Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuhamasishane tuingie mtaani jamani hatutatoka kwenye hali hii!Kupanda kwa bei ya dhahabu, tanzanite na vyote made in Tanzania hakujawahi kuakisiwa popote positively katika nchi hii.
Kote upigaji ndiyo ulio kipaumbele.
Serikali kupitia LATRA ilitangaza bei mpya za nauli kwa kuzingatia diesel @ 2,800/- wakiyataka mabasi kutokutumia nauli hizo kabla ya 14 May.
Hadi 14 May wenye mabasi waendelee kuvuna hasara japo wao serikali hata huwa hawa subiri hata yale ya siku 27 tu ya store kutumika.
Kwamba wao serikali ndiyo waseme wanasimamia maslahi ya mlaji? Huu si ni usanii tu?
Tulipo sasa bei za mafuta zimepanda tena kwa karibu 600/- @ Lita.
Hili si la vyama tena.
Wananchi - twafa!
Achia mbali rushwa za polisi ambazo ni rasmi majiani, ushuru usio tija, gharama za ving'amuzi, faini za kubambikiziana nk, sisi walaji wa mwisho tunasalimikia wapi?
-----------
Source: Bei mpya ya petroli, dizeli hii hapa!
Kwa hakika bila kusimama imara tusishangae kuambiwa lita moja imefika 10,000/-.Tuhamasishane tuingie mtaani jamani hatutatoka kwenye hali hii!
🤣🤣🤣Hata Burundi nilipotakiwa kuhamia na waziri mwenye dhamana mwigulu sikwenda sembuse kwa amri ya kinyangarika wewe?
Hizi ni bei za Aprili. Nilisema bei hizi wakati ule.Zawadini huko Zenji hizi ndiyo bei zenu na vigezo na masharti haya kuzingatiwa?
Yawezekana Zanzibar hawahitaji Katiba Mpya sasa
Ni dhahiri kuwa Zenji kumenoga!
Hizi ni bei za Aprili. Nilisema bei hizi wakati ule.
expand...Lita ya petroli kwa sasa ni zaidi ya shilingi 2640.
Ni vizuri kuangalia bei za mwezi Mei. Hata hivyo bei zinaweza zikawa ndogo kidogo huku kwani serikali imeondoa baadhi ya makato ambayo Bara wanaita TOZO.
Jee hili linaondoa madai ya katiba mpya? Na katiba ipi? Huku kwetu tuna katiba mbili ambazo zinaenda kwa pamoja, yaani ya Tanzania na ile ya Zanzibar.
Kwa mantiki hiyo sio vibaya kusema Zanzibar kumenoga ila sio sahihi kusema Wazanzibari hawataki katiba mpya.
Inapokuja suala la misimamo juu ya katiba mpya, Wazanzibari ni wa kupigiwa mfano. Hivi ni Mbara gani anaweza/ameweza/aliweza kusamehe nafasi nyeti kwa msimamo wa kisiasa na kupigania haki ya Tanzania. Huku Zanzibar iko mifano mingi.
Wacha Kaizari aitwe Kaizari. Huku kwetu tunasema "mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni"