TV inaonesha battery charge 100%

Wakuu,nimenunua tv ya kichina mpya,iko vzuri tu.
Ila cha ajabu kwenye kona juu kulia,inaonyesha alama ya battery na 100%,cjui inamaanisha nini?View attachment 2916669
Angalia isije ikawa zile za Solar. Jaribu kudisconect umeme! Kisha iwashe....ikiwaka itakuwa na Backup battery ndani yake. Maana zipo TV zina backup Battery ndani yake
 
Siyo hiyo chanel labda au kifaa unchotumia kupata hiyo video decoda etc? Kma ni TV Nadhani hizi TV wanaweka OS ya Android so kuna kitu wamechemsha hapo imeanza kuonyesha hivo, chunguza settings, kama ina uwezo wa kufanya update fanya hivyo au fanya factory reset.
 
Wakuu, nimenunua TV ya kichina mpya, iko vizuri tu.

Ila cha ajabu kwenye kona juu kulia, inaonyesha alama ya battery na 100%, sijui inamaanisha nini?

Assumption:
Watakuwa ni Azam wenyewe, inategemea na hiyo content wanayoionesha ina play toka katika kifaa gani...

Most likely kifaa wanachotumia kina battery kama backup system, na alama imekuja baada ya main power kukatika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…