Tuyajue Magari haya Part 2

sosolegrande

Member
Joined
Feb 23, 2015
Posts
13
Reaction score
8
Toyota vx
Toyota Land Cruiser ambapo imetokana na neno la kijapani Toyota Rando-kurūzā[SUP]?[/SUP]) ni aina ya magari yanayo tumia mfumo wa 4WD atika utendaji kazi wake yakiwa na nguvu na kasi kubwa katika swala zima la utendaji kazi wake. Uzalishwaji wa kizazi cha kwanza cha Toyota land cruiser ilianza Rasmi mwaka 1951.

TOYOTA VX FIRST GENERATION



1985 - The Direct-injection 12H-T turbodiesel engine ika anzishwa sasa kwa ajili ya kuruhusu utengenezwaji wa series mpya 70 series ambayo ndo VX sasa!!!!! HII ILIITWA PIA CRUISER DUME.

1988 - jamaa waka amua kiongezea uwezo ile petrol engine kwenda 4.0 L 3F-E EFI (Electonic Fuel Injection) engine. Ndo wakaitambulisha landcruiser FJ62G VX-Series kuruhusu sasa Land Cruiser kuzwa japan kama gari ya Abiria.

Kama utaona
Itu hapo utagundua wa japan ni noma walianza kuutumia mfumo wa EFI zaman kidogo.

Body style

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 264"]
[TR]
[TD="width: 3"][/TD]
[TD="width: 343"] Full size SUV, 4-door station wagon[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 3"][/TD]
[TD="width: 343"] Engine[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 3"][/TD]
[TD="width: 343"] 4.2 L 2F I6 (FJ60)
4.0 L 3F I6 (FJ62)
4.0 L 3F-E I6 (FJ62 from 1988)
3.4 L 3B I4 diesel (BJ60)
4.0 L 2H I6 diesel (HJ60)
4.0 L 12H-T I6 turbo diesel (HJ61)
Transmission[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 3"][/TD]
[TD="width: 343"] 4-speed H41F or H42F manual
4-speed A440F automatic
5-speed H55F manual ( hii kwa wale walio nje ya USA pekee
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


TOYOTA VX
SECOND GENERATION J80 (1990–1997)



Land cruiser 80 series ilizinduliwa rasmi octobeer 1989 pale tokyo ni ikanza kuuzwa rsmi mwaka 1994 ikiwa na mfumo mpya wa milango uitwao '' swing had swing-out back doors''.

gari hii ya kisasa zaidi kwa ipindi hicho ilipewa majina tofauti tofauti kama vile "Burbuja (Bubble) nchini Colombia na Venezuela utokana na ubabe wa gari hyo barabarani, japokuwa nchi hizo mbili nzima ilikuja kuitwa rasmi Autana.


ENGINE

4.0 L 3F-E I6

4.5 L 1FZ-FE I6
4.2 L 1HZ I6 diesel
4.2 L 1HD-T I6 turbo diesel

TRANSIMISSION

4-speed automatic

5-speed manual



TOYOTA VX series 100 (1998–2007)



Mwaka 1998 January 100 series ya Land cruiser ia anzishwa ikiwa kwa lengo la ku ireplace series 80 ambayo ilisha pita miaka 8 toka kutengenezwa kwake. Gari hili lilioneshwa mwaka 1997 october ikipewa jina la "Grand Cruiser" pale Tokyo japan motor show.

Uundaji wa mashine hii ulianza mwaka 1992 na mtindo wa mwisho ukamalizika mwaka 1994 ndo gari ikakamilika lakin ikaja ikaachiwa waka 1998, hii yote katika ku hakikisha kwamba wanatoa kitu bora zaidi. Gari hii pia ilijulikana Lexus LX 470
.

ENGINE

4.5 L 1FZ-FE I6
4.7 L 2UZ-FE V8
4.2 L 1HZ I6 diesel
4.2 L 1HD-T I6 turbo diesel

4.2 L 1HD-FTE I6 turbo diesel

TRANSIMISSION
4-speed automatic

5-speed automatic

5-speed manual


Body style

4-door wagon



TOYOTA VX V8 J200 (2007–present)


Hii ni ya 2007-2013


hii ni ya 2014 had leo

In 2002, miaka 5 ya mipango na ubunifu wa waha jamaa wa kijapani kwenye100-series platform Sadayoshi Koyari na Tetsuya Tada wakaja na zao jpya kabisa la VX V8 Uundaji wa gari hili ulianza mwaka 2002 na kuja isha rasmi mwaka 2008.

Gari ikiwa imeongezewa mifumo mingi kama
hai (active )automotive night vision system, system hii ilikua ikitumia mfumo wwa kisasa kwenye taa zake za mbele headlight projectors emitting near infrared light na CCD CAMERA ambayo hudaka matukio yote yanayoendelea nje ya gari kwa lengo la kuipa gari crediti kwenye swala zima la usalama kwani inauwezo wa kutembea ikiwa imezima taa zake usiku na ikimfanya dereva kuona vyema.

