Tuzo ya Samatta yafutwa

Tuzo ya Samatta yafutwa

Joram Dymisster

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2014
Posts
502
Reaction score
429
upload_2017-12-27_8-6-30.jpeg


Kama unaikumbuka tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa Afrika ambayo Mbwana Samatta alishinda usiku wa January 7, 2017 haitakuwepo kwa mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kutolewa mwaka 1992.

Sababu ya msingi ambayo imetolewa na shirikisho la soka barani Afrika ni kwamba, waliopewa jukumu la kuchagua mchezaji bora wa kipengele hicho wote wamekosa sifa na walichaguliwa kimakosa kuwepo katika jopo hilo.

Kwa mujibu wa CAF tuzo hiyo huenda ikarudi endapo watapatikana watu sahihi watakaounda jopo ambalo kazi yake ni kuteua majina ambayo yatawania tuzo hiyo.

Kwa maana hiyo, kwa sasa wachezaji wa ndani watapambanishwa na wachezaji wanaocheza nje ya Afrika kuwania tuzo ya mchezaji bora hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Chanzo; Priority10News
 
Africa tuko disorganized sana, ndo maana watawala wanataka kufia madarakani
 
Kwa maana hiyo Mbwana Samatta anaendelea kuwa mshindi wa tuzo hiyo hadi watakapo amua vinginevyo.(This is Africa!)
Mkuu baada ya samata kuna mwingine ameshashinda hii tuzo
 
Back
Top Bottom