Kama kuna jambo lililoumiza wapenzi wa mpira wasio washabiki wa mpira, ni kitendo cha Ramos kufanya niseme dirty game au faulo mbaya ambayo alimfanyia Mo Salah
Binafsi pia nilijiskia vibaya, ila sasa tuzungumzie kwamba wengine wanasema bahati mbaya, wengine wanasema alidhamiria na wengine wanasema ilikua ni game plan baada ya kuona wanashambuliwa kwa dakika nyingi za mwanzoni kabla ya yeye kuumizwa na kutoka.
Sasa kwa taarifa zilizopo ni kwamba ameumia sana kwenye mifupa ya bega na huenda akakosa michuano ya kombe la dunia,
Tukiacha ushabiki, hivi ile haikua makusudi kweli? Kwanini aliung'ang'ania mkono hadi kwenda chini. ?
Huko kwenye akaunti yake ya instagram anatukanwa sana ila jamaa anachekelea tu, nafikiri angetumia fursa hii kutoa neno la kuomba radhi, ila wanasema hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo kwa wachezaji hasa katika mechi za fainali.