Maendeleo ya wazanzibar yaletwe na wazanzibar wenyewe, alitamani kuona mzanzibar anapata elimu sawa na elimu aliyokuwa akipewa Muhindi na muarabu, kutendewa sawa mbele ya jicho la haki na sheria za nchi.
Sasa ni miaka 57 tangu Mapinduzi hayo yalifanyika na kwa hakika tumeona tofauti kubwa ya maisha ya mzanzibar wa wakati wa usultani na baada ya Mapinduzi. Leo hii tunashuhudia kuwepo kwa serikali na taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kwa sababu ya mapinduzi ya Zanzibar. Maamuzi ya kuunganisha Tanganyika na Zanzibar yalitokana na wazanzibar wenyewe pamoja na watanganyika, na hiyo ndiyo ilikuwa kazi ya kwanza ya kuwaambia usultani kwamba sisi wazanzibar tunashiriki moja kwa moja katika kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa letu wenyewe. Hata hivyo, kukomeshwa kwa ubaguzi wa muafrika mzanzibar, alitazamwa mtu sawa katika jicho la sheria. Kupata huduma za jamii ikiwa ni elimu, afya na maji, ulinzi na usalama n.k yote hayo yalitolewa sawa pasipo kuwepo na ubaguzi wowote ule. Kubwa zaidi kuruhusiwa kwa watu weusi kuweza kuoa kwenye familia ya waarabu na waarabu kuoa kwenye familia ya wazanzibar waafrika.
Nipende kuhitimisha kwa kusema kuwa, Mapinduzi yale ya mwaka 1964 yalikuwa si Mapinduzi ya kuuondoa utawala wa kisultani pekee bali na kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya mzanzibar na muafrika kwa ujumla, ikumbukwe Tanzania ni moja ya matunda ya awali kabisa ya Mapinduzi hayo.
Na kwa sasa tunaona jinsi Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt. Hussein A. H. Mwinyi pamoja na Rais wa Tanzania Dkt. John P. J. Magufuli wanavyoendelea kuitekeleza dhana hiyo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar katika kufanya maboresho makubwa ya kiuchumi kwa kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na Tanzania kwa kuhakikisha nchi zetu hizi zinajitegemea kiuchumi na kwamba rasilimali za nchi zinawanufaisha wazanzibar wote pasipo ubaguzi.
Tunaona maboresho makubwa katika sekta ya elimu, afya, maji, utalii, uvuvi, usafirishaji n.k ambapo msukumo mkubwa umewekwa kuhakikisha Mapinduzi matukufu yanaendelea kuenziwa kwa vitendo. Na kwa hakika Viongozi wetu hawa wameendelea kusimamia misingi hiyo iliyowekwa na waasisi wetu kupitia chama cha ASP, sasa ni CCM. Mapinduzi ya Zanzibar yanatajwa katika jina la chama tawala yaani Chama Cha Mapinduzi na kwamba yanatekelezwa kwa mujibu wa katiba ya chama na sera ambazo zinaiongoza serikali ya Zanzibar na Tanzania.
Tuyaenzi Mapinduzi haya kwa kufanya kazi na kulipa Kodi kwa serikali, ili Mapinduzi daima yaweze kuwa na tija kwa Zanzibar na Tanzania. Hongereni sana kwa kushiriki maadhimisho haya kwa kuendelea kufanya kazi. Mapinduziiii Daimaaaa!!!
Sauti ya Mdodomia