Tuzikatae propaganda za CCM, wanazodai kuwa Watanzania chini ya asilimia 5 ndiyo wanaolipa kodi nchini!

Unajua maana "Kodi" au unajua tu kuanzisha nyuzi hata kwa jambo usilolijua?
Haya wewe "mjuaji" nipe definition ya Kodi, maana yake nini??😎

Ni kwanini basi, Kila ninapofanya miamala ya simu, nakuta VAT ya asilimia 18, niambie kama hiyo siyo Kodi, ni kitu Gani hicho??😚
 
Sasa hiyo ni item 1 tuu yenye udhibiti,Je hizo ambazo haziko kwenye mifumo? Hapo ndio inatakiwa itashi na uelewa wa mnunuzi kudai risiti,ukidai muizaji hawezi kukataa
 
Nadhani wanamaanisha PAYE ( Pay As You Earn)
 
Kuna kodi za Aina nyingi, nafikiri ilitolengwa hapo ni kodi kwenye kipato cha mtu. Kwa mfano mfanyakazi hukatwa PAYE kwenye mshahara wake kabla hata hajaanza kuutumia na ataendelea kulipa tozo na kodi nyingine atakapokuwa anautumia.. kama VAT, tozo za miamala, n.k.
Sasa kwenye kodi ya kipato ndio nafikiri ni wachache ndio wanaolipa tena sanasana wafanyakazi ndio wanalipishwa kodi stahili ila sekta nyingine hazina utaratibu madhubuti kubana wote wenye kipato chochote walipe kodi kwenye mapato yao.
Embu tuambie wakulima wadogowadogo kwa mfano ambao ni asilimia kubwa ya watanzania, wanalipa kodi gani ya kipato wanachopata baada ya kuuza mazao yao? Wafanyabiashara wangapi wadogo wanaolipa kodi halali kwenye mapato yao?
Somo la kodi ni Pana sana... kabla ya kuleta hoja ni bora kulifanyia utafiti kulielewa vizuri.
 
Haya wewe "mjuaji" nipe definition ya Kodi, maana yake nini??😎

Ni kwanini basi, Kila ninapofanya miamala ya simu, nakuta VAT ya asilimia 18, niambie kama hiyo siyo Kodi, ni kitu Gani hicho??😚
Usitumie MB zako kuingia JF tu. Zitumie kujielimisha pia.
 
Ilo sasa ni tatizo lao wenyewe.kwasababu hawataki kubadilika ili kila sekta ishiriki kwenye kodi.Tunalalamika walipa kodi ni wachache wakati huo huo tunabana baadhi ya shughuli za kiuchumi za wananchi.Ziko biashara huwezi kufanya masaa 24 kwasababu za kijinga tu wakati zingeweza kuingiza fedha kibao.sasa hiyo kodi italipwaje.Tatizo lingine liko kwenye matumizi.matumizi yakiwa mabovu lazima kipato kionekane hakitoshi.
 
Wewe sasa ungeweka wazi hapa- ni nani ambaye halipi kodi? Na kama ccm ambao ndio wanaongoza serikali wanaweza kusema 5% ya waTanzania ndio wanalipa kodi, sasa wao wanafanya nini? Kama ni hivyo ni wazi kazi imewashinda.
 
Hizi bidhaa ulizoainisha, ni biashara kubwa ambazo kama serikali Ina nia thabiti ya kukusanya kodi Hawa wafanyabiashara hawawezi kukwepa. Sio kama zile biashara za rejareja mitaani. Kwa hiyo wanaosema ni 5% tu ya watu wanalipa kodi, hao hao ndio wanawakula rushwa na kutoa makadirio ya chini ya kodi kuliko uhalisia.
 
Kodi inalipwa na kila mlaji wa mwisho !
Mpaka mtoto atakayenunua pipi au biskuti atakuwa ameshalipia kodi iliyotozwa kwenye hizo bidhaa !
 
Mfanyabiashara anakwepa kama wewe mnunuzi wa mwisho hudai risiti
 
Hata kama ni kweli.

Mwenye jukumu la kufanya Watanzania 80-90% walipe Kodi ni Nani ?

Hiyo Kodi toka kwa hao 5% inafanya nini?
 
Wewe sasa ungeweka wazi hapa- ni nani ambaye halipi kodi? Na kama ccm ambao ndio wanaongoza serikali wanaweza kusema 5% ya waTanzania ndio wanalipa kodi, sasa wao wanafanya nini? Kama ni hivyo ni wazi kazi imewashinda.
niwe hivyo mara ngapi sasa πŸ’

taarifa ya serikali ni sahihi,
wasio lipa kodi ni wengi ukilinganisha na wanao lipa kodi. Na hii ni kutokana na aidha uelewa mdogo juu ya masuala ya kodi, kukwepa kulipa kodi kwa kujua au kutokujua, kutokufahamu jinsi ya kulipa kodi, na sababu nyingine zinazofanana na hizo πŸ’

hapa suala la kushindwa halipo wala sio la kufikiria kabisaa. Hapa suala ni kuhakikisha kila Mtanzania analipa kodi na kuelewa kwamba huo ni wajibu wake πŸ’
 
Hata kama ni kweli.

Mwenye jukumu la kufanya Watanzania 80-90% walipe Kodi ni Nani ?

Hiyo Kodi toka kwa hao 5% inafanya nini?
Kama wenyewe watawala wa CCM wanakiri kuwa 95% ya watanzania hawalipi Kodi, tafsiri yake ni kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwaongoza watanzania na inalazimika seriksli hii ya CCM iachie madaraka Ili chama kingine ambacho kitakuwa "serious" kipewe madaraka ya kuongoza nchi hii😁
 
Kuna tozo nyingine umeisahau tunayotozana sisi kwa sisi raia bila risiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…