Tuzungumzie alichofanya Ramos kwa Salah

Mkuu Sisi mashabiki tunaendaga uwanjani kuangalia burudani. Hatuendi kuangalia mieleka pale.
Beki ukipitwa na forward tunasubiri tuone uhodari wa kipa langoni.
Sasa we ukipitwa unapiga mieleka.

Ile sio football hata kdg.
Am telling you that.
Mechi mhimu kama ile sio ya kumlalamikia ramos hata kidogo mkuu.
 
Mechi mhimu kama ile sio ya kumlalamikia ramos hata kidogo mkuu.
Hamna anayemlalamikia Ramos. Hapa tunaongeaga ukweli Tu.
Mechi ya Jana watu wameenda kuangalia burudani itakayotolewa na wachezaji wote 22 Kwa kila upande.
Sasa we kumuumiza mchezaji mwingine Kwa makusudi unategemea nini.

Ndio mana unaona watu wanampa lawama hasa yeye Kwa kuwa mechi ya Jana ilikuwa ina uzito wake zaidi.

Mbona akimchezeaga rafu Messi huwa inapotezewa Tu kawaida.

Kumkosa Mo Jana kuna kitu kilipungua.
Yule ni mchezaji wa muhimu Sana.

Tuache ushabiki wa kimaandazi.
Elewa alichokifanya Ramos sio cha kiungwana.
Umeona Nani ameunga mkono Kwa aliyoyafanya.
 
Umemeza debe la Omo,ninachojua hata Madrid wenyewe hawajafurahia huu ubingwa,una doa.
 
Yaani Salah kageuzwa kisingizio cha kushindwa Liverpool ha haa haaaa, maana kila "mpinzani" wa Madrid ukimgusa tu, Salah, sijui Ramos mhuni, blah blah kibao. Ila inasaidia kupunguza maumivu. Poleni sana wote ambao hamkutaka Madrid ashinde. Hongereni Madrista wote.
 
Umemeza debe la Omo,ninachojua hata Madrid wenyewe hawajafurahia huu ubingwa,una doa.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€...watu Madrid City huko wanakula pilau la ushindi wewe unajipa tumaini hapa. Mm mmoja wao nafurahia sana na hakuna doa. Ramos, super captain "mutu mbaya" imetumwa kazi naimeifanya kazi.
 
Umemeza debe la Omo,ninachojua hata Madrid wenyewe hawajafurahia huu ubingwa,una doa.
Endelea kujipa moyo, ndoo ya 13 na imewekwa kwenye historia. Mo Salah ni nani kwa Madrid wasifurahie ubingwa wa jasho lao?? Aliumizwa CR7 europe cup na maisha yakaendelea, alipewa kadi nyekundu BECKHAM wa Uingereza kombe la dunia na maisha yakaendelea sembuse Mo Salah huyu ambaye bado hajashinda hata kombe moja??

Povu anatoa aliyeumizwa na kipigo cha jana sio mimi, mimi nimefurahishwa na Liver kuukalia.

Angalia hii kitu hapa kisha uendelee kujipa moyo kuwa Madrid hawajasherehekea.

Endelea kujipa moyo!


Hii video clip ya chini NAWAKUMBUSHA MACHUNGU YA JANA, tutasiriba chumvi kwenye hivyo kidonda mpaka kipone sasa.
 
KWa aliyewahi kucheza mpira hawezi kushangaa lile tukio hata kidogo. Kazi ya beki ni kufanya kila awezalo kupunguza nguvu ya washindani wao. Na kazi ya foward ni kufanya kila awezalo kupata bao, iwe kwa kujirusha au hata kusababisha kupigwa. Lengo ni BAO.
Kutengeneza frastration ni moja ya burudani pia. Unakumbuka yule wa simba alitemewa mate? Unajua kwa nini? Inawezekana alimpima oil mshikaji kimtindo, refa hakuona. Kwa hasira akampa kohozi la uso. Akala nyekundu, simba wakapeta.
Unakumbuka Zizou alivyofanywa na Materaz kwenye ile fainali kati ya ufaransa na Italy? Alitukanwa, akaghadhika akampa jamaa ''ndoo'', akala red. Italy wakachukua ubingwa huku france wakiwa pungufu. Hiyo ndio fabo mzee, ni kawaida sana ile.
 
Mkuu tuyaache hayo weather jamaa hakufanya fair au laa.

Ubingwa nani kachukua?
 
Wewe ni shabiki mkuu, mpira unaujua kwa kuangalia kwenye Tv.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€...watu Madrid City huko wanakula pilau la ushindi wewe unajipa tumaini hapa. Mm mmoja wao nafurahia sana na hakuna doa. Ramos, super captain "mutu mbaya" imetumwa kazi naimeifanya kazi.
Wakipenda wamuite Sergio Ramos JAMBAZI. Jamaa ni super captain.
 
Kudadadeq, Ramos unalaaniwe popote uliko, Huwezi kumfanyia Mwafrika mwenzetu kitu kama hii... AlaH...!!
 
Ronaldo akiwa na off day mchezoni kuna mashine zingine zafanya kazi.
Hapa sioni haja ya kumlaumu Karius kwa kushindwa zuia michomo ya Bale, jamaa ni kama HULK.
 
mkuu humu kuna ushabiki maandazi bora tujikalie kimya tunaambiwa hatujui mpira wao ndo wanajua mpira na sheria 17 za soka.
tena lait angefanya jambo ambalo lingepelekea mchezaji kupoteza maisha basi zingeandikwa rip nyingi sana na wao wangeandika kwamba walimpenda sana ila bado wangesifia ujembe wa aliyefanya
hawababaishi hawa ndugu kwenye maeneo ya kujidai kama samaki samaki na vibanda umiza hua tunakaa nao sana tunawajua mashabik maandazi tena utamjua kwa kua mropokaji ovyo tu muda wote na anachoongea hakina mantiki, wenye kuujua mpira unakuta tumetulia na wine zetu barrridi tunawaangalia tu na kucheka.
 
Ulipotoa maelezo ulikua unatakaje!?
yani nauliza ulitaka niandike nini maana nilichoandika mimi wewe umesema nimeandika pumba sijui ujinga ndo nakuuliza ulitakaje sasa??

ngoja nikuambie kitu mkuu, mpira ni kama vile vitabu tunavyosoma darasani kama Ngoswe, Takadini, Three Suitors One Husband, Pass Like A Shadow and all stuffs like that na siku ya mtihani kila mtu atakuwa na jibu lake tho kitabu mlisoma pamoja.

same to mpira wote tumeangalia kwa pamoja tukio tumeangalia kwa pamoja mimi nimeona nilichopresent hapa wewe pia umeona ulichoona tho hujakiwakilisha.

ubaya zaidi unataka kunilazimisha kile unachoamini wewe na mimi niamini hicho hicho na hapo ndio unapokosea.

NARUDIA TENA FOOTBALL IT'S ALL ABOUT PHYSICAL CONTACT

uje na hoja usije kama mlevi unakosoa bila kuja na hoja....hoja upingwa kwa hoja.

Get Well Soon Salah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…