Tuzikatae propaganda za CCM, wanazodai kuwa Watanzania chini ya asilimia 5 ndiyo wanaolipa kodi nchini!

Tuzikatae propaganda za CCM, wanazodai kuwa Watanzania chini ya asilimia 5 ndiyo wanaolipa kodi nchini!

Unajua maana "Kodi" au unajua tu kuanzisha nyuzi hata kwa jambo usilolijua?
Haya wewe "mjuaji" nipe definition ya Kodi, maana yake nini??😎

Ni kwanini basi, Kila ninapofanya miamala ya simu, nakuta VAT ya asilimia 18, niambie kama hiyo siyo Kodi, ni kitu Gani hicho??😚
 
Hapo kwenye mafuta karibu kila siku nanunua mafuta na mashine zinatoa risiti
Karibu kila siku nafanya miamala ya kutuma, kutoa, na kulipa na huko nakatwa kodi moja kwa moja iwe ndogo au kubwa lakini nalipa kodi.

Sasa iweje mbunge asimame bungeni asema watanzania mil 3 tu ndio wanalipa kodi.
Sasa hiyo ni item 1 tuu yenye udhibiti,Je hizo ambazo haziko kwenye mifumo? Hapo ndio inatakiwa itashi na uelewa wa mnunuzi kudai risiti,ukidai muizaji hawezi kukataa
 
Kuna kodi za Aina nyingi, nafikiri ilitolengwa hapo ni kodi kwenye kipato cha mtu. Kwa mfano mfanyakazi hukatwa PAYE kwenye mshahara wake kabla hata hajaanza kuutumia na ataendelea kulipa tozo na kodi nyingine atakapokuwa anautumia.. kama VAT, tozo za miamala, n.k.
Sasa kwenye kodi ya kipato ndio nafikiri ni wachache ndio wanaolipa tena sanasana wafanyakazi ndio wanalipishwa kodi stahili ila sekta nyingine hazina utaratibu madhubuti kubana wote wenye kipato chochote walipe kodi kwenye mapato yao.
Embu tuambie wakulima wadogowadogo kwa mfano ambao ni asilimia kubwa ya watanzania, wanalipa kodi gani ya kipato wanachopata baada ya kuuza mazao yao? Wafanyabiashara wangapi wadogo wanaolipa kodi halali kwenye mapato yao?
Somo la kodi ni Pana sana... kabla ya kuleta hoja ni bora kulifanyia utafiti kulielewa vizuri.
 
Haya wewe "mjuaji" nipe definition ya Kodi, maana yake nini??😎

Ni kwanini basi, Kila ninapofanya miamala ya simu, nakuta VAT ya asilimia 18, niambie kama hiyo siyo Kodi, ni kitu Gani hicho??😚
Usitumie MB zako kuingia JF tu. Zitumie kujielimisha pia.
 
Kuna kodi za Aina nyingi, nafikiri ilitolengwa hapo ni kodi kwenye kipato cha mtu. Kwa mfano mfanyakazi hukatwa PAYE kwenye mshahara wake kabla hata hajaanza kuutumia na ataendelea kulipa tozo na kodi nyingine atakapokuwa anautumia.. kama VAT, tozo za miamala, n.k.
Sasa kwenye kodi ya kipato ndio nafikiri ni wachache ndio wanaolipa tena sanasana wafanyakazi ndio wanalipishwa kodi stahili ila sekta nyingine hazina utaratibu madhubuti kubana wote wenye kipato chochote walipe kodi kwenye mapato yao.
Embu tuambie wakulima wadogowadogo kwa mfano ambao ni asilimia kubwa ya watanzania, wanalipa kodi gani ya kipato wanachopata baada ya kuuza mazao yao? Wafanyabiashara wangapi wadogo wanaolipa kodi halali kwenye mapato yao?
Somo la kodi ni Pana sana... kabla ya kuleta hoja ni bora kulifanyia utafiti kulielewa vizuri.
Ilo sasa ni tatizo lao wenyewe.kwasababu hawataki kubadilika ili kila sekta ishiriki kwenye kodi.Tunalalamika walipa kodi ni wachache wakati huo huo tunabana baadhi ya shughuli za kiuchumi za wananchi.Ziko biashara huwezi kufanya masaa 24 kwasababu za kijinga tu wakati zingeweza kuingiza fedha kibao.sasa hiyo kodi italipwaje.Tatizo lingine liko kwenye matumizi.matumizi yakiwa mabovu lazima kipato kionekane hakitoshi.
 
