Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Miongoni mwa vijana wachache majasiri, ambao Tanzania imebahatika kuwa nao, ni huyu Mwaipaya, Huyu alimpiga Spana Jiwe hadi Jiwe akamtumia Watekaji, Jiwe alikuwa muoga sana! Kijana mdogo kama huyu unamtumia Watekaji badala ya kujibu hoja! Noma kweli yaani!
Hapa akifundisha siasa Keifo FM
Sasa Mwaipaya kaingia kwao Kyela, kuwaamsha ndugu zake, unaambiwa mikutano yake inajaa watu Mbowe anasubiri, kijana ana ushawishi ule wa Alphonce Mawazo
Hakika siasa ni Karama, wala huhitaji msafara wa Magari 300 huku kila gari likiwa na watu 10 ili kujaza uwanja (kwa sauti ya Mama Maria Nyerere), Ushawishi ndio silaha pekee .
=====
Bwana Mwaipaya amepokea kero za Wana Kyela, ambako wengi wanalalamikia kudhulumiwa kwa fidia ya Bomoa bomoa ya ujenzi wa barabara ya Ibanda- Kajunjumele, inadaiwa bil 1.4 iliyotengwa kwa ajili ya fidia imetafunwa ( Hata hivyo ujenzi wa barabara hiyo umeyeyuka mithili ya barafu wakati wa kiangazi, hela ya mradi huo imetajwa kupelekwa kwenye fungu la kampeni za ccm 2025), Hata hivyo Wananchi wamestuka!
Kingine ambacho wananchi wamemlalamikia Mwaipaya ni Mkandarasi wa barabara hiyo kuharibu miundo mbinu ya maji, kwa sasa Kyela hakuna maji ya bomba kutokana na jambo hilo na hakuna anayejali, idara ya maji wala mbunge wamenyamaza.
Kutengwa kwa baadhi ya maeneo ya mjini kyela kwenye ukarabati wa barabara za mitaa kwa sababu za Ukabila ni kilio kingine cha wananchi, Kwa mfano kijiji cha Bondeni kimenyimwa barabara za mitaa kwa sababu ni kijiji ambacho wengi wanaokaa huko ni BHAJANGA (yaani watu wa kuja ambao siyo wanyakyusa, Wangoni na wayao)
Lami zimeishia CRDB na kipande kimefika hadi Uwanja wa Mwakangale tu huko kwa bhajanga hakutakiwi kutiwa lami, Hata Mahakama ya Mwanzo iliyokuwa kwenye kijiji hicho imebomolewa kwa sababu ya kinachoitwa Ujenzi wa Barabara, pamoja na kuwa na eneo kubwa lililobaki lakini haitajengwa hapo kwa sababu hizo hizo.
Mwaipaya amepokea vilio hivyo na ameahidi kufikisha kwenye Kamati kuu ya Chama chake.