Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Na Elius Ndabila
ewndabila@yahoo.com
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na hoja ambayo imeshikiwa bango na baadhi ya Watanzania wakiomba Mh RAIS Dkt John Magufuli aongezewe muda wa kuliongoza taifa hili. Hoja hii mwanzo ilianza kama utani na Mh Juma Nkamia Mbunge wa Chemba. Ninaweza kusema huyu ndiye mwasisi wa hili. Hoja hii imeendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali wakitoa mapendekezo yao. Ukisikiliza na kutafakari Juu ya hoja wadau hawa wanaotaka Mh Rais kuongezewa muda utaona ni za msingi na zinazoingia akilini. Hoja yao kubwa wanadai kwa muda mfupi serikali ya JPM imefanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya maendeleo na Tanzania kuingia kwenye rekodi ya nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.
Kwa mantiki hii wanaamini Mh Rais akiongezewa muda anaweza kuifanya Tanzania kuwa Dubai. Wanadai muda wa miaka mitano ya mwanzo na mitano ya pili kama ilivyo desturi ya CCM haitamfanya Rais kumaliza matatizo yote bali akiongezewa muda anaweza kumaliza na kuwaachia Watanzania nchi ikiwa kwenye maendeleo makubwa. Wanainga kuongezwa muda bado hawajaja na hoja za kushawishi kuwa ni kwa nini hawataki aongezewe, bali wengi wamejikita kwenye hoja dhaifu ya kuwa ni udikiteta. Lakini ukisoma misingi ya udikiteta kuongezewa muda wa kuwa madarakani si udikiteta bali kujiongezea muda ndio udikiteta. JPM angesema anataka kujiongezea muda hapo tungesema ni udikiteta lakini kama wanaosema ni watu huku yeye akisema Urais ni kazi ngumu basi hapa tunaikuta misingi ya demokrasia na siyo udikiteta.
Baada ya kupima hoja za wanaotaka Rais kuongezewa muda binafsi nanaona ni za msingi hasa ukizingatia hoja yao iliyojikita kwenye mkutadha wa maendeleo. Hili halipingiki kuwa Mh Rais anafanya kazi kubwa ambayo hata siku akiondoka mate do na Kazi Zane zinaelezeka. Lakini pamoja na kuungana wanaotaka kuongezewa muda mimi ninatofautiana nao katika approach na maudhui ya kuongezewa muda. Si pingani nao kwa maana kuwa hoja zao ni dhaifu, rahasha! Ninapingana nao kwa kuwa hoja zao hazitutafutii majibu ya kufukuza bali wanatupatia hoja zenye majawabu ya muda mfupi. Kunatofauti kubwa kati ya majawabu na majibu, lakini leo si muda wake wa kutofautisha haya. Ila ninaomba ukisoma makala hii hadi mwisho utapata hii tofauti na nitaruhusu kunikosoa kwani haya ni mawazo yangu ambayo unaweza kuyapinga kwa kuyakosoa au kuyasahihisha.
Binafsi ninadhani muda huu tungekuwa tunazungumza zaidi Juu ya instrument na siyo personality. Hii ni kwa kuwa personality haidumu lakini instrument inadamu sana, personality ni utashi ambao inategemea nafsi. Lakini instrument inategemea taasisi na vyombo vingine. Ninajua Ayla hii inakuwa ngumu kuelewa hasa kwenye instrument na personality. Ninatamani aya zinazofuata utaelewa lakini kwa ufupi wanaotamani Rais kuongezewa muda wanatazama personality na si kwa mawanda mapana ya kuijenga taasisi.
