SoC02 Tuzikumbuke na Shule za Msingi

SoC02 Tuzikumbuke na Shule za Msingi

Stories of Change - 2022 Competition

mrdocumentor

Member
Joined
Nov 27, 2021
Posts
45
Reaction score
56
Nimekuwa nikijiuliza Kwa Muda mrefu sana kuhusu Hali ya shule zetu za msingi. Serikali yetu imefanya jitihada kubwa sana katika kuhakikisha takribani kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi. Jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno. Lengo la kufanya hivyo lilikuwa ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora ili iweze kumnufaisha yeye mwenyewe na taifa kwa ujumla.

Lakini pia serikali imehakikisha takribani kila kata inakuwa na shule ya sekondari ili wale watoto wanaotoka shule ya msingi wasisafiri umbali mrefu kwa ajili ya masomo ya sekondari pale wanapohitimu masomo ya msingi. Lakini pia serikali imeweka mazingira mazuri pia kwa wale watakao faulu kidato cha nne waweze kujiendeleza kimasomo yaani kidato cha tano na sita.Lakini pia katika sekta hii serikali imejitahidi kuweka miundombinu mizuri na ya kisasa katika ngazi ya vyuo vikuu pamoja na vyuo vya kati, lengo ni kuhakikisha hawa vijana tuliotoka nao huku chini tunapanda nao hadi juu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Turudi tena kwenye shule za msingi
Kama wote mna kumbukumbu nzuri mtakubaliana na mimi kuwa mwaka 2016 kulitokea changamoto mbalimbali katika sekondari zetu za serikali changamoto ambazo zilisababishwa na ongezeko la udahili wa wanafunzi mara tu baada ya kutangazwa kuwa elimu ni bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Mfano wa changamoto hizo ni kama vile uchache wa madawati, Upungufu wa walimu na mfano wa hizo.

Serikali kwa kushirikiana na wananchi walikuwa bega kwa bega ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa mapema ili watoto waweze kupata elimu bora kwa manufaa ya Taifa. Serikali ilianzisha miradi mbalimbali ya kuongeza madarasa lakini pia wananchi walitumia nguvu zao wenyewe kuhakikisha janga hilo linaisha. Lakini pia jitihada hizo vile vile huwa zinafanyika katika kuhakikisha elimu ya juu pia inakuwa na mazingira bora.

61ec8ead60b014dc5932dfd2e0a11aef.png

Picha kutoka mtandaoni

“Mbona kama tunasukia ukili jikoni?”
Nikisema hivyo namaanisha kuwa msusi anaesukia ukili jikoni hata siku moja hawezi kumaliza ususi wake kwa mafanikio.

Ni kama vile jukumu la serikali liliishia pale kwenye kujenga shule za msingi tu.

Hivi hili suala la uchakavu wa majengo na miundombinu ya shule za msingi nauona mimi Peke yangu?
Hakika hali ni mbaya sana katika shule hizi za msingi sio za vijijini wala za mjini zote zina hali mbaya sana tena Sana. Unapita eneo la shule kama si kusikia sauti za wanafunzi unaweza kuhitimisha kwa kusema hili ni jumba bovu ambalo hawaishi watu. Kuta zina hali mbaya, mabati hayatamaniki tena hapo bado hujaingia kwa walimu au wanafunzi wanaoishi katika mazingira hayo kuwauliza changamoto zingine wanazopitia lakini tayari unakuwa umekinai kusema “hapa wanateseka” kwa changamoto ulizoziona nje tu.

66327c1f4c87237545ed78a97f878b03.png

Picha kutoka mtandaoni

Ndio hawa ambao tunatarajia waje kuendesha hii nchi, lakini pia ndio huku huku ambako sisi tumetoka.
Mi naona hamna ubaya au dhambi yeyote ikiwa mtu ataweka mazingira mazuri ya kule alikotoka. Lakini pia ni Sisi ambao tuna jukumu la kusafisha njia ili vijana wetu wapite bila shida.

Naunga mkono suala la kuboresha miundombinu ya elimu ya juu lakini hiyo haina maana ikiwa tutasahau kuboresha na hapa chini kwa sababu hao mnaowaandalia mazingira uko juu ndio hawa ambao mmewapotezea hapa chini sijui watafikaje uko bila msaada wenu. Mnatakiwa kukumbuka kuwa hata hao walimu hawawezi kufurahia kazi yao na kufundisha kwa moyo wote ikiwa mazingira ni mabaya hivi.

bcca1ae2f577d9d9e2e8bdc6ef26f055.png

Picha kutoka mtandaoni

Ripoti ya (Tamisemi) ya Takwimu msingi (Best 2021) ilionyesha idadi ya walimu wa shule za msingi kati ya mwaka 2017 hadi 2021 ilipungua kwa asilimia 4.07. Zipo sababu nyingi ambazo Tunaweza kusema kuwa zimesababisha walimu wetu kupungua. Unaweza kupata mshangao kidogo kwa sababu Tanzania tuna walimu wengi sana kwanini walimu wapungue? Tena mwalimu ambae ameajiriwa na serikali Kwanini aache kazi au wanapungua kwa namna gani? Wanaenda wapi? Na kama kuna Sehemu wanaenda wanafuata nini ambacho kwenye shule zetu sisi hatuna?