ENGINE
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 264"]
[TR]
[TD] 4.0 L 1GR-FE V6 4.6 L 1UR-FE V8[SUP][25][/SUP] 4.7 L 2UZ-FE V8[SUP][26][/SUP] 5.7 L 3UR-FE V8[SUP][27][/SUP] 4.5 L 1VD-FTV V8 turbodiesel
TRANSMISSION[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 6-speed automatic 5-speed automatic 5-speed manual
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

VX V8 YA KUANZIA MWAKA 2004 IMEKUJA IKIWA NA TRANSIMISION MBILI KWA WAKAT MMOJA YAAN GARI MOJA GIA MOJA LAKIN INA MFUMO MIWILI AUTOMATIC NA MANUAL KAZ NI WEWE KUCHAGUA TU UNATAKA UPII!!!!!


NB:
Toa pendekezo topic ijayo tulichanechane gari gani
 
Daaah series za land cruiser nimezifaidi Sana enzi hizo ding Imeneja NMC mpaka katibu mkuu wa wizara nasikia raha Sana kutumia matoleo ya land cruiser yako bomba Sana....
 
Mkuu mbona 70 series hazipo kina mkonga hadi airbags
 
ni kweli hakuna mabadiliko makubwa kwa hizi Land-Cruiser ya 2014 kwenda 2015
ila kwa ubora ni zaidi ya RR
tatuzo ya hizi Automatic ni matumizi ya mafuta Land-Cruiser kuanzia GX yanakamua hadi lita moja kwa 5.7 km
lusungo nakutafutia jibu lako la matumizi ya mafuta katika post yako ya garI ndogo (Toyota Brevis) lakini mm nilitoka kwa tofauti ya magari haya nikiendesha Dom-Dar-Dom
(Dodoma -Dar km 450 unaweza tumia lita 75 na kurudi ni km 170lt kwa LandaCruiser GX
wakati gari ndogo ya Corolla cc1490 Dar ni lita 25 ukiridi ni 50ltr)
2015 Toyota Land Cruiser: New Car Review - AutoTrader.com
 
Ndugu ahsante kwa mchanganuo,naomba unijuze juu ya toyota TX nazipenda sana hizi gari
 
Mkuu mbona 70 series hazipo kina mkonga hadi airbags

Hapa tulikua tunazungumzia land cruiser vx pekee ! Toyota nyingine tumeziacha kama hyo series 70, lexus, gx, lx, prado, tundra, hilux na zingne nying!
 
Daaah series za land cruiser nimezifaidi Sana enzi hizo ding Imeneja NMC mpaka katibu mkuu wa wizara nasikia raha Sana kutumia matoleo ya land cruiser yako bomba Sana....

nishakujua kaka.....!
 
natania tu mkuu....namfahamu aliekuwa DG wa NMC watoto wake nimesoma nao na walikuwa jirani zetu...mzee wako alikuwa DG?


No wangu alikua meneja Wa mkoa Fulani then akahamishiwa wizarani
 

Kaka unazidi kuishusha hio LC VX.....sasa mtoa review anasema siku hizi imekuwa MORE A RR???? Ushasikia LIONEL MESSI akijiita MRISHO NGASSA?? Ngassa ndio atajiita MESSSI!!
 
Kaka unazidi kuishusha hio LC VX.....sasa mtoa review anasema siku hizi imekuwa MORE A RR???? Ushasikia LIONEL MESSI akijiita MRISHO NGASSA?? Ngassa ndio atajiita MESSSI!!
Mkuu nimekupata ila nimeelezea ninayoitumia ni LC - GX na ni ya 6 cyilinder tena straight na ni Diesel
hizo VX-V8 sijawahi
ilishawahi kunipita huko Isuna Singida nikiwa 110km/h mm nikapigwa faini yenyewe ikawa imeacha hadithi kwa Traffic kwani ilikuwa zaudu ya 170km/h ndio nikaijua kuwa si ya kawaida
 
Daaah series za land cruiser nimezifaidi Sana enzi hizo ding Imeneja NMC mpaka katibu mkuu wa wizara nasikia raha Sana kutumia matoleo ya land cruiser yako bomba Sana....
NMC mzee wako hakutumia pajero kweli wewe? Hukuwa unakuja shule na pajero za NMC kabla hazijaporwa na wezi?
 
Haya madude ni hatari: usiombe sasa ukakutana na VX-V8 petrol, hapo ni mwisho wa mambo. Kwenye speed limit ya 20 haiwezi kwa kuwa inakuwa kama imesimama ndio maana mwendo ni kuanzia mia kwenda mbele!
 
NMC mzee wako hakutumia pajero kweli wewe? Hukuwa unakuja shule na pajero za NMC kabla hazijaporwa na wezi?

Ha ha ha ha,

Sio pajero mkuu ni VX hiyo ya pili rangi ya khaki
 
Ha ha ha ha,

Sio pajero mkuu ni VX hiyo ya pili rangi ya khaki
Mimi nakumbuka wakurugenzi wa NMC walitumia mapajero miaka ileeeee. Tena ndio pajero zinaingia Tanzania kwa mara ya kwanza. Kama nakuona vile ndani ya pajero ya kijivu na mistari myekundu ukishushwa shule
 
Mimi nakumbuka wakurugenzi wa NMC walitumia mapajero miaka ileeeee. Tena ndio pajero zinaingia Tanzania kwa mara ya kwanza. Kama nakuona vile ndani ya pajero ya kijivu na mistari myekundu ukishushwa shule

Mkuu sio mikoa yote sisi ilikua hiyo vx second generation aisee enzi hizo DDC mlimani park ilikua shiidah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…