swala la uelewa na ufahamu wa masuala ya kodi ni dhahiri liko chini ya wastani kwa kuzingatia tu, mfano wa mtoa hoja na baadhi ya wachangiaji katika hoja hii mezani 🐒

nafurahi kuona wengi wanajipambanua kinagaubaga kwamba hawana uelewa wala ufahamu wa kutosha juu ya masuala mbalimbali ya kodi 🐒

Na huu utakua msingi au mwanzo muhimu sana, wa kuona kwamba ipo haja , sababu au ulazima wa somo la kodi kuwa ni la Lazima kuanziya chekechea, ili kuimpact nature ya kupenda kulipa kodi, kujenga msingi imara wa uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya kodi stahiki ambazo mlipakodi anawajibika kuzilipa, na sio hiki ambacho mnapeana matumaini ati ndio kodi 🐒
Wewe sasa ungeweka wazi hapa- ni nani ambaye halipi kodi? Na kama ccm ambao ndio wanaongoza serikali wanaweza kusema 5% ya waTanzania ndio wanalipa kodi, sasa wao wanafanya nini? Kama ni hivyo ni wazi kazi imewashinda.
 
Mambo ya mawasiliano Yana alternative na sio sehemu kubwa inayotoa Mapato Kwa Serikali ukilinganisha na manunuzi ya bidhaa Moja kwa Moja ambapo naweza kukuonesha list ya biashara zinazotumiwa zaidi na ndio huko watu Hawalipi kodi.

Angalia hapa chini,hizi bidhaa bila kutoa na kudai risiti ni kazi bure Mapato yanapotea 👇👇

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1683735734795083776?t=xVqzpDitAcbQYKpXzTOkzQ&s=19

Just imagine bidhaa za Trilioni 36 ziliingizwa ndani kutoka Nje,Sasa kwenye manunuzi ya kawaida Serikali ilioata Kodi kiasi gani? Unakuta hata Trilioni 10 haijafika

Hizi bidhaa ulizoainisha, ni biashara kubwa ambazo kama serikali Ina nia thabiti ya kukusanya kodi Hawa wafanyabiashara hawawezi kukwepa. Sio kama zile biashara za rejareja mitaani. Kwa hiyo wanaosema ni 5% tu ya watu wanalipa kodi, hao hao ndio wanawakula rushwa na kutoa makadirio ya chini ya kodi kuliko uhalisia.
 
Kumekuwa na propaganda zinazoendelea, ambazo zinaongozwa na wanaccm, zinazodai kuwa watanzania wanaolipa kodi, eti ni kama milioni 3, ambazo ni chini ya asilimia 5 ya watanzania wote milioni 60!

Mimi nazikataa propaganda hizo za wanaccm Kwa nguvu zote, Kwa kuwa watanzania wanakamuliwa Kodi kuliko nchi nyingi sana duniani!

Tukija Kwa upande wa "data" naweza kuzikana kabisa hizo propaganda zinazosambazwa na watawala hawa wa CCM, wanazodai kuwa watanzania wachache sana ndiyo wanaolipa kodi.

