BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Profesa Penina Mlama Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu anazungumza
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ujenzi wa taifa ni kujenga tabia za Wananchi, mitazamo ya kuweza kuishi pamoja.
“Kila taifa lina mitazamo yake ili watu waweze kuishi pamoja.
“Ujenzi wa Taifa unahitaji kujenga mitazamo na tabia inayowezesha kuishi pamoja katika urafiki na mshikamano, kila Taifa lina hali hiyo anayoizungumzia baba wa Taifa.
“Mitazamo na nyenzo za kujenga tabia niyozungumzia hapa ni tabia nzuri na mbaya, haki.
“Maandishi bunifu ni moja ya nyenzo muhimu kwa Taifa lolote, kwa kuwa maandishi hayo yanabeba msingi wa jamii husika.
“Jamii iliyostaarabika huwa inasisitiza usomaji wa maandishi kwa kutambua ni nyenzo muhimu.
“Umuhimu wa maandishi bunifu umesaidia jamii kukuza hifadhi na kusaidia waandishi bunifu.
“Umuhimu wa maandishi bunifu umepelekea uwepo wa tuzo za kimataifa mbalimbali, lakini pia kuna tuzo za kitaifa.
“Tanzania haijabaki nyuma nasi tuna waandishi wetu kadhaa, mfano ni Shaban Robert na wengineo
“Umuhimu wa uandishi bunifu umesaidia kujenga mitazamo tofauti na kukuza amani, kwa kusoma maandishi bunifu hata watoto wamefanikiwa kufahamu historia ya nchi hii.
“Baadhi ni mapambano dhidi ya ukoloni, harakati za siasa za ujamaa, changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo, pia imesaidia kukuza Lugha ya Kiswahili.
“Hivyo, tuzo hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, “
Jina la Tuzo
Anasema: “Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, jina hili limetokana na kumuenzi Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mwandishi na kiongozi.
“Malengo yake ni kuwatambua kitaifa na kuwazawadia waandishi katika nyanja za riwaya na ushairi, kukuza Lugha ya Kiswahili, kukuza vipaji vya uandishi, kukuza utamaduni wa kujisomea, kuhifadhi historia, kukuza sekta ya uchapishaji na kuongeza hifadhi ya vitabu.
“Mwaka wa kwanza tuzo itatolewa katika riwaya na ushairi, tuzo zijazo zitajumuisha na nyongeza ya hadithi za watoto, tamthilia, hadithi fupi na tafsiri.”
Vigezo
Profesa anaeleza: “Mshiriki lazima awe Mtanzania, kutumia Lugha ya Kiswahili, mshiriki awasilishe kazi yake katika nyanja moja tu.
“Riwaya iwe na urefu wa maneno 60,000 hadi 100,000, mkusanyiko wa mashairi usipungue kurasa 60,000.
“Pia mshiriki anaruhusiwa kushiriki mara moja tu, andiko liwe makini na muhimu ya kidunia.
“Kuwasilisha, dirisha linaanza kuwa wazi kuanzia Septemba 13, 2022 hadi Novemba 30, 2022, na itapokelewa kupitia barua pepe.”
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba
Profesa Penina Mlama Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu
Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa
Wahudhuriaji
Waziri wa Elimu Prof. Mkenda
Shafi Adam Shafi aliyeadika kitabu cha Vuta nikuvute
Waziri wa Elimu Prof. Mkenda akizindua Shindano