Twambie Changamoto ya kiafya na Tiba yake ambavyo kisayansi ni kama havimake sense ila kiuhalisia vipo

Twambie Changamoto ya kiafya na Tiba yake ambavyo kisayansi ni kama havimake sense ila kiuhalisia vipo

Engager

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
1,522
Reaction score
3,255
Kizazi cha wazee wetu wenye kujua tiba mbadala kwa matatizo ya kiafya yasiyo elezeka kisayansi, kinazidi kuisha. Tunabaki sisi akina .com

Hivyo basi, kama uliwahi kudokezwa, kufanya ama kuona mtu akifanya tiba flani mbadala kwa changamoto flani ya kiafya na ikafanikiwa, si mbaya tukishirikishana. Nitaanza mimi:

Tunaambiwa si vyema mama mjamzito kulala kitanda kimoja na mtoto mdogo hasa ujauzito ukiwa bado mchanga. Hii ni kweli. Iwe mtoto bado ananyonya ama ulishamwachisha.

Katoto kako kamefikisha miaka miwili na sehem ama mitatu ila bado unalala nako kitanda kimoja na sasa unahitaji kukaletea mdogo wake.

Ukibebe ujauzito halafu ukaendelea kulala na hako ka junior kitanda kimoja, hasa ukilala karibu nako, baada ya muda kataanza kudhoofika, joto la mwili kupanda, kukosa hamu ya kula, hivyo yani. Vihoma homa flani hivi vibaya.

Ukikapeleka hospitali mara nyingi utaambiwa hawaoni ugonjwa, ingawa kweli anaonekana anaumwa. Kwahyo watakushauri vya kukushauri.

Turudi sasa huku kienyeji. Pigo moja tuu litamrudisha mtoto katika hali ya usawa.

Kama scenerio imemtokea mtoto katika mazingira niliyoelezea hapo juu na umempeleka hospitali wakakwambia hawaoni ugonjwa, fanya hivi;

Usiku wakati wa kwenda kulala, andaa maji kwenye chombo cha wazi, beseni kwa mfano. Usiku huo utatakiwa kunyanduana na baba wa huyo mtoto. Hapa nieleweke. BABA WA HUYO MTOTO.

Mkishamaliza kunyanduana, mkasafishe nyeti zenu kwenye hayo maji uliyoandaa. Wote wawili wewe na baba wa huyo mtoi muosheè humo kwenye maji.

Zoezi la kuosha likisha kamilika, chukua hayo maji yaweke kwenye uvungu wa kitanda mnacholalia halafu mlale kwa Amani.

Asubuhi sana kabla jua halijachomoza, chukua yale maji mchukue na mtoto. Chota maji yale kidogo mpe mtoto anywe. Kisha nenda nae nje mlangoni umuoshe na yale maji. Sio lazima umuoshe na sabuni, alimradi tuu yamfikie mwilini, mwaili wote. Hakikisha wakati wa zoezi hili hakuna mtu anakuona.

Ukishamaliza kumuosha, mwaga maji huko huko nje, usirudi nayo ndani. Kisha utamkausha mtoto kama kawaida. Usimpake mafuta. Niamini, siku hiyo utaona mwenyewe hali ya mtoto inabadilika anaanza kuwa fresh.

Zingatia:
1. Tiba hiyo unafanya na Baba wa mtoto, ukifanya na mwanamme tuu mwingine inaweza kumdhuru mtoto. Madhara yake yanaweza kuwa serious zaidi ya unavofikiri.
2. Wakati wa kumuosha, hakikisha hakuna mtu anakuona. Ikitokea mtu kakuona, tiba hatofanya kazi. Hivyo utapaswa kurudia zoezi.
3. Acha kulala na huyo mtoto. Kama hauna namna ya kuacha kulala nae basi jitahidi usimkaribie wakati wa kulala. Unaweza kufanya hivo kwa kutafuta kitenganishi kati yako na yeye hapo hapo kitandani. Kama umeolewa, mume wako anaweza kulala kati kati yenu kuwatenganisha. Tatizo likijirudia, rudia tiba.
 
Back
Top Bottom