Niwaulize hao watawala wa CCM, hivi hizi Kodi zinazotozwa Kwenye miamala ya simu, ambazo Kwa taarifa zao TCRA, Kuna laini za simu karibu ya milioni 60, ambazo ni sawasawa na idadi ya watanzania wote, ambao Kila kukicha wanapambana na Makato ya Kodi, zokiwemo VAT ya asilimia 18 Kwa Kila muamala wa simu, hivi hizo siyo Kodi zinazoingia Kwenye hazina yetu ya Taifa??

Hivi hizi "data" wanazotoa hawa watawala wetu wa CCM, wanazitoa wapi??

Kwa kuwa Kwa "data" zangu ni kuwa Kila mtanzania analipa Kodi, tofauti na hizo propaganda wanazozieneza hao Wana CCM kuwa ni watanzania chini ya milioni 3 ndiyo wanaolipa kodi hapa nchini
Kodi inalipwa na kila mlaji wa mwisho !
Mpaka mtoto atakayenunua pipi au biskuti atakuwa ameshalipia kodi iliyotozwa kwenye hizo bidhaa !
 
Hizi bidhaa ulizoainisha, ni biashara kubwa ambazo kama serikali Ina nia thabiti ya kukusanya kodi Hawa wafanyabiashara hawawezi kukwepa. Sio kama zile biashara za rejareja mitaani. Kwa hiyo wanaosema ni 5% tu ya watu wanalipa kodi, hao hao ndio wanawakula rushwa na kutoa makadirio ya chini ya kodi kuliko uhalisia.
Mfanyabiashara anakwepa kama wewe mnunuzi wa mwisho hudai risiti
 
Hata kama ni kweli.

Mwenye jukumu la kufanya Watanzania 80-90% walipe Kodi ni Nani ?

Hiyo Kodi toka kwa hao 5% inafanya nini?
 
Wewe sasa ungeweka wazi hapa- ni nani ambaye halipi kodi? Na kama ccm ambao ndio wanaongoza serikali wanaweza kusema 5% ya waTanzania ndio wanalipa kodi, sasa wao wanafanya nini? Kama ni hivyo ni wazi kazi imewashinda.
niwe hivyo mara ngapi sasa 🐒

taarifa ya serikali ni sahihi,
wasio lipa kodi ni wengi ukilinganisha na wanao lipa kodi. Na hii ni kutokana na aidha uelewa mdogo juu ya masuala ya kodi, kukwepa kulipa kodi kwa kujua au kutokujua, kutokufahamu jinsi ya kulipa kodi, na sababu nyingine zinazofanana na hizo 🐒

hapa suala la kushindwa halipo wala sio la kufikiria kabisaa. Hapa suala ni kuhakikisha kila Mtanzania analipa kodi na kuelewa kwamba huo ni wajibu wake 🐒
 
Hata kama ni kweli.

Mwenye jukumu la kufanya Watanzania 80-90% walipe Kodi ni Nani ?

Hiyo Kodi toka kwa hao 5% inafanya nini?
Kama wenyewe watawala wa CCM wanakiri kuwa 95% ya watanzania hawalipi Kodi, tafsiri yake ni kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwaongoza watanzania na inalazimika seriksli hii ya CCM iachie madaraka Ili chama kingine ambacho kitakuwa "serious" kipewe madaraka ya kuongoza nchi hii😁
 
Kila Mtanzania analipa kodi/tozo/ushuru/unyang'anyi kila sekunde anayopumua.Hii ipo direct or indirect payments.Kila huduma apatayo mtu/mwananchi Mtanzania hulipa kodi. Ukinunua vocha,maandazi,bia,ukilipa nauli yoyote,chakula,kinywaji,huduma ya maliwato,nyumba ya wageni nk kote kuna kodi/tozo na unyang'anyi mtupu!Kuwaamini CCM na miuongouongo yao ni kujiunga na wendawazimu wanaofaidi mfumo wa kijambazi.
Kuna tozo nyingine umeisahau tunayotozana sisi kwa sisi raia bila risiti.
 
Back
Top Bottom