TWAWEZA: Asilimia 64 ya Watanzania waridhishwa na matumizi ya tozo

TWAWEZA: Asilimia 64 ya Watanzania waridhishwa na matumizi ya tozo

Niliandika humu na Naendelea kuandika Tena na Tena kuwa mh Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan anaeleweka vizuri Sana na mamillion ya watanzania, niliwambia kuwa watanzania wanamkubali Sana mh Rais, niliwaambia kuwa watanzania wanamuunga mkono mh Rais katika kuchangia kidogo kidogo kutokanaa na vipato vyetu ili kuijenga nchi yetu

Watanzania wameridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais wetu katika matumizi ya kila sent inayopatikana, watanzania wanaziona huduma zivyosogezwa karibu yao na kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma, watanzania wanafurahishwa na namna mh Rais wetu alivyo muwazi katika matumizi ya Fedha za umma, watanzania wanaimani kubwa Sana na mh Rais wetu katika usimamaizi wa fedha za umma na wanaona kuwa zipo katika mikono salama

Wananchi walio wengi wanasubili muda ufike tu ili akachukuliwe fomu ya kugombea Urais maana bado tuna muhitaji Sana mama yetu Katika Kuendelea kutuongoza na kututumikia, Tunaendelea kumwombea uzima na Afya njema
 
Ndio maana Magu huyu Wakuza sijui Jakuzi alimtia DISCIPLINE kwa upuuzi wake.

Kuna mtanzania anahitaji TOZO?
 
Hapo muamala umesoma halafu vinafuatia vichekesho kama hivi.
 
Hao Twaweza nao wamekuwa wajinga, hao wajinga wenzao waliowahoji wakaridhishwa na matumizi ya tozo waliwaokota wapi?

Utaridhishwaje na kitu usichoambiwa kimekusanywa kiasi gani kila mwezi, wala kuambiwa matumizi yake yatakuwa yapi?

Hawa wajinga wanatukosea heshima sana.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Shirika lisilo la Kiserikali la TWAWEZA East Africa limezindua ripoti ya matokeo ya utafiti mpya wa Sauti za Wananchi ulioangazia maoni na uzoefu wa Watanzania kuhusu hali ya taifa kati ya Oktoba 2021 na Julai 2022 ikiwa umejumuisha maoni na uzoefu wa wananchi kuhusu tozo za miamala ya fedha kwa njia ya simu.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa Wananchi walio wengi, takribani asilimia 64 wameridhishwa na matumizi ya mapato yatokanayo na miamala ya fedha kwa njia ya simu.

Katika matokeo ya takwimu yaliyotolewa ni asilimia 24 pekee ya Watanzania ambao wameeleza kuwa hawaridhiki na matumizi ya mapato yatokanayo na tozo za miamala huku asilimia 12 wakieleza kuwa hawana maoni.

Matokeo ya tafiti katika ripoti hiyo yameonesha utayari mkubwa wa watanzania kulipa kodi kwa hiari kwani tafiti zimeonesha kuwa karibu wananchi wote(asilimia 90) wanakubaliana na wazo la msingi, kwamba kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Huku takwimu hizo zikifafanua kuwa karibu wananchi wote (takribani asilimia 88) wanasema wangependa kulipa kodi bila shuruti, na wengine (asilimia 67) wanasema si vyema kuficha kipato ili kulipa kodi chini ya kipato na asilimia 63 ya wananchi wanasema ni wajibu wa wote kulipa kodi.

Vilevile wananchi wameonesha dalili kwamba wangeunga mkono zaidi tozo hizo iwapo wangekuwa na taarifa kamili za namna mapato yanayopatikana yanavyotumika, ambapo takribani asilimia 63 wanasema wangekuwa tayari zaidi kulipa ushuru kama wangefuatilia jinsi fedha zinavyotumika.

Huku asilimia 39 wakisema wanajua jinsi fedha hizo zinavyotumika na asilimia 44 wakieleza kuwa wanaweza kujua kwa urahisi kutoka serikalini matumizi ya fedha zilizokusanywa

Kwa upande mwingine tafiti hiyo inaonesha kuwa wananchi walio wengi(asilimia 67), wanakubali kwamba tozo ni njia muhimu ya serikali kupata mapato na kwamba inahakikisha kuwa kila mtu anachangia maendeleo ya taifa.

Huku asilimia 66 ya Wananchi walikubaliana na pendekezo kwamba tozo yenyewe siyo tatizo bali gharama za miamala zinazotozwa na watoa huduma.

Watuletee kwanza aina ya maswali yaliyoulizwa hadi kutoa matokeo hayo!
 
Ndio maana mwamba JPM alimshughurikia huyu Eyakuze na viutafiti vyake vya kibwege...
He is Useless indeed...
Wananchi wanalalamika yeye anakuja na hii takataka very Sad indeed...
 
Nadhani wana hoji familia zao ndio zinatoa hayo majibu..
 
Back
Top Bottom