TUZO YA MESSI

TUZO YA MESSI

Nihzrath

Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
51
Reaction score
116
TUZO YA MESSI

ZAWADI PEKEE AMBAYO ANASTAHILI MWANADAMU HUYU

NA
NIHZRATH NTANI JNR

Jioni moja, ukiwa umejipumzisha nyumbani. Umri wako sio ulionao sasa, wakati huo. U mzee ,mwenye mvi nyingi kichwani. Unaongea taratibu huku ukiwa na wajukuu zako sebuleni .

Nyote kwa pamoja, macho yenu yameganda yakitazama Televisheni iliyopo sebuleni hapo. Wachambuzi vijana wanaendelea kuwazungumzia wanasoka wa zamani.

Mjadala kuhusu Lionel Messi na Cristiano Ronaldo unashika hatamu. Wote hawa hawakuwahi kuwashuhudia watu hawa. Ni baada ya kuwatazama kupitia "Documentary"zao.Kumbukumbu nyingi za miaka mingi iliyopita angali ukiwa kijana zinarejea mawazoni mwako.

Ghafla!. Unawakumbuka marafiki zako ambao ulikuwa ukibishana nao kuhusu upinzani wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo katika soka hapo zamani.

Wengine wakiwa wametangulia mbele ya haki.Unabaki peke yako huku huzuni na furaha inakuja kwa wakati mmoja. Machozi yanakudondoka bila kutambua.

"Babu mbona unalia?"Mjukuu wako anakuuliza.

Unamtazama kisha
unatabasamu.Tabasamu la uongo mbele yake. Uongo wenye maumivu ndani yake. Wewe ni miongoni mwa kizazi cha dhahabu kilichopata nafasi ya kuwashuhudia wanasoka hao wawili enzi zao.

Unawaza; " kiukweli kizazi chetu kina bahati ya kuwafurahia nyakati nzuri za wachezaji wawili ambao ,hapana ubishi ni wachezaji bora wa nyakati zote. Ni uwendawazimu, kupoteza muda na nguvu kuwafananisha.

Ni watoto pekee bado wangali wakibishana kuhusu utofauti wa ubora wa watu hawa wawili. Tungependa kuwashukuru watu hawa wawili kwa kile walichotuonesha machoni petu. Mwisho wa kumbukumbu yako. Nimewaza!

WAZO LA KUANZISHWA KWA TUZO YA MESSI KATIKA LA LIGA, JE TUTAMPA HESHIMA ANAYOSTAHILI?

Ndio, kitu pekee ambacho tunaweza kumpatia mwanadamu huyu baada ya kustaafu. Ni kuipa jina lake ama kuanzishwa kwa tuzo lenye jina lake. Hapo ndipo tutaweza kuheshimu mchango wake. Namzungumzia Lionel Messi na si Cristiano Ronaldo.

Nimelipokea wazo kwa furaha sana kutoka kwa raisi wa La Liga, Javier Tebas. Tebas anasema; wanafikiria kuanzisha tuzo ya Lionel Messi baada ya kustaafu kwake.

Kwanini tusimpe heshima hii kwa kile alichokifanya katika La Liga? Achana na umahiri na kipaji chake. Yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote katika La Liga. Ametwaa mataji mengi ya La Liga kuliko mchezaji yoyote yule anayecheza La Liga hivi sasa.

Ndiye mfungaji bora wa muda wote wa El Clasico. Kumbuka pia ,ndiye mfungaji bora wa klabu ya Barcelona wa muda wote. Ametwaa tuzo lukuki binafsi.

Yeye ni moja ya sababu ya mashabiki wengi wa soka kuipenda La Liga na kuifuatilia. Amefanya kila kitu kwa ajili ya soka la Hispania.

Nchini Argentina mahala alipozaliwa anachukuliwa kuwa mchezaji asiyefanya kitu chochote katika soka la nchi yake lakini hali ni tofauti nchini Hispania. Yupo Lionel Messi mmoja tu Duniani. Ni nani awezaye fananishwa na mtu huyu? Jibu ni moja tu, ni Lionel Messi mwenyewe.

Ni makosa kumuandika kuhusu yeye, ebu muelezee yeye baada ya kumtazama. Kuna sababu nyingi kwanini Messi ni tofauti na wengine. Mguu wake wa kushoto unaufanya mchezo wa soka uonekane ni mchezo rahisi mno kuucheza.

Wako watu watahoji! Kwanini isiwepo tuzo lenye jina la Ronaldo pia? Jibu ni moja tu. Aliyoyafanya Lionel Messi kunako La Liga, hakuna mwanadamu mwingine aliyewahi kufanya. Hivyo anastahili.

Nchini Hispania kumekuwa na utaratibu huo. Ipo tuzo ya Telmo Zarra ambayo anapewa mfungaji bora raia wa hispania. Ipo tuzo ya Zamora. Hii ni kwa ajili ya kipa bora. Tuzo ya mfungaji bora wa La Liga imepewa jina la "Pichichi" kwa heshima ya. Rafael "Pichichi" Moreno.

Hapana shaka kuwa ,tuzo yenye jina la Lionel Messi inaweza kuanzishwa ndani ya La Liga. Bahati mbaya FIFA hawataweza kumpa Messi heshima hii.

Tuzo ya Farenc Puskas inabakia tuzo pekee yenye jina la mchezaji kwa shirikisho hilo la soka Duniani. Puskas alikuwa na maajabu mengi ngazi ya klabu na timu ya Taifa lake.

Tuendelee kumshuhudia kiumbe huyu aitwaye Lionel Messi ila kumbuka, barua ya marehemu haifurahishi kamwe.
Daima huacha kumbukumbu zenye kutuumiza tunaobakia.

Je umewahi kuamini yanayotufurahisha leo, ndio yatakayotuumiza kesho? Basi, tunafurahia uwepo wa Lionel Messi leo ila tutahuzunika siku akitangaza kustaafu soka na kuondoka machoni mwetu. Ni ngumu kukubali siku hiyo ikifika.
 
Europe's top five leagues in 2018-19:

Most goals - Messi
Most assists - Messi
Most dribbles - Messi
Most chances created - Messi
Most free-kicks scored - Messi
Most key passes per 90 mins - Messi
Most goals from outside the box - Messi

He missed three weeks due to injury.
 
Back
Top Bottom