Tuzingatie na haya kuinua elimu nchini

Tuzingatie na haya kuinua elimu nchini

WISEJ

Member
Joined
Jan 27, 2014
Posts
5
Reaction score
0
Watanzania tuinue viwango vya elimu kwa kigezo cha ubora pia na si wingi wa wanafunzi wanaojiunga nakuhitimu kiwango fulani cha elimu. Haina maana yoyote kuwa na wahitimu wa kidato cha nne wengi wakiishia kupata sifuri na hii inasababishwa na uchaguzi mbofu wa wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza toka shule za msingi. Ni kweli watanzania viongozi wetu wamejitahidi kusimamia kujengwa kwa shule nyingi sana hapa nchini, lakini tusijali kujaza wanafunzi tu hizi shule bali tuzingatie ubora na uwezo wa wanafunzi wanaokwenda kusoma shule hizi. Tunakubali kuwa majirani zetu kama Kenya kwakiasi fulani wakombele kwa idadi ya wasomi ila watanzania tusishindane nao kwa kujaza wahitimu wenye miziro, bali tuboreshe elimu tupate wasomi wazuri wenye uwezo wakukabiliana na changamoto za ushindani wakiajira nchini na hata nje ya nchi yetu.
Watanzania tuliowengi tunategemea sana shule za serikali kwa sababu yauwezo mdogo wa kifedha kuweza kusomesha shule za binafsi, lakini shule hizi ndizo zenye kila aina ya matatizo, mishahara midogo kwa walimu, vitabu havitoshi, motisha kwa walimu hakuna na mazingira mabovu ya kufundishia na ya kuishi. Serikali ichukue hatua mahususi kupitia kile wasemacho BIG RESULT kwa kutekeleza yote waliojiwekea kama malengo ya hiyo big result pia kuwasikiliza wadau na wataalam muhimu wanaoitaza elimu kwa upana wake. Kuna usemi wa kiswahili usemao ""aisifuye mvua imenyea"" Ebu sasa serikali wasikilizeni walimu matatatizo yao na kuyatekeleza kwani wao ndio tunaamini watendaji wakuu katika masuala ya elimu
 
Back
Top Bottom