Wakati hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiliongoza Taifa hili binafsi sikuwepo, lakini vita us mbalimbali tunavyosoma vya history vinanipa nguvu ya kumtoa bus Nyerere, kutambua misimamo yake na kujua mafanikio makubwa ya kipindi cha uongozi wake. Hivyo hii tu inanipa ushujaa wa kumuelezea Nyerere na kumzungumzia jemedari wa Tanzania wa Sasa Mh Magufuli. Ukisikiliza hotuba nyingi za Mh Rais utasikia akisema mambo mengi anayofanya ilikuwa ndoto ya Baba wa Taifa lakini hayakufanyika na mengine aliyofanya Baba wa Taifa yaliharibiwa kwa kuwa yalikosa eidha usimamizi au maamzi ambayo hayakuzingatia matakwa ya nchi. Kwa mfano ndege zinazonunuliwa kwa aridhi ya Tanzania si ngeni, kipindi cha Nyerere zilikuwepo ila ziling'atuka baada ya Mwalimu kustaafu. Nyerere alisimamia sana swala la maadili ndiyo maana hadi akafikia kuanzisha azimio la Arusha ambalo msingi wake mkubwa ilikuwa ni Binadamu wote ni sawa. Hata sasa kipindi cha JPM maadili ni kipao mbele namba moja. Haya na mengine mengi aliyofanya Nyerere na ambayo sasa anafanya JPM ndiyo yanawafanya Watanzania kumuomba JPM aongezewe muda ili kuendelea kulinyosha Taifa.
Maswali ya kujiuliza ni mengi, mojawapo ni kuwa Je akiongezewa muda atamaliza matatizo yote? Je, tunajua Kama maisha yetu mwenye haki nayo ni Mungu? Ikitokea Mungu ukafika wakati wa kumchukua kiumbe wake nani atayafanya haya? Binafsi ninaamini kuwa mtu kama anafanya vizuri kukaa muda mrefu madarakani ni jambo jema kwani anasaidia kuongeza chachu ya maendeleo. Hili sina shaka nalo kwani tunaona China wao huku walishapita. Lakini ninakuwa na mashaka tunapotanguliza personality badara ya instrument. Tumeona huko nyuma ndoto na kazi nyingi za Nyerere zilizima baada ya Nyerere kuondoka madarakani. Je haya mazuri anayofanya JPM hata akiongezewa miaka 50, baada ya yeye atayefuata atayasimamia? Hatauza ndege zetu? Hatabinafsisha meli zetu na mali zetu zingine tukarudi tena Misiri badara ya Kanani?
Maoni yangu ni kuwa huu ambapo yupo mzalendo huyu mwenye ndoto na matamanio makubwa ya Taifa hili basi tuanze kuliomba Bunge kutunga sheria ili haya anayofanya JPM mtu msingi be akina akayasimamie. Tuandae sera ya nchi ambayo kila Rais akija atakuwa anaitekeleza badara ya kutekeleza ya kwake. Leo hii nchi ingekuwa na sheria na sera ya kinchi basi yale yote ambayo Nyerere alikuwa akitekeleza waliofuata wangeyaendeleza, lakini kwa kuwa katiba yetu haitoi mwongozo ndiyo maana sasa JPM anahangaika kuirudisha nchi Kanani. Leo hii hata tukisema JPM aongoze hadi akichoka, lakini hatujui baada ya yeye nani atakuja? Wenzetu nchi zilizoendelea kiongozi unakuwa na mambo machache ya kwako, lakini mengine yote unasimamia sera ya nchi. Ninadhani sasa ni muda wa Juma Nkamia kuanda mswada binafsi wa kufanya mabadiriko kwenye katiba yetu ili haya anayofanya JPM siku akiondoka yasipotee.
Mwisho nihitimishe kwa kusema tuliombe Bunge litengenezee sheria ambazo zitasaidia kuja na sera ya nchi. Sheria zitasaidia kwa kuwa hata mkipata Rais yeyote na wa chama chochote hatafanya kazi Nje na misingi ya kisheria inayomuongoza. Lakini tukisema hoja ya kuongezea miaka ya kuongoza ndiyo tuishikie kidedea, siku akitoweka huyu hatutakuwa na sauti tena. Ni vema tukaanza na sheria ili hata Kama hatakuwepo lakini yale tunayoyategemea kutoka kwake tukaendelee kuyapata kwa wengine.