Kumekuwa na propaganda zinazoendelea, ambazo zinaongozwa na wanaccm, zinazodai kuwa watanzania wanaolipa kodi, eti ni kama milioni 3, ambazo ni chini ya asilimia 5 ya watanzania wote milioni 60!
Mimi nazikataa propaganda hizo za wanaccm Kwa nguvu zote, Kwa kuwa watanzania wanakamuliwa Kodi kuliko nchi nyingi sana duniani!
Tukija Kwa upande wa "data" naweza kuzikana kabisa hizo propaganda zinazosambazwa na watawala hawa wa CCM, wanazodai kuwa watanzania wachache sana ndiyo wanaolipa kodi.
Niwaulize hao watawala wa CCM, hivi hizi Kodi zinazotozwa Kwenye miamala ya simu, ambazo Kwa taarifa zao TCRA, Kuna laini za simu karibu ya milioni 60, ambazo ni sawasawa na idadi ya watanzania wote, ambao Kila kukicha wanapambana na Makato ya Kodi, zokiwemo VAT ya asilimia 18 Kwa Kila muamala wa simu, hivi hizo siyo Kodi zinazoingia Kwenye hazina yetu ya Taifa??
Hivi hizi "data" wanazotoa hawa watawala wetu wa CCM, wanazitoa wapi??
Kwa kuwa Kwa "data" zangu ni kuwa Kila mtanzania analipa Kodi, tofauti na hizo propaganda wanazozieneza hao Wana CCM kuwa ni watanzania chini ya milioni 3 ndiyo wanaolipa kodi hapa nchini
Ma - CCM ni maongo sana aisee..
They are so strategic.
Ukiona Mbunge au wabunge wa CCM wanaropoka hivi ktk Bunge la bajeti, basi tambueni kuwa yanafagia njia ya kuiengenezea uhalali serikali kuingiza kodi zingine kandamizi na za maumivu kwenye bidhaa na huduma muhimu zinazotumiwa na mamilioni ya wananchi wa kawaida.
Jiandaeni kwa bajeti ya kodi, Kodi, Kodi za maumivu.
Ni mwaka wa uchaguzi 2024 na 2025. CCM wanatafuta pesa za kampeni kupitisha vikaragosi wao kuwa viongozi wetu.
Just imagine, kuwa, Mbunge mtu mzima anasimama bungeni ndani ya chombo muhimu Cha kuishauri na kuielekeza serikali kwa niaba ya wananchi ifanye mambo yake kwa manufaa ya wananchi hawa, badala yake Mbunge huyu anakuwa source ya ukandamizaji wa wananchi waliomtuma, anasimama na kuropoka tu mambo pasipo kufanya utafiti wa kina kabla ya kusema.
Na inashangaza kuwa, serikali huchukua mawazo ya wajinga kama hawa na kuyafanyia kazi na matokeo yake huleta vurugu na mikinzano na malalamiko ktk jamii kiasi cha baadaye wabunge wenyewe Hawa kujiuliza: Tulipitishaje hiki kitu? Tulikuwa tumelala au tunasinzia?
Hapa Tanganyika kila mtu analipa Kodi. Hata mimba (watoto wakiwa bado tumboni) wanalipa kodi.
Tunatofautiana viwango tu vya kodi kulingana na tofauti ya vipato na hali ya uchumi ya mtu mmoja mmoja.
Na kanuni ya kodi inataka hivyo. Kuwa mwenye kipato kikubwa analipa zaidi ya mwenye kipato kidogo. Lakini Tanganyika ni tofauti. Wenye kipato ndio wakwepa Kodi wakubwa. Wasio nacho/wenye kipato kidogo wanakamuliwa hadi damu kulipa Kodi zao.
Na kusema kuwa Watanganganyika hatulipi kodi kama Marekani au ni asilimia 6 pekee ya Watanganganyika ndio wanalipa Kodi, huo ni uongo wa mchana kweupe.
Mfano VAT iko kwenye kila bidhaa na huduma inayotumiwa na mwanadamu, utasemaje watu hawalipi kodi?
Kodi za laini za Simu, LUKU METER, mafuta ya petrol ambapo hata kama mtu hana gari au pikipiki au chombo Cha moto, basi atakutana na kodi hiyo kwenye kwenye huduma ya usafiri na usafirishaji (nauli).
Huyu Mbunge Elibariki Kingu ni mwongo na hajafanya utafiti wake vyema. Apuuzwe tu..
Infact katika nchi ambayo watu wake wanatozwa kodi nyingi na kubwakubwa lakini pasipo kuona matunda ya kodi zao hizo ktk viwango vinavyotakiwa katika huduma wanazopatiwa na serikali yao, basi nchi hiyo ni Tanganyika.
Huko Marekani na nchi zingine zilizokwisha kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi ni kweli wanalipa kodi. Lakini tofauti yao na sisi ni kuwa, watu wanaona kwa uwazi matunda ya kodi zao. Hakuna viongozi kula au kuiba pesa za walipa Kodi na kuachwa free wakitamba na kufurahia utajiri wa wuzi. Vipi hapa Tanganyika?
Na sababu ya hiyo👆👆ni UFISADI na RUSHWA. Kwamba pesa nyingi za Kodi huibiwa na viongozi wa CCM kwa kushirikiana na matajiri wao wachache. Na huachwa wakitamba tu mitaani kulingishia watu.
Na ukiona kauli za wabunge wa dizaini ya Elibariki Kingu zikitangulia ktk kipindi hiki cha Bunge la bajeti, basi tambueni kuwa ni maandalizi ya kuingizwa kwa kodi mpya za maumivu kwa wananchi kwenye bidhaa na huduma muhimu zinazotumiwa na mamilioni ya watu kama umeme, simu, mafuta ya petrol nk huku serikali ikiacha eneo muhimu la Maliasili (natural resources) kama misitu, madini, bandari nk ambalo ndilo linalopaswa kuingiza mapato makubwa ya nchi pasipo kumbagaza mwananchi masikini yakiachwa mikononi mwa matajiri wa dunia bure kabisa.