TV1 Kurusha Live ligi kuu ya Uingereza(EPL)

TV1 Kurusha Live ligi kuu ya Uingereza(EPL)

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
KITUO cha Televisheni cha TV1 Tanzania kinatarajia kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu.

Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.

TV1 Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi husika.

Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania Joseph Sayi alisema hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja, Mkuu wa kitengo cha masoko wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania ligi kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.

Baadhi ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.

Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey alisema watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji nyota na makocha mahiri kama Antonio Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na makocha hasimu Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

Tv1 Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo kilianza kurusha matangazo yake rasmi Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia ving’amuzi vya Startimes namba 103,Azam 119 na Ting 36.


Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino


Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.
Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
 
Isije ikawa kama zile zakuchaguliwa mechi na kuishia kuonyesha mechi zenye mvuto mdogo. MU na Ars,au MU na Chelsea au Man city unakuta hawazionyeshi
 
Inamaana hiyo Tv 1 haijitegemei kwa Ving'amuzi?

Kama Chanel hiyo itakuwa ndani ya Startimes na Azam basi sitaona tofauti kati yake na Dstv. Maana hapa huyo Tv 1 aweke chake na Azam/Startimes aweke chake, we mlala hoi utauziwa bei gani hicho kifurushi?

Aaah hata hivyo ngoja tusubiri.

BACK TANGANYIKA
 
Dstv ndio wana haki hiyo, wao si wale wa match moja ya jmosi, kwanza wanachannel moja tu, sidhani kama ni match zote
 
Safi, hiki kituo wanajielewa sana na wako professional nawaaminia haitakuwa kama tbc wakati ule mechi za kupangiwa
 
Inamaana hiyo Tv 1 haijitegemei kwa Ving'amuzi?

Kama Chanel hiyo itakuwa ndani ya Startimes na Azam basi sitaona tofauti kati yake na Dstv. Maana hapa huyo Tv 1 aweke chake na Azam/Startimes aweke chake, we mlala hoi utauziwa bei gani hicho kifurushi?

Aaah hata hivyo ngoja tusubiri.

BACK TANGANYIKA

hata akiweka 20000 bora kuliko makaburu aisee
 
Dstv ndio wana haki hiyo, wao si wale wa match moja ya jmosi, kwanza wanachannel moja tu, sidhani kama ni match zote
Mkuu Tv1 haiko Tanzania tu kumbuka, ndo maana inaitwa Tv1 Tanzania
 
Wengi wanafikiri kuwa sasa TV1 inaenda kurusha mechi zote za epl kama supersports.Haki ya matangazo yakulipia kwa ukanda wa jangwa la sahara bado dstv wana exclusive right.Njia hii ya kununua ili kuuza ndiyo pekee inampa muuzaji haki yakurusha mechi zote kwa wateja wake kupitia chaneli atakazozichagua.Hapa sasa ndo unaona dstv wanarusha kupitia supresports channels.

Njia nyingine ni kununua mechi moja ya jumamosi itakayochezwa kati ya saa nane mchana mpaka saa kumi za uingereza.Mnunuaji wa haki hii yeye analazimika kutouza hizo mechi,anatakiwa kuzirusha kupitia free to air channels(FTA) ambazo atakuwa ameingia nazo makubaliano ya kibiashara.Hapa sasa unawakuta ECOMAT wa Zimbabwe ambao wamepewa haki hizo mpaka msimu wa 2018/19.Wao watarusha hiyo mechi moja ndani ya muda huo tajwa siku ya jumamosi kupitia hizo TVs.Moja ya hizo TV ni TV1 ambao wamekubaliana na ecomat kurusha mechi moja siku ya jumamosi kwa hapa Tanzania na popote inapofika TV1 ndani ya kusini mwa jangwa la sahara.

Kwahiyo sio kama watu wengi walivyoelewa.Ukiangalia ratiba ya epl mechi nyingi kali hazichezwi jumamosi.Na hata zile kali chache zilizopangwa jumamosi hazichezwi muda huo ulioruhusiwa kwa tv za FTA.Hii inafanywa makusudi ili kuto wakosesha wateja watu wa pay TV kama dstv ambao wanalipa pesa nyingi kununua hizo haki.

Kwa hiyo umuhimu wa dstv kwa hapa bongo bado hauwezi kupunguzwa hata kidogo na hili suala la TV1.Kuna jumamosi zitakuwa hazina mechi hata moja kwa watu wa FTA kwakuwa tu mechi siku hiyo zinaanza late,zaidi ya ule uliokuwa stated kwenye mkataba wao na epl board.

Kwa makadirio ya mechi moja kila wiki tv1 wangerusha mechi 33 tu kwa msimu mmoja.Lakini kwa sababu ya limitation ya muda ni dhahiri zitakuwa chini ya 33.Sasa unawezaje kuibana dstv mwenye mechi 330 kwa season za epl huku wewe unapewa mechi chini ya asilimia 10 tena za kuchaguliwa kimkakati?
 
Back
Top Bottom