Tuzo za TFF ni za mchongo

Mukuu123

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2019
Posts
319
Reaction score
1,223
Unajua team bora ndio hutoa kikosi bora. Team ya Simba haijashinda kikombe chochote hata kikombe cha kahawa msimu huu halafu eti ndio team iliyoingiza wachezaji wengi kwenye kikosi bora, hii kabisa haingii akilini hata kidogo.

Ni tuzo zilizokosa credibility kabisa, unawezaje kutomuweka mtu kama Aucho pale kwenye kile kikosi ambaye amekuwa mhimili mkubwa sana pale Yanga? Kama siyo kujuana ni nini?

Hzi tuzo kuna mtu mmoja alikaa home kwake, akatoa maelekezo, maana zinakosa uhalisia.
 
TFF maskini ya Mungu. Kila upande unalalamika. Si Utopolo si kwetu Simba.

Naomba nikujibu hoja yako. Ainisha ni mchezaji gani wa Simba ambaye unadhani hakustahili kuwepo.

Kisha ainisha ni nani alistahili awepo kwa maoni yako. Alafu tuweke mezani takwimu za kila mmoja.

Simba kakosa ubingwa. Ila timu yake ndiyo imeonesha uhai katika maeneo mengi. Imefunga magoli mengi na kuruhusu machache sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…