Tuzungumzie alichofanya Ramos kwa Salah

Ramos alifanya makusudi kinachoshangaza mwamuzi alikuwa karibu lakini hakujali.Ile ni tabia ya Ramos,ana mambo ya kihuni ,alifanya hivyo baada ya kuona hali ni mbaya kwao.
Ndio zinaitwa mbinu za kushinda mechi kwa vyovtote vile. Maana mechi ni moja na haina marudio.
Kwann mwamuzi hakutoa kadi , sababu ramos aliugusa mpira kwanza... kama asingeusa ile ilikuwa yellow.
 
Hawajajifunza toka kwa tim nyingine ambazo baada ya main player wao kuondoka zimeyumba.
Baada ya salah kutoka, liverpool wamerud nyuma. Wamekosa confidence, so unaona timu nzima ilikuwa haina option B , iwapo salah ataumia
Kwa madrid key player ni Ronaldo ila anapokua hafanyi vizuri haimaanishi Madrid haifanyi vizuri option zinakua ni nyingi sana so kwa game ya jana Liverpool lawama zote ni kwa kocha wao hakua na plan B wachezaji wake aliwajengea imani kwamba everything is Salah alivotoka ndio basi game kwa upande wao ikawa imekwama.
 
Thats right. Alijiamini kupita kiasi. Wazungu wanasema overconfidence makes you careless.
Angejipanga vizur na kuwa na plan B. Ila ndio hivyo hakuwa nayo..
 
Ramos ile kitu amefanya makusudi. Amemshikilia ule mkono na walipoanguka akajiangusha kwenye bega la Salah.

Ramos kama defender kafanya kazi yake, ila LFC players kama wachezaji hawakuonesha kuumizwa na kuvunjwa bega mchezaji wao. Ingekuwa enzi zile, Ramos angemjua Roy Keane ni Mtu au Jini. Zisingepita dakika 5 Ramos angevunnjwa kiongo chochote tu. Thats the only way to deal with such players.
 
Kwa akili hizo kwamba tulio comment hatujui mpira, basi huko tunakoenda utatuambia Ramos aliyecheza ile mbinu siyo mchezaji.
nakujibu hoja sio ushabiki...
eti unaiita "mbinu"...kwaio kumbe kwenye mpira wa miguu wanaposema fair play hua mnaelewa nini ?

sasa nakujibu kama mpenzi wa mpira wa miguu
ramos ni mchezaji wa mpira wa miguu, na nafasi yake ni beki. kitendo alichofanya ni cha kihuni na unfair play. nimemaliza.
 
Ule haukuwa mchezo wa mpira bali ilikuwa ni mieleka mibaya sana hata kule WWE akina Cena wala huwa hawavunjani mifupa kama alivyofanya jamaa!
 
Kwani refa hakuwepo? Mpira wa miguu kama mchezaji akifanya kosa huadhibiwa kwa kupewa kadi ama ya njano au nyekundu. Sasa thibitisha kosa alilofanya mtaalam Ramos (japo mie simpendi kwa kutufunga dakika za mwishoni kwenye El Classico). Hata mtuhumiwa huthibitishwa mkosaji na hakimu tu.
 
Ni ugeni wa ligi khbwa na presha ya mechi ilisababisha. Mane angeangalia ile gemu ya mwisho ya barca na madrid akamuiga messi kumlisha mitama ya kiufundi ramos bila refa kushtukia
hahaha kabisa, na angeweza kufanya vizuri zaidi....Mane anajua kwakweli.
 
Kwa hiyo Ramos siyo mchezaji na hajui mpira!
 
Salah ndo alianza kucheza Rafu, hapa wa kulaumiwa ni Salah
 
Ramos ana history mbaya ya kupigwa red na hata jana juna sehemu alimpiga na kiwiko kipa wa Liv refa hakuona japo kipa alikuwa anamwambia refa jamaa kanipiga kwenye kidevu.
 
Mashabiki wa Liverfools mmelizwa tu pigeni kimya ile ni kawaida kwenye mchezo kifupi fainali ilikuwa rahisi sana kwa Madrid mmekoswa sana umiliki wa mpira mlizidiwa hamkuwa na option nyingine zaidi ya kusubiri kukandamizwa tu na kipa alishapanic unategemea nini toka mlivyoshinda kwa Roma kibahati nikajua mnaenda tu kupakatwa ile fainali ilikuwa ya As Roma na Madrid
 
Inaitwa clavicle fracture. Upone upesi na uendelee na majukumu yako.
 
kwa Ramos sijaona kipya pale... ile michezo ni kawaida yake, sema tu kiungwana amewakwaza watu wengi waliokuwa na Matarajio makubwa kwa Mo salah.

nimejaribu kukumbuka rafu za Sergio ramos hii naona bahati mbaya zaidi imeenda kwa Mo salah maana hakumkamia kiviile
 
Dammm.. world cup ndio basi tena. Dah. Apone haraka jmn
 
Umeandika mengi ila ni ujinga tu..faulo ngapi waamuzi huziacha na kuzua lawama!?,..kabla salah hajatoka hali ya mchezo ilikuaje?!..salah mfupi anaanzaje kuingiza mkono ndani ya mkono wa ramos!!?..alianza marcelo kucheza rafu kwa sala mara mbili..hazikwenda kama alibotarajia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…