Tuziangalie bei za Vifurushi kiuchumi na matokeo yake kwenye ukuaji wa 'Services'

Tuziangalie bei za Vifurushi kiuchumi na matokeo yake kwenye ukuaji wa 'Services'

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Bei za virushi hazijaongezeka, zimepaaa, thus ukipima percentage change ni zaidi ya 200%. Je kutakuwa na matokeo gani kiuchumi

1. Ikumbukwe kuwa 'services' imekuwa ikiongezeka kila uchao na huku 'production' ikiwa katika hali fulani tofauti. Kikubwa ni kuwa kulikuwa na huduma na hata wanaouza bidhaa walijazana mtandaoni kutafuta wateja au kuwahudumia wateja. Kupaa huku kwa bei hasa za MBs kutafanya gharama ya kutangaza bidhaa au huduma kuwa kubwa. Na ikumbukwe masuala ya kubandika matangazo kwenye mistimu na minara ni very old version na kwa baadhi ya huduma na bidhaa haziwezi kutegemea kukua kwa sampuli hiyo ya matangazo

Hence, wateja inabidi wachangie huduma ya bando hivyo kunaweza kuwa na slight increase ya huduma zinazopitia internet. Mathalani huduma za internet cafe zitapanda kama kwa saa ilikuwa 1000, sijui kwa sasa kwa saa itakuwa sh ngapi. kwa wale waombaji wa kazi kupitia internet cafe huko ajira portal wameathiriwa moja kwa moja

Kwa kuwa bado sina study ya kuonesha makundi ambayo yameguswa, nataja tu hayo yanayonijia kichwani

2. Kama watu watajiweka sawa na bei hizi, lazima kuwa na kugawana gharama hizo, ambapo bei za vitu vingine pia zitaathiriwa, ambayo kimsingi baada ya muda(Unknown) kutakuwa na increase of general price levels, ambayo then inaweza kuwa na madhara zaidi kwenye thamani ya fedha

FAIDA INAYOONEKANA
Faida kubwa ni kwa makampuni ya mawasiliano na serikali kwa ujumla(Kama watu watarespond vizuri)

Kiulinzi serikali itakuwa sawa kwa kuwa ni rahisi kufauatilia sms(hazina encryption) ukifananisha na whatsapp messages nk. Aidha ni rahisi kufanya filtration kwa sms kuliko aina nyingine za kuwasiliana

Andiko hili halina kitu serious, tusubiri miezi kadhaa ipite then tu-examine impact yake tukijaaliwa

Signed OEDIPUS
 
Mama Samia atuondolee "MISUKULE" yote ya awamu ya 5. Ni tatizo kwa kuzoea kuingilia kupanga bei za kila kitu nchini, haiwapi uhuru wafanyabiashara kushindana kutafuta wateja kwa kushusha bei na kwa ubora wa bidhaa.

Mataifa mengine wafanyabiashara wana uhuru wa kushusha bei wanavyotaka ili kuvutia wateja, ila huku kwetu wafanyabiashara wanapangiwa bei ili wafukuze wateja na waharibu biashara. Hakuna freedom of competition.

1) Waliua biashara Za Korosho kwa kupangia wakulima bei.

2) Waliua biashara za Fast Jet na Precision Air, kisa kumfufua "MAREHEMU AIR TANZANIA". Na bado ATCL likaendeshwa kwa hasara ya Billion 60 kuanzia 2016 - 2021.

3) Waliua biashara za Wafanyabiashara Kariakoo.

4) Wameua biashara ya mitandao ya simu kwa kuwabambikiza fine, vifurushi vilitoka kuanzia 1,500/=Tsh kwa GB 1.5 kwa week mpaka Sh 3,000/=Tsh kwa GB 1 (Na sasa ni Sh 3,000/=Tsh kwa MB 500) *tiGO. Wameua biashara za wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotegemea mitandao.

5) Wameua biashara za Makampuni Ya Ujenzi, waajiriwa warudishwa mtaani.

6) Wameua sekta ya Walimu, kuazia 2015 - 2021 hakuna mwalimu aliepewa motisha wala kuongezewa mshahara wala kuongezewa madaraja.

7) Wameuwa soko lote la ajira kwa wahitimu.

Wamedhihirisha hawana uwezo wala maarifa ya kazi zao. Fukuza wote waje mtaani waone hali ilivyo.
 
Je bei ziachwe zijipange zenyewe kwa nguvu ya soko(Forces of demand and supply)?
 
Back
Top Bottom