Moja ya vitu vinavyoweza kumfanya mfanyakazi yeyote aendelee kufanya kazi katika ofisi yako ni mazingira mazuri ya kufanya kazi. Kama mazingira ya shule zetu za msingi ndio yapo hivyo sio jambo la ajabu kuona walimu wetu wanatukimbia tena endapo hatutazinduka mapema na kuweka mazingira mazuri kwa walimu na wanafunzi wetu tutarajie walimu kupungua zaidi ya hiyo asilimia 4.07. Kwa hali ilivyo usione ajabu mtoto kukataa shule kwa sababu hajaona kama shule ni Sehemu salama ya yeye kuishi ikumbukwe kuwa hawa ni watoto kila kitu ili wafanye vizuri wanahitaji kushawishiwa.

Tufanye nini?
Jambo la msingi hapa la kufanya ni kuhakikisha serikali inaweka bajeti ya kutosha kwa ajili ya ukarabati wa hizi shule lakini pia kuondoa hii hali ya kuzisahau shule hizi basi iundwe hata tume ambayo itazisemea shule hizi pale zinapopata changamoto kama hizi lakini pia tume ndo itaweka mikakati madhubuti ya ukarabati wa shule hizi.

Lakini hayo yote yanaweza kufanyika ila ikiwa serikali haitaamua kulibeba hili kama janga basi hamna kitu kitafanyika. Serikali kama ambavyo iliamua kuwashirikisha wananchi katika kutatua changamoto za sekondari basi wakiamua kuwashirikisha na kuweka kampeni na kuzisimamia basi hili linaweza kwisha mara moja.

Kwa sasa shule za msingi yaani walimu na wanafunzi wao wana deni kwetu kwani richa ya hizo changamoto zote wanazopitia bado wanajeshi hawa wamepambana na wanaendelea kupambana kufanya vizuri hii inaonyesha ni wazi kuwa ikiwa tutaweka mazingira mazuri ya kundi hili basi wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hapa.

Pongezi
Hongereni walimu wa shule za msingi kwa kazi kubwa mnayoifanya tena mnaifanya katika mazingira magumu mno.

Serikali na wananchi wake tunatambua mchango wenu.

Ahsanteni
 
Upvote 5
Hili andiko limenigusa kwel kweli...mchango wa elimu ya msingi katika maisha yetu Ni mkubwa mno. Hakuna kijana au mzee wa Sasa ambae haujui umuhimu wa shule za msingi. Sio muajiriwa wala muajiri ambae amefika alipofika bila kupitia huko. Na pia ikumbukwe si serikali tu yenye dhima ya kuivaa hii CHANGAMOTO peke yao. Wito wangu Ni kwa watanzania wote waguswao, taasis binafsi, mashirika ya dini na ya umma. Sote kwa pamoja tushirikiane kuitatua changamoto hii kwani Tanzania yetu ya kesho inatengenezwa na msingi imara wa leo.
 
Ni kweli kabisa ikiwa wote tutashirikiana changamoto hizo zitaisha
 
Nimekuwa nikijiuliza Kwa Mda mrefu sana kuhusu Hali ya shule zetu za msingi. Serikali yetu imefanya jitihada kubwa sana katika kuhakikisha takribani kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi. Jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno. Lengo la kufanya hivyo lilikuwa ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora ili iweze kumnufaisha yeye mwenyewe na taifa kwa ujumla.

Lakini pia serikali imehakikisha takribani kila kata inakuwa na shule ya sekondari ili wale watoto wanaotoka shule ya msingi wasisafiri umbali mrefu kwa ajili ya masomo ya sekondari pale wanapohitimu masomo ya msingi. Lakini pia serikali imeweka mazingira mazuri pia kwa wale watakao faulu kidato cha nne waweze kujiendeleza kimasomo yaani kidato cha tano na sita.Lakini pia katika sekta hii serikali imejitahidi kuweka miundombinu mizuri na ya kisasa katika ngazi ya vyuo vikuu pamoja na vyuo vya kati, lengo ni kuhakikisha hawa vijana tuliotoka nao huku chini tunapanda nao hadi juu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Turudi tena kwenye shule za msingi
Kama wote mna kumbukumbu nzuri mtakubaliana na mimi kuwa mwaka 2016 kulitokea changamoto mbalimbali katika sekondari zetu za serikali changamoto ambazo zilisababishwa na ongezeko la udahili wa wanafunzi mara tu baada ya kutangazwa kuwa elimu ni bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Mfano wa changamoto hizo ni kama vile uchache wa madawati, Upungufu wa walimu na mfano wa hizo.

Serikali kwa kushirikiana na wananchi walikuwa bega kwa bega ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa mapema ili watoto waweze kupata elimu bora kwa manufaa ya Taifa. Serikali ilianzisha miradi mbalimbali ya kuongeza madarasa lakini pia wananchi walitumia nguvu zao wenyewe kuhakikisha janga hilo linaisha. Lakini pia jitihada hizo vile vile huwa zinafanyika katika kuhakikisha elimu ya juu pia inakuwa na mazingira bora.

View attachment 2352160Picha kutoka mtandaoni

“Mbona kama tunasukia ukili jikoni?”
Nikisema hivyo namaanisha kuwa msusi anaesukia ukili jikoni hata siku moja hawezi kumaliza ususi wake kwa mafanikio.
Ni kama vile jukumu la serikali liliishia pale kwenye kujenga shule za msingi tu.
Hivi hili suala la uchakavu wa majengo na miundombinu ya shule za msingi nauona mimi Peke yangu?
Hakika hali ni mbaya sana katika shule hizi za msingi sio za vijijini wala za mjini zote zina hali mbaya sana tena Sana. Unapita eneo la shule kama si kusikia sauti za wanafunzi unaweza kuhitimisha kwa kusema hili ni jumba bovu ambalo hawaishi watu. Kuta zina hali mbaya, mabati hayatamaniki tena hapo bado hujaingia kwa walimu au wanafunzi wanaoishi katika mazingira hayo kuwauliza changamoto zingine wanazopitia lakini tayari unakuwa umekinai kusema “hapa wanateseka” kwa changamoto ulizoziona nje tu.

View attachment 2352181
Picha kutoka mtandaoni

Ndio hawa ambao tunatarajia waje kuendesha hii nchi, lakini pia ndio huku huku ambako sisi tumetoka.
Mi naona hamna ubaya au dhambi yeyote ikiwa mtu ataweka mazingira mazuri ya kule alikotoka. Lakini pia ni Sisi ambao tuna jukumu la kusafisha njia ili vijana wetu wapite bila shida.
Naunga mkono suala la kuboresha miundombinu ya elimu ya juu lakini hiyo haina maana ikiwa tutasahau kuboresha na hapa chini kwa sababu hao mnaowaandalia mazingira uko juu ndio hawa ambao mmewapotezea hapa chini sijui watafikaje uko bila msaada wenu. Mnatakiwa kukumbuka kuwa hata hao walimu hawawezi kufurahia kazi yao na kufundisha kwa moyo wote ikiwa mazingira ni mabaya hivi.

View attachment 2352183

Picha kutoka mtandaoni

Ripoti ya (Tamisemi) ya Takwimu msingi (Best 2021) ilionyesha idadi ya walimu wa shule za msingi kati ya mwaka 2017 hadi 2021 ilipungua kwa asilimia 4.07. Zipo sababu nyingi ambazo Tunaweza kusema kuwa zimesababisha walimu wetu kupungua. Unaweza kupata mshangao kidogo kwa sababu Tanzania tuna walimu wengi sana kwanini walimu wapungue? Tena mwalimu ambae ameajiriwa na serikali Kwanini aache kazi au wanapungua kwa namna gani? Wanaenda wapi? Na kama kuna Sehemu wanaenda wanafuata nini ambacho kwenye shule zetu sisi hatuna?.
Moja ya vitu vinavyoweza kumfanya mfanyakazi yeyote aendelee kufanya kazi katika ofisi yako ni mazingira mazuri ya kufanya kazi. Kama mazingira ya shule zetu za msingi ndio yapo hivyo sio jambo la ajabu kuona walimu wetu wanatukimbia tena endapo hatutazinduka mapema na kuweka mazingira mazuri kwa walimu na wanafunzi wetu tutarajie walimu kupungua zaidi ya hiyo asilimia 4.07. Kwa hali ilivyo usione ajabu mtoto kukataa shule kwa sababu hajaona kama shule ni Sehemu salama ya yeye kuishi ikumbukwe kuwa hawa ni watoto kila kitu ili wafanye vizuri wanahitaji kushawishiwa.

Tufanye nini?
Jambo la msingi hapa la kufanya ni kuhakikisha serikali inaweka bajeti ya kutosha kwa ajili ya ukarabati wa hizi shule lakini pia kuondoa hii hali ya kuzisahau shule hizi basi iundwe hata tume ambayo itazisemea shule hizi pale zinapopata changamoto kama hizi lakini pia tume ndo itaweka mikakati madhubuti ya ukarabati wa shule hizi.

Lakini hayo yote yanaweza kufanyika ila ikiwa serikali haitaamua kulibeba hili kama janga basi hamna kitu kitafanyika. Serikali kama ambavyo iliamua kuwashirikisha wananchi katika kutatua changamoto za sekondari basi wakiamua kuwashirikisha na kuweka kampeni na kuzisimamia basi hili linaweza kwisha mara moja.

Kwa sasa shule za msingi yaani walimu na wanafunzi wao wana deni kwetu kwani richa ya hizo changamoto zote wanazopitia bado wanajeshi hawa wamepambana na wanaendelea kupambana kufanya vizuri hii inaonyesha ni wazi kuwa ikiwa tutaweka mazingira mazuri ya kundi hili basi wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hapa.

Pongezi
Hongereni walimu wa shule za msingi kwa kazi kubwa mnayoifanya tena mnaifanya katika mazingira magumu mno.

Serikali na wananchi wake tunatambua mchango wenu.

Ahsanteni
Keep it up kijana
 
Back
Top